Waziri Lukuvi aagiza Ekari 12700 Rukwa zirejeshwe Serikalini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,604
2,000
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa william lukuvi, ameagiza eneo ya lililokuwa shamba la mifugo la Malonje wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa lenye ukubwa wa ekari 12,750, lirejeshwe serikalini kwa vile utaratibu wa kuligawa umekiukwa kwa kiwango kikubwa, na masharti ya uendeshaji hayajazingatiwa kabisa.

Akiongea mjini Sumbawanga baada ya kulitembelea shamba hilo la Malonje, Waziri Lukuvi amesema utaratibu wa kugawa kwa kuuza vitalu vya shamba hilo la mifugo umefanyika bila ya kuzingatia sheria,hali ambayo imesababisha watu wamiliki maeneo hayo kienyeji bila ya hati yoyote,na kwa hali hiyo kuikosesha serikali mapato mengi yatokanayo na kodi ya ardhi,na kuagiza kila halmashauri ishughulikie eneo lake bila ya kuingiliana.


Aidha amesema kuwa juu ya mgogoro uliopo kati ya eneo la shamba hilo linalomilikiwa na mwekezaji na vijiji tisa vinavyolizunguka, ameiagiza serikali ya mkoa wa Rukwa kupitia kwa upya mipaka ya vijiji vyote tisa,ili kuondoa mgogoro mkubwa uliopo hivi sasa unaotishia amani iliyopo.ITV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom