PACHO HERRERA
JF-Expert Member
- Jul 23, 2018
- 460
- 527
Habarini za jioni...
Kwa muda mrefu sana, swala la ardhi hapa nchini limekuwa tatizo sugu..
Hii imepelekea kuibuka kwa migogoro mbalimbali na mafarakano katika jamii na wakati mwingine kusababisha hata maafa.
Katika mkoa wa morogoro kumeripotiwa visa vingi sana vinavyotokana na migogoro ya ardhi..
Kwa haraka haraka utagundua kwamba bado kuna shida kubwa sana katika ofisi nyingi za ardhi ambazo ni shida za kiutendaji ambazo kwa kiasi kikubwa zinasababisha migogoro hii..
Kwa upande wangu mimi ni mfanyabiashara nipo morogoro, na kwa kipindi kirefu ofisi hizi zimekuwa zikinikwamisha sana mambo yangu.
Moja ya biashara zangu ni kununua viwanja, kujenga na kuuza nyumba ama kuzipangisha..
Hapa ndo nilipokutana na mtihani mkubwa.
Unaenda kubadilisha jina la hati ya kiwanja baada ya kukinunua unazungushwa hata miezi sita, mara mafaili hayaonekani, mara sijui nini, mara hakuna mtandao, mara maafisa wameenda kufanya kazi field mwezi mzima, mara system ina shida mara kimeuzwa kwa watu wawili.. daaah tabu tupu..
Mwezi uliopita ndo nilichanganyikiwa kabisa,
Nilikua nafuatilia mkopo wangu benki fulani, nikawa nimeweka dhamana ya nyumba yangu mojawapo iliyopo wilaya mojawapo ya mkoa huu inayoanziwa na herufi 'k'..
Benki waliniambia nikalipie kiwanja changu (squatter) malipo ya kila mwaka ya kodi ya ardhi, bwaaaanaweee, shuhuli ikawa kwenye kupata control number
Yaani nimezunguka mwezi mzima hawanipi control number ya kulipia kiwanja changu..
Nimekaa mwezi mzima wanajizungusha, mara mfumo haupo, mara kimeenda kimerudi, mara access hamna mara sijui nini..
Mpaka benki wakaniona mzushi ikabidi wa-reject ombi langu na kunishauri nijipange kwa wakati ujao.
Ukiangalia nimekosa fusra kubwa maana nilishapata wapangaji wa kituruki ambao walikubali kupanga kwangu kwa mwaka mzima na walinipa masharti ya kurekebisha nyumba kwanza ( ndio maana nikaomba mkopo)
Muheshimiwa waziri, kwanza kitendo cha mimi kupata control number ili nilipie kiwanja changu, ni kuliingizia taifa kipato, sasa watu wako wanatunyima kuchangia pato la taifa. Wana majibu mabaya sana mpaka wanakera na muda mwinhine wanaficha mafaili makusufi ili tutoe hela za posho..
Hata 'official search' ambayo ni huduma ya bure wamekuwa wanatuchaji..
Muheshimiwa naamini kwa ujumbe huu utafanyia kazi na kutupa ahueni wananchi..
NAWASILISHA