Waziri Kombani Ndani Ya Sakata La Jerry Muro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Kombani Ndani Ya Sakata La Jerry Muro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Superman, Feb 24, 2010.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Wanabaraza;

  Leo nimesikia katika udondozi wa magazeti kupitia redio kuwa Waziri Celina Kombani yuko ndani ya Sakata la Jerry Muro.

  Mwenye taarifa zaidi atujuze.

  ===============================


  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete akimwapisha Waziri mpya wa Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Celina Kombani Ikulu Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo. (Picha na Mroki Mroki).
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  wewe ulisikia nini?
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Boss, kama nilivyoandika ilikuwa ni undondozi wa magazeti Radio One Stereo walisoma kichwa cha habari tu. Sikuwahi kusikia ni gazeti gani.

  Kuna mahali nilisoma siku za nyuma kuwa katika laptop ya Jerry kulikuwa na kumbukumbu zilizokuwa zinamhusisha waziri moja mabaye inasemekana alinunuliwa gari na kusaidiwa mambo mengine ya kibiashara, lakini haikutajwa ni waziri gani.
   
 4. W

  WildCard JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa kwenye gazeti la MwanaHalisi. Ni yaleyale tunayoyapigia kelele humu ya mawaziri kutafuna taasisi zilizo chini ya wizara zao.
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,944
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo Selina Kombani
  ametafuna pesa za taasisi ipi?
  kuweni specific kidogo.
   
 6. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katika habari ya wali gazeti lilisema kuwa yule mhasibu aliyesimamishwa na Pinda kule bagamoyo alikuwa na mawasiliano ya karibu sana na Waziri mmoja na huyo waziri hakutajwa katika gazeti lile. hivyo leo ndiyo katajwa. Habari ya awali ilikuwa inaonyesha kuwa mhasibu amemfanyia mambo mengi sana waziri husika. ( Nimeeleza nilivyoelewa na sijanukuu)
   
 7. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mfwatiliaji
  Naamini wewe unazo habari zote ya awali na hii, tusaidie kuweka kumbukumbu sawa hapa.
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,812
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Hiyo story iliandikwa na Raia Mwema

  http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2037

  bila kumtaja jina na sasa MwanaHalisi wameambua kumtaja jina.


  Waziri ndani ya sakata la Muro

  Mwandishi Wetu
  Februari 10, 2010

  [​IMG]Achunguzwa kwa mahusiano na waliotimuliwa Bagamoyo

  WAZIRI Mwandamizi katika serikali ya Rais Jakaya Kikwete, anahusishwa na sakata lililomsibu Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, na sasa uchunguzi dhidi yake unaendelea, Raia Mwema limefahamishwa.

  Habari za ndani ya Serikali zimeeleza kwamba vyombo vya dola vimeshitushwa na taarifa za kuhusika kwa waziri huyo ambaye taarifa zake zimekutwa kwa Muro na wenzake wawili Edmud Kapama na Deogratias Mgasa.

  Kwa mujibu wa habari hizo, vyombo vya dola vilipowapekua na kuwahoji Muro na wenzake vilipata ushahidi wa waziri huyo kuwa na ‘mahusiano’ na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, waliotimuliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

  Waliotimuliwa madarakani na Pinda ni Mkurugenzi Mtendaji Rhoda Nsemwa; Mweka Hazina, Michael Karol Wage; Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Naftal Rhemtullah; Ofisa Mipango, Aloyce Gabriel na Mkaguzi wa Ndani, Abdul Mwinyi.

  “Jerry Muro na wenzake walikutwa na ushahidi unaoonyesha kwamba waziri (anamtaja jina) alikuwa akinufaika na fedha za ubadhirifu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Walikuwa na ushahidi wa gari ambalo Waziri huyo amenunuliwa na liko Morogoro katika sehemu ya biashara zake,” kinaeleza chanzo cha habari serikalini.

  Raia Mwema limefahamishwa kwamba vyombo vya dola kwa pamoja sasa vinachunguza jinsi waziri huyo (jina tunalo) alivyonufaika na fedha kutoka halmashauri hiyo ya Bagamoyo na sababu za mmoja wa watumishi hao kutoa fedha kwa waziri huyo.

  “Unajua wanaangalia mahusiano kati ya Waziri huyo na mmoja wa watumishi waliofukuzwa kazi na Waziri Mkuu, maana lazima Serikali ijiridhishe walitoa fedha kwake kwa maslahi gani na kama wana mahusiano ya binafsi, kibiashara ama ya kikazi kabla ya kuchukua maamuzi na pia kina Muro na wenzake walizipataje hizo taarifa na walikuwa wanazitumia kwa malengo gani,” anaeleza Ofisa Mwandamizi serikalini.

  Mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe wa mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Jerry Muro na wenzake wawili walishtakiwa kwa pamoja, wiki iliyopita, kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 toka kwa Mweka Hazina wa Wilaya ya Bagamoyo, Wage, aliyefukuzwa kazi hivi karibuni na Waziri Mkuu kwa ubadhirifu.

  Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Boniface Stanslaus akiwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Benny Lincoln wamedai mahakamani hapo kwamba mshitakiwa wa kwanza na wa pili pia wanakabiliwa na shitaka la kujipachika wadhifa ambao si wao.

  Inasemekana January 29, 2010 katika hoteli ya Sea Cliff washtakiwa walijitambulisha mbele ya Wage kuwa wao ni maafisa wa TAKUKURU wakati si kweli.

  Mapema mwaka huu, Waziri Mkuu, Pinda, aliwavua madaraka viongozi watendaji hao wakuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, kwa kutowajibika ipasavyo na kutozingatia kanuni za fedha na ameteua wapya.

  Pinda alitangaza uamuzi huo mjini Bagamoyo mwanzoni mwa mwaka huu kwenye mkutano na viongozi na watendaji wa Halmashauri hiyo, akiwa Waziri mwenye dhamana ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

  Aliwavua madaraka watendaji wakuu hao kwa kutumia kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na kusema hatua nyingine za kinidhamu zitafuatia kadri itakavyoonekana inastahili.

  Baada ya kuwavua madaraka watendaji hao, aliwateua Samuel Saiyanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Halmashauri hiyo, akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Fidelis Nenetwa kuwa Mweka Hazina, akitokea Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

  Wengine walioteuliwa ni Fidelica Myovelo, kuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Iringa; Felista Masamba kuwa Mkaguzi wa Ndani akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na Prudence Mtiganzi kuwa Mhandisi wa Maji akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

  Alisema uamuzi wa kuwapumzisha watendaji hao unatokana na mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Septemba na Oktoba mwaka jana.

  Uchunguzi wa Mdhibiti ulitokana na tuhuma za ukiukwaji wa kanuni za fedha, uzembe wa kufuatilia utekelezaji wa miradi na ubadhirifu katika Halmashauri hiyo.

  Ripoti hiyo ilibainisha ukiukwaji mkubwa wa kanuni za fedha, uzembe na kushindwa kuwajibika na matokeo yake kuzorota kwa miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.

  Waziri Mkuu alisema pamoja na kuwa hatua hizo zimechukuliwa kwa Bagamoyo, halmashauri zingine nchini zikae chonjo na zitashughulikiwa kwa kuwa nazo zina matatizo yanayofanana na ya Bagamoyo.
   
 9. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli, ndani ya CCM hamna asiye msafi. hata Pinda amelidhihirisha hilo kwa aliyoyatamka Igunga.
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,935
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Leteni data wadau!
   
 11. J

  Jafar JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani - mwenye nondo /data aziangushe hapa
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,935
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  DUH kweli wadanganyika tunaliwa, Mamaaaaaaaaaa
   
 13. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  "Jerry Muro na wenzake walikutwa na ushahidi unaoonyesha kwamba waziri (anamtaja jina) alikuwa akinufaika na fedha za ubadhirifu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo. Walikuwa na ushahidi wa gari ambalo Waziri huyo amenunuliwa na liko Morogoro katika sehemu ya biashara zake," kinaeleza chanzo cha habari serikalini.

  Raia Mwema limefahamishwa kwamba vyombo vya dola kwa pamoja sasa vinachunguza jinsi waziri huyo (jina tunalo) alivyonufaika na fedha kutoka halmashauri hiyo ya Bagamoyo na sababu za mmoja wa watumishi hao kutoa fedha kwa waziri huyo.


  "Unajua wanaangalia mahusiano kati ya Waziri huyo na mmoja wa watumishi waliofukuzwa kazi na Waziri Mkuu, maana lazima Serikali ijiridhishe walitoa fedha kwake kwa maslahi gani na kama wana mahusiano ya binafsi, kibiashara ama ya kikazi kabla ya kuchukua maamuzi na pia kina Muro na wenzake walizipataje hizo taarifa na walikuwa wanazitumia kwa malengo gani," anaeleza Ofisa Mwandamizi serikalini.

  Source: Mwandishi Wetu; Raia Mwema; Februari 10, 2010
  https://www.jamiiforums.com/celebrities-forum/51642-tbc-journalist-jerry-muro-held-over-alleged-graft-115.html
   
 14. W

  WildCard JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Wachunguzeni Mawaziri wote. Mtakuta hali ni hiyohiyo. Uwaziri ni dili bwana. Asikudanganye mtu.
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,115
  Likes Received: 2,412
  Trophy Points: 280
  Huyu mama yaani huwezi kumdhania!
   
 16. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na umdhaniae ndie siye!
   
 17. J

  Jafar JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Duuu hhh
  The lady (Celina) looks so innocent.
  Lisemwalo .......na kama halipo.......
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Ohh..naona mnakumbuka shuka usubuhi..Ndo maana kila siku nasema humu, wadanganyika wengi mnategemea kuvuna madafu kwa kupanda chelewa.

  Kaaz kwelikweli.
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  SMU,
  Umdhaniae ndiye mara nyingi anakuwa siye. Mawaziri wanazitafuna kwelikweli taasisi zilizo chini ya wizara zao. Hali ni hiyohiyo kwa mawaziri wengi tu. Ni ufisadi ambao umejificha kidogo. Tuliowahi kuwa watumishi wa umma tunaufahamu sana. Nashangaa TAKUKURU wanakomalia posho za wabunge wanauacha huu unaotafuna mamilioni.
   
 20. W

  WildCard JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Tumeyasema sana humu. Sema huu ni mfumo uliokomaa sana. Ulianzishwa na CCM kuchangiwa na taasisi za UMMA. Hamjawahi kushtukia utajiri mawaziri wetu unatokana na nini muda mfupi baada kushika nyadhifa hizi? Mchezo huu pia unazikumba PCCB, TISS ndio maana ni vigumu mno kuudhibiti.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...