Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
Waziri Kombo Apokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Comoro kwa Niaba ya Rais Samia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amepokea ujumbe maalum wa Rais wa Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Azali Assoumani uliowasilishwa na Katibu wa Rais na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, katika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza baada ya kupokea ujumbe huo, Mhe. Kombo amemshukuru Mhe. Mohamed Ali kwa kufikisha ujumbe huo ambapo amehaidi kuuwasilisha kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haraka iwezekanavyo.
“Ninakushukuru sana Mhe. Youssoufa Mohamed Ali kwa kufikisha ujumbe huu muhimu kwa Rais wetu, na labda niweke bayana tu kuwa Mheshimiwa Rais Samia ameelezea kufurahishwa na uamuzi wa Comoro kuichagua Tanzania kama mshirika katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Muungano wa Visiwa vya Comoro yatakayofanyika Moroni, tarehe 6 Julai, 2025” alisema Mhe. Kombo.
Aidha, Mhe Kombo amesema katika kipindi cha nusu karne, uhusiano kati ya Tanzania na Visiwa vya Comoro umeendelea kuimarika na kuonesha mafanikio katika nyanja za kisiasa, kijamii, na kidiplomasia, huku fursa mpya zikijitokeza kupitia mikakati ya maendeleo ya kikanda na ushirikiano wa kimataifa.
Kwa upande wake, Katibu wa Rais na Waziri wa Ulinzi wa Umoja wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake katika kukuza uhusiano wa pande mbili kati ya Tanzania na Comoro na kutoa kipaumbele katika kuimarisha diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kikanda katika biashara na uwekezaji.
Kikao cha makabidhiano ya ujumbe huo kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Visiwa vya Comoro nchini Tanzania, Mhe. Dkt. El Badaoui Mohamed, na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.