Waziri Kombo ahitimisha ziara nchini China

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
Waziri Kombo ahitimisha ziara nchini China

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amehitimisha ziara yake ya kikazi nchini China iliyofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 19 Juni, 2025.

Akiwa nchini China, Mheshimiwa Waziri Kombo aliongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Mawaziri wa kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (Forum on China-Africa Cooperation-FOCAC Coordinators Meeting) uliofanyika jijini Changsha katika jimbo la Hunan kuanzia tarehe 11 hadi 12 Juni 2025 na kushiriki hafla ya uzinduzi wa Maonesho ya Nne (4) ya Kimataifa ya Biashara kati ya China na Afrika yaliyofanyika tarehe 13 hadi 15 Juni, 2025 katika jiji hilo.

Pembezoni mwa mkutano huo, Waziri Kombo pia alifanya mazungumzo na Mheshimiwa Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) na Waziri wa Mambo ya Nje wa China kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kimkakati kati ya Tanzania na China.

Aidha, katika muendelezo wa ziara yake Waziri Kombo pia alitembelea katika jiji la Shenzhen, Guangzhou, Beijing na Chengdu ambapo alikutana na viongozi wa Serikali wa miji hiyo pamoja na kampuni kubwa za uzalishaji wa bidhaa na huduma nchini China ikiwemo kampuni ya ER-Kang, HUAWEI, China Electronic Company, Fangda, CADFund, China Development Bank, China Railway Construction Corporation (CRCC) na kampuni ya Shudao. Mikutano hiyo ililenga kuimarisha na kuongeza ushirikiano wa kidiplomasia na kisiasa, na kuhamasisha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na China.

Kadhalika, Waziri Kombo alitembelea Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Guangzhou na kuzungumza na watumishi wa kituo hicho. Vilevile, alikutana na Watanzania waishio katika jiji hilo ambao aliwasisitiza kuchangamkia fursa za kiuchumi sambamba na kueleza umuhimu na mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Kombo atatufaa AWAMU ya Saba 2030-2040. Shukran Jazilan
 
Mabox ya kura yashaletwa
 
Back
Top Bottom