Waziri kivuli ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kivuli ni nani?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mumwi, May 22, 2011.

 1. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2011
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wajameni naomba mnisaidie katika nchi yetu nimekuwa nikisikia hiki cheo cha waziri kivuli nasema hivyo ni baada ya kusoma na kuona runinga zikisema kuwa kuna mbunge mmoja wa chama fulani kutoka mkoa fulani kwenda kuchochea vurugu, na inajulikana kuwa ni mbunge G. Lema ndio alikuwa Tarime pia G. Lema ni waziri kivuli wa mambo ya ndani je cheo cha waziri kivuli hakina uzito wowote?
   
 2. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hao ni vyombo vya habari - makanjanja-. waziri kivuli ana kazi nzito ya kufuatilia majukumu yaliyo katika wizara yake ili aweze kuibusha uhalisia na kuipa changamoto serikali hususan waziri muhusika kuhusiana na yanayojiri katika wizara hiyo. Vyombo vya habari vinafikiri ni uchochezi kuifurahisha serikali ya ccm, wapate mradi wao.
   
 3. t

  tumpale JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 201
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hivyo vyimbo vya habari waandishi wake ni makanjanja ndo maana hawajui nafasi ya waziri kivuli, kwani kama wangepitia darasani nadhani wangefundishwa maana na majukumu ya waziri kivuli.
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Katika mfumo wetu wa siasa unatulazimu kuwa na serikali kivuli ambayo kazi yake ni kurekebisha pale serikali inapokosea, lakini pia serikali inapowajibika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake basi hii kivuli inaweza kushika serikali wakati wa mpito. Hii iko kisheria na inatambulika hao wanao kengeusha uhalisia ni waandishi walio kula vya watu na si wakweli
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mi hapa sitachangia kwa swali lako,ila nusu waziri Kagasheki asubiri aone impact ya uyo mbunge mmoja wa chama kimoja. Kesi ya Tarime ni nzito usivofikiria. Haitoshangaza Mabere Marando na Tundu Lissu kungurumisha kesi nzito dhidi ya serikali na hatimaye wauaji kuhukumiwa adhabu ya kifo na pia fidia kubwa kwa wafiwa. Ikumbukwe kwa nguvu za mbunge uyo mmoja wa chama kimoja alizuia maiti5 za wahanga kuzikwa mpaka jumatano inayokuja. Pia wafiwa wameipa cdm majukumu yote ya vifo ivo. Tundu Lissu naye ndani ya Tarime sasa Kagasheki atakuwa anasema "Wabunge wawili,wa chama kimoja". Subiri uone nguvu ya cdm!!
   
 6. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  WAZIRI kivuli anasifa zote za waziri husika,kinachotofautisha ni statutory autonomous kati ya watu hawa wawili.Waziri husika toka chama tawala ndiye wengi humwona anathamani sana kuliko shadow minister while its wrong.
  So,vyombo vya habari hasa hivi vya chama/Tbc/uhuru/almuur n.k vinafanya kazi ya kudhoofisha upinzani kwa njia yoyote,kitu ambacho hakipo.Makanjanja sana mavyombo ya hapa kwa Tz.
   
Loading...