Waziri Lugola amtimua Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa kwenye kikao kwa kuchelewa

Acha kuleta shangwe zako za ufipa. Hajatimuliwa. Kuna tofauti kati ya kutimuliwa na kufungiwa kutoingia kikaoni.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, amemfukuza kikaoni Kamishna Mkuu wa Magereza, Juma Malewa kwa kuchelewa.
Lugola amemfukuza Dk Malewa leo Julai 6, saa tano asubuhi ikiwa ni dakika chache baada ya kikao hicho kuanza.


Awali, Lugola alisema ikifika saa 5 kamili, mlango ufungwe na kama alivyoagiza, ulifungwa.
Ilipofika saa 5:1 mlango ulifunguliwa ili Dk Malewa aingie.
Baada ya kuingia Dk Malewa, Lugola akahoji kwa nini amefunguliwa mlango?


Licha ya Dk Malewa kuomba msamaha, Lugola alikataa kata kata. Pia Lugola ameagiza Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, kumshusha cheo hadi kubaki na nyota tatu, mkuu wa usalama barabarani, Mbeya, Leopold Fungu.


Pia ameagiza Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto mkoa wa Kagera, George Mrutu ashushwe cheo.
Kikao hicho ni cha kimkakati cha viongozi wa vyombo na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo.
Kaanza Kwa PUPA huyu Mzee, kitakacho kuja mpata hatokisahau.
 
Hii inaonesha ni kwa jinsi gani akili ndogo inatawala akili kubwa!! Eti Tanzania ya viwanda!! Labda vya kutotoa watoto!!

Kuanzia juu mpaka chini kuna watu wasiojua wanafanya nini au wafanye nini!!

Pole Tanzania kwa kukanyagwa na wajalaana ambao hata matumbo ya mama zao yanajuta kuwabeba!
 
Ndio maana JPM alisema anaweka waliopitia kazi sawa au za karibu ili wakafanye kazi vizuri kwa pamoja as maraia wa kawaida hawawezi..

Oyaaaa yangu macho na masikio kwa sasa
 
Lesser fare iishe ili watu wawe na adabu, wewe unaambiwa bosi anawahitaji kikaoni alafu unachelewa hadi mlango unafungwa ili iweje? waafrika tuna misuse sana time na kwa hili naunga sana mkono nchi nzima ngoma hii itafune
 
Time is money, kwa hiyo mkuu wa magereza amepishana na pesa. Tuheshimu muda, angetoa taarifa kabla ya kikao kuanza ili asaidiwe km atachelewa dakika moja. Mazoea mabaya sana, Lugola ataonekana mbaya lakini ukweli tunazembea sana kujali muda
 
Mweeeh hadi huruma sasa. Kuna uzembe sana kwenye jeshi la polisi, japo uhaba wa barabara mkoani Mbeya nao unachangia kwa kiasi kikubwa sana kutokea kwa ajali.Serikali lazima ikumbuke hili.
 
Back
Top Bottom