Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Abas Abdullahi Sheikh Siraji, hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia, kwani alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland.
Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi, huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa viongozi.
Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo, tayari wamekamatwa.