Waziri Kelemani na serikali mlitudanganya wananchi,mgao wa umeme ni mkubwa na hamtaki kuutangaza,kwanini msiwajibike??

isupilo

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
303
1,254
image.jpeg

Mwaka 2015 August,hii serikali ya CCM ilituahidi kufikia September Mosi,tatizo la mgao wa umeme litakuwa historia.Kupitia Waziri wa wakati huo Simbachawene tuliambiwa kuwa mgao utakuwa mwisho sababu mradi wa Kinyerezi Two utakuwa umekamilika.

Mpaka sasa uwongo huu wa serikali ya CCM imeendelea kutudanganya,na bado kuna watu walipokuwa Kinyerezi wakasema mradi huo unakamilika muda mfupi toka walipoenda.Serikali hii inavunja kanuni za "Social Contract",tuliwapa kura ili watupe huduma bora za jamii,lakini ni usanii mtupu.

Sasa kuna mgao mkubwa wa umeme,maeneo ya jiji la Dsm kwa mfano,umeme ulikatwa toka jana saa sita usiku na haujarudi mpaka sasa,kuna maeneo umeme umekatwa asubuhi na sehemu zingine umeme umekatwa mchana.

Huyu Mbunge wa Chato na Waziri wa Nishati anatoka mbele ya waandishi,anamfukuza kaimu meneja wa Kidatu na anasema Watendaji wanafanya hujuma,meneja kaondoka lakini umeme bado ni mgao mkubwa sana.Waziri anakataa kutangaza mgao wa umeme,lakini mpaka sasa tunaona mgao mkubwa sana.

Hivi hawa wanasiasa wanataka nini?kwanini tunadanganyana?mwingine anaita nyufa ndio "expansion joint",mwingine hataki kusema kuna mgao,na wengine wanasema wanaoenda kwa hao waongo eti sababu wanatekeleza sera za maisha bora,hivi nyie mwatuona sisi wajinga??

Waziri Kelemani,tunaomba utangaze mgao,na kwa sababu ulisema hakuna mgao na sasa kuna mgao,kwanini usiachie hiyo ofisi??Tunachezeana sana akili nyie wanasiasa
 
Ni vizuri watangaze tu na watupe ratiba ya huo mgao tujipange, sio mtu unanunua samaki wako biashara halafu umeme unakuwa haupo kutwa nzima samaki wanakuozea.
 
Ni vizuri watangaze tu na watupe tu ratiba ya huo mgao tujipange, sio mtu unanunua samaki wako biashara halafu umeme unakuwa haupo kutwa nzima samaki wanakuozea.
Na waanaufunika mgao wa umeme kwa kununja wanaisiasa ili kupoteza malalamiko na manung'uniko ya tatizo la umeme
 
Kalemani....
Angekuwa anatoka Kaskazini labda ndo angeondoka..
 
Kimya ,usiwe unazambaza habari za uwongo utanyimwa dhamana
 
Kuwajibika na kutumbuliwa hakuwahusu wakolomije Mkuu.
 
Back
Top Bottom