Waziri Lugola amtaka Kamishna Uhamiaji kutotoa kibali kwa Mtanzania yeyote anayeenda kufanya kazi nje ya nchi bila kujiridhisha

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemuagiza Kamishna wa Uhamiaji kutotoa kibali kwa Mtanzania yeyote kuondoka nchini kwa madai ya kupata kazi nje ya nchi bila kujiridhisha kuwa anayo mikataba ya sehemu anayokwenda kufanya kazi

Ametaka pia Kamishna wa Uhamiajia ajiridhishe kwa kufanya mawasiliano na Balozi husika katika nchi ambayo mtanzania huyo atadai anaenda kufanya kazi

Kauli hiyo ameitoa wakati wa shughuli ya maadhimisho ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu nchini jana Julai 30 katika viwanja vya Mnazi Mmoja

Pia amesisitiza kuwa Serikali haikatazi Watanzania kwenda kufanya kazi nje ya nchi bali kinachotakiwa ni kufuata utaratibu kutokana na nchi kuendelea kuathirika na watu kusafirishwa kiharamu na kwenda kuteswa

Aidha katika maadhimisho hayo, Waziri Lugola amemfuta kazi Mjumbe wa Sekretarieti ya kupinga usafirishaji Haramu wa binadamu kwa kushindwa kujua idadi ya vyombo vinavyotakiwa kutaifishwa

Ifahamike kuwa, Tanzania imefanya maadhimisho ya kupinga usafirishaji hafamu kwa binadamu kwa mara ya kwanza yakiwa yamebeba kauli mbiu ya "Tokomeza usafirishaji haramu kwa watoto na vijana kufanikisha uchumi wa Viwanda"
 
Ina maana walikua wanajitolea tu vibali?

Oh! Maagizo yake mangapi yameshatekelezwa tokea aingie madarakani?
 
Ukipata Visa ya Nchi unayokwenda maswali ya unaenda kufanya nini huko una kiasi gani yote yamejibiwa mpaka ukapata Visa kinachotakiwa ni kuangalia anaesafiri ndie mwenye Mkwaju huo na wazee wa kuzuia usafirishaji sumu uhamiaji mnapomzuia kumpa ruhusa mtu asafiri wakati Nchi husika wamekubali kwa kupitia ubalozi wao mnakosea na mnarudi nyuma sana kiutendaji...labda mtu awe anasafiri kwa Nchi ambazo tunagonga Visa tunapofika hapo kama Hong Kong,Singapore, South Korea,Cambodia na nyinginezo kujua anakwenda kufanya nini kule na wengi wanarudishwa kwa kukosa vigezo kinachotakiwa ninyi ni kutangaza vigezo kwa watalii,wafanyabiashara au wafanyakazi wanaoenda huko ili wasirudishwe airport zao ila kupiga Simu kwenye ubalozi anakokwenda mnaleta mlolongo usio na maana wakati wenzetu wanafanya jitihada za kupunguza ninyi ndio mnalala mkiamka mnaongeza sisi tutasafiri tuu maana kuna siku mtatoa Tangazo la kusitisha kutoa passport kwa Watanzania mpaka pale mtakapojiridhisha ndio mnakoenda huko...
 
Ajira zipo Dunia nzima,kila kona ya Dunia utakuta wakenya wapo na wanakuza uchumi kwa kufanya Kazi nje ya nchi, je sisi tukibanana hapahapa na Kazi hakuna, uchumi utakuwa?
 
Back
Top Bottom