Waziri KITWANGA alipoikubali CHADEMA mbele ya hadhara....

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,488
14,355
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga juzi alilazimika kutumia salamu za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili kuwashawishi wanafunzi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) waweze kumsikiliza.

Kitwanga alilazimika kukikubali japo kwa muda Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kutokana na hatua ya wanafunzi wa chuo hicho kuguna kila alipoitaja ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi wakati akizungumza nao kuhusu inavyotekeleza sera ya elimu.
Waziri huyo alilazimika kuwasalimia wanafunzi hao akisema "CHADEMA hoyee!!, na ukumbi mzima ulizizima kwa mayowe na vifijo vya wanafunzi waliopaza sauti zao wakimjibu "Oyeeee" huku kila mmoja akimpungia alama ya vema kwa kuonyesha vidole viwili. Kitendo cha Waziri Kitwanga kutumia jina la CHADEMA katika kibwagizo hicho kilitokana na hatua ya wanafunzi hao kuguna pale alipoanza kujibu maswali yao kwa kusema "katika Ilani ya ya CCM….." bila kumalizia kusema alishtushwa na miguno

source: Tanzania Daima
 
Walianza kuiga elimu bure sasa wanatumia JINA............... Na bado ipo siku watahamia kabisa
 
Salamu hizo, zimfikie na Mh Makamba, na Tambwe Hiza. Huo ndo ukweli jamaa wameonyesha itikadi yao wazi wazi. Huo ndo ujumbe kuelekea 2015.

Ni wazi kuwa wapigakura wa ccm wanazidi kupungua huku wale wa CDM wakizidi kuongezeka. 2015 mmh sijui, nadhani ni vema ccm wakaanza kupaki maana safari imeiva
 
Hii habari ni njema na nadhani Marope na ndugu yake Hiza ujumbe umefika kuwa hawawezi kuzuia mvua isinyeshe. Chadema ni kama mvua wametanda kwa wingu zito muda sio mrefu mvua rasmi itashuka sasa wenye baiskeli za udongo(thithiem) wameanza kuhaha.
 
Back
Top Bottom