Waziri kivuli Chadema aachia ngazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri kivuli Chadema aachia ngazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jun 13, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  WAZIRI Kivuli wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), na Mbunge wa Viti Maalumu Chadema, Leticia Nyerere amejiuzulu wadhifa huo.Hatua ya kujiuzulu kwa mbunge huyo imekuja kipindi kisichozidi miezi minne tangu kuundwa kwa baraza hilo katika Mkutano wa Bunge la Februari.

  Taarifa za kujiuzulu kwa Nyerere zilivuma kuanzia jana mchana huku Spika wa Bunge Anne Makinda, akisema anasubiri taarifa za uteuzi kutoka kwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

  Akizungumza kwa simu jana jioni, Nyerere alithibitisha kujiuzulu akisema hatua yake ni uamuzi aliouita wa kidemokrasi kwani unalenga kutoa fursa kwa wengine kuongoza. Hata hivyo, hakutoa sababu za kuchukua hatua hiyo. Alisema Chadema kina wabunge 48 wakati nafasi za mawaziri ni 18 ukiacha manaibu, hivyo ameamua kuwapa nafasi wengine wapate uzoefu.

  My Take: Nini hasa kimemsibu huyu mbunge mpya kuna mwenye fununu?
   
Loading...