' Waziri Kawambwa Umepewa nini na Wahindi?' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

' Waziri Kawambwa Umepewa nini na Wahindi?'

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by MziziMkavu, Sep 12, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mojawapo ya mabango ya wafanyakazi wa shirika la reli Tanzania walioko kwenye mgomo Tuesday, September 08, 2009 9:25 PM
  Maneno hayo ni miongoni mwa maneno yaliyoandikwa kwenye mabango ya wafanyakazi wa shirika la reli Tanzania ambao wako kwenye mgomo wa malipo yao wakati walipokutana na Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa. Picha za mabango ya wafanyakazi hao mwisho wa habari hii. Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawambwa alipokolewa na nyimbo na mabango ya kumkebehi wakati alipojitokeza kukutana na wafanyakazi wa shirika la reli nchini TRL ambao wanaendeleza mgomo wao wa malipo kwa siku ya sita sasa.

  Waziri Kawambwa alipokelewa mabango yaliyokuwa yakisema "Kawambwa Wahindi wamekupa nini", "Hii ni serikali ya India au Tanzania", "Hatutaki siasa tunataka pesa" na bango jingine lilisema "Kupewa mshahara tarehe 38 Inauma".

  Wafanyakazi wa shirika hilo la reli ambalo hivi sasa limeingia ubia na shirika la reli la India, walisema kuwa wataendelea na mgomo wao mpaka watakapolipwa pesa zao.

  Waziri Kawambwa alifika kwenye mkutano na wafanayakazi hao wa TRL huku akipewa ulinzi wa hali ya juu wa askari wengi wenye silaha nzito pamoja na mbwa.

  Kawambwa aliwataka wafanyakazi hao warudi kuendelea na kazi kama kawaida na huku madai mengine yakiendelea kushughulikiwa kwakuwa hali hiyo ya mgomo inawaathiri watumiaji wa huduma hiyo.

  Aliwataka wafanyakazi hao kuwa wavumilivu kwa kuwa Serikali tayari imeshamuita Mkurugenzi Mtendandaji wa kampuni ya Rates, Vinay Agrawal kuzungumza nae juu ya uendeshaji mbovu wa shirika hilo na haitasita kuuvunja mkataba ukibainika kuwa umeshindwa kuboresha huduma hizo.

  Alisema kuwa serikali imeshachoshwa na uendeshwaji mbovu wa shirika hilo na kwa sasa inachukua hatua za kuangalia hatua kwa hatua kuangalia mikataba ya kampuni hiyo na itakuwa tayari kuuvunja endapo watabaini kuna matatizo.

  Mgomo huo umewaathiri zaidi abiria wa shirika hilo ambao wamekwama katika stesheni mbalimbali nchini pamoja na kurudishiwa nauli zao kwani nauli zao walizorushiwa hazijitoshelezi kutafuta usafiri mwingine kuendelea na safari zao.


  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3034674&&Cat=1
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Sep 12, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  KIKWETE AMEMPA HUYU BWANA KAZI WIZARA HII KWA UNDUGU TU, UKWELI NI KWAMBA HAIWEZI!! KUTHIBITISHA HILO MPAKA LEO HII AMEIKALIA ILE RIPOTI YA TUME ALIOIUNDA JUU YA atcl NA KUWAPA ULAJI RAFIKI ZAKE; LAKINI MPAKA LEO HII HAJAIWEKA HADHARANI!! AMEWEKWA WIZARA HII ILI AKAMILISHE KUJENGA MIUNDOMBINU ZIKIWEMO BARABARA KUELEKEA MAKASILI YA MUUNGWANA HUKO MSOGA!!
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mhh!!!!, huyu tutamlaumu bure, ikiwa ripoti zote zilizotolewa na tume zilizoundwa kuchunguza madhambi yote yaliyofanyika wahusika hawajachukuliwa hatua stahili, unategemea hii ripoti itoke? na hata ikitoka hakuna la zaidi ila porojo zataendelea tu. Mkuu wa nchi mwenyewe anashindwa kuwachukulia hatua waliotajwa kwenye ripoti ambazo alisha kabidhiwa, unategeme nini kwa huyu waziri
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Sep 12, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..tatizo hii nchi inategemea sana uwezo wa kiutendaji wa Raisi.

  ..the system of checks and balance is very weak.

  ..tukiendelea kuchagua maraisi wasio na uwezo msitegemee Mawaziri wake watakuja kumuokoa.

  NB:

  ..huyu Kawambwa kasoma vizuri tu. haiyumkiniki kwamba kazi ya uwaziri tena wa fani aliyoisomea umshinde. msije mkashangaa akaondoka hapa akaenda zake Namibia/Botswana/Rwanda halafu akafanya maajabu huko.
   
Loading...