Waziri Kombo: Tumestahimili mtihani mzito wa Oktoba 29, Dunia ikatuelewa

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameeleza kuwa diplomasia ya Tanzania imepita katika mtihani mzito zaidi tangu uhuru kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, lakini sasa nchi imerejea katika mstari baada ya kueleweka kimataifa.

Akizungumza leo, Januari 15, 2026, mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania katika hafla ya ‘Diplomatic Sherry Party’, Ikulu Chamwino, Balozi Kombo amekiri kuwa matukio ya uchaguzi uliopita yaliharibu taswira ya nchi duniani na kuzua maswali mengi kutoka kwa washirika wa maendeleo.

“Nilipokea simu nyingi na ujumbe wa maandishi wa kutia moyo na mshikamano kutoka kwa marafiki na washirika wetu wengi wa karibu. Baadhi walijumuisha wasiwasi pia, huku wengine wakiuliza nini kimeipata Tanzania, nchi inayojulikana kama kitovu cha amani kwa miaka 64 iliyopita katika kanda hii tangu uhuru wake. Wengine waliwasilisha ujumbe wao kupitia njia za kidiplomasia kwako Mheshimiwa, huku baadhi isivyo bahati wakitumia majukwaa na maeneo yasiyo rasmi”, amesema Balozi Kombo.

Waziri huyo amebainisha kuwa chini ya maelekezo ya Rais Samia, Wizara ilifanya kazi ya ziada kufafanua ukweli wa mambo kwa kutumia ushahidi katika miji mikuu ya dunia hatua iliyosababisha nchi kueleweka. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) umekubali kutoa nafasi ya uponyaji kupitia Tume ya Uchunguzi (Inquiry Commission) iliyoundwa na Rais, ambayo itafuatiwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa.

Balozi Kombo amesisitiza kuwa mbinu ya "4R" (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya) ya Rais Samia imekuwa nguzo muhimu katika kurejesha imani ya jumuiya ya kimataifa, huku akibainisha kuwa kila sauti ya upinzani au wasiwasi ilisikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati muafaka.
 
Asamehewe tu, kwa kuwa anajua atendalo ni uongo.
 
Wanaujua uwezo wake, ndiyo maana wanamdanganya kiurahisi, kama yule aliyemdanganya kuwa eti atamleta Mange kwenye mahakama bandia za Tanzania.

Tena waendelee kumdanganya hivyo hivyo. Halafu aanze kusafiri nje, akiwa huko nje, ndipo arrest warrant itoke, na achukuliwe huko huko. Wamdanganye kuwa mambo yameisha, wampe mwaliko, halafu wamdake huko huko.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameeleza kuwa diplomasia ya Tanzania imepita katika mtihani mzito zaidi tangu uhuru kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, lakini sasa nchi imerejea katika mstari baada ya kueleweka kimataifa.

Akizungumza leo, Januari 15, 2026, mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania katika hafla ya ‘Diplomatic Sherry Party’, Ikulu Chamwino, Balozi Kombo amekiri kuwa matukio ya uchaguzi uliopita yaliharibu taswira ya nchi duniani na kuzua maswali mengi kutoka kwa washirika wa maendeleo.

“Nilipokea simu nyingi na ujumbe wa maandishi wa kutia moyo na mshikamano kutoka kwa marafiki na washirika wetu wengi wa karibu. Baadhi walijumuisha wasiwasi pia, huku wengine wakiuliza nini kimeipata Tanzania, nchi inayojulikana kama kitovu cha amani kwa miaka 64 iliyopita katika kanda hii tangu uhuru wake. Wengine waliwasilisha ujumbe wao kupitia njia za kidiplomasia kwako Mheshimiwa, huku baadhi isivyo bahati wakitumia majukwaa na maeneo yasiyo rasmi”, amesema Balozi Kombo.

Waziri huyo amebainisha kuwa chini ya maelekezo ya Rais Samia, Wizara ilifanya kazi ya ziada kufafanua ukweli wa mambo kwa kutumia ushahidi katika miji mikuu ya dunia hatua iliyosababisha nchi kueleweka. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) umekubali kutoa nafasi ya uponyaji kupitia Tume ya Uchunguzi (Inquiry Commission) iliyoundwa na Rais, ambayo itafuatiwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa.

Balozi Kombo amesisitiza kuwa mbinu ya "4R" (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya) ya Rais Samia imekuwa nguzo muhimu katika kurejesha imani ya jumuiya ya kimataifa, huku akibainisha kuwa kila sauti ya upinzani au wasiwasi ilisikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati muafaka.
aendelee kujidanganya tu
 
Watu wa namna hii ndiyo waliolifikisha taifa kwenye shida hiyo ya MO29.
Wanampa taarifa za kuongo ili mradi hizo taarifa ziwe za kumfurahisha boss wao.
Wampe taarifa halisi ili atafute jinsi ya kuzitatua changamoto husika. Wanauingiza matatizoni bibi wa watu.
 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameeleza kuwa diplomasia ya Tanzania imepita katika mtihani mzito zaidi tangu uhuru kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, lakini sasa nchi imerejea katika mstari baada ya kueleweka kimataifa.

Akizungumza leo, Januari 15, 2026, mbele ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania katika hafla ya ‘Diplomatic Sherry Party’, Ikulu Chamwino, Balozi Kombo amekiri kuwa matukio ya uchaguzi uliopita yaliharibu taswira ya nchi duniani na kuzua maswali mengi kutoka kwa washirika wa maendeleo.

“Nilipokea simu nyingi na ujumbe wa maandishi wa kutia moyo na mshikamano kutoka kwa marafiki na washirika wetu wengi wa karibu. Baadhi walijumuisha wasiwasi pia, huku wengine wakiuliza nini kimeipata Tanzania, nchi inayojulikana kama kitovu cha amani kwa miaka 64 iliyopita katika kanda hii tangu uhuru wake. Wengine waliwasilisha ujumbe wao kupitia njia za kidiplomasia kwako Mheshimiwa, huku baadhi isivyo bahati wakitumia majukwaa na maeneo yasiyo rasmi”, amesema Balozi Kombo.

Waziri huyo amebainisha kuwa chini ya maelekezo ya Rais Samia, Wizara ilifanya kazi ya ziada kufafanua ukweli wa mambo kwa kutumia ushahidi katika miji mikuu ya dunia hatua iliyosababisha nchi kueleweka. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa (UN) umekubali kutoa nafasi ya uponyaji kupitia Tume ya Uchunguzi (Inquiry Commission) iliyoundwa na Rais, ambayo itafuatiwa na mchakato wa maridhiano ya kitaifa.

Balozi Kombo amesisitiza kuwa mbinu ya "4R" (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga Upya) ya Rais Samia imekuwa nguzo muhimu katika kurejesha imani ya jumuiya ya kimataifa, huku akibainisha kuwa kila sauti ya upinzani au wasiwasi ilisikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati muafaka.
Huyu Kombo ni mpumbavu sana
 
Wanasema mama kaletewa summons akihitajika na Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai (ICC)
Hawana taarifa kuwa Dunia ilisha tuelewa 😀😀😀
Kamanamuona vile Kitima na jamaa zake walivyo vimba kwa hasira😄😄
 
Sifa kuu ya baadhi ya wanasiasa ni uongo na ulaghai.

Wao husema "siwapigi busu watoto kuwasalimu au kuonyesha upendo bali nawaibia pipi zao".
 
Back
Top Bottom