Ndugu,
Viongozi nao ni raia wa nchi hii na wana HAKI ya kumiliki migodi. Madini ni rasilimali ya WATANZANIA (including hawa viongozi) wote.
Migodi ni kama biashara yoyote ile, pato lake linaingia kwenye mfuko wa Taifa kupitia KODI. Naona tunataka kwenda kwenye enzi ambayo mtu akijituma na kujitahidi kujipatia riziki yake kupitia MIGODI awe adui wa nchi.
Hao wanaolalamika hawajui hata jinsi ya kutafuta claim na kumiliki mgodi. Huo ni uvivu wa fikra...Jitumeni Wajameni.
ES,
right on point bro.....enough with "do nothingism" mindset. Kama CCM wote wangekuwa kama wewe basi gurudumu la maendeleo lingekuwa kileleni saa hii....enough is enough, ili tufanikiwe inabidi partisan politics ziende likizo!!!.
Kwa hiyo kesho kukigundulika mgodi wa dhahabu wenye kukisiwa una dhahabu ya thamani ya $100 billion na kuambiwa mgodi huo mwenye nao ni Yussuf Manji hakuna tatizo! kukigundulika mafuta Tanzania na ikisemwa kwamba visima vya mafuta vyenye kukisiwa kuwa na mafuta ya thamani ya $1,000 billioni na mwenye navyo ni Manji hakuna tatizo!
Hivi sisi wabongo ni lini tutaacha kuwa wadanganyika!? rasilimali ya Watanzania wote leo mtu kwa kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu na kinachopatika hapa ni changu badala ya kuwa pato la Taifa na bado kuna baadhi yetu wanaona hilo ni sawa tu! Duh! bado tuna safari ndefu kweli kweli!
Ndio Hakuna Tatizo! "kukigundulika" - kumbuka wenye kutaka kufanya biashara hizi hufanya utafiti wa kina kujua wapi kunafaa kuchimbwa na kurudisha gharama. Hakuna "kukigundulika". Ondoa mawazo haya na fanya utafiti zaidi.
Sawa ameshagundua...kuna sheria zinazofuatwa ili kuhakikisha nchi inafaidika na ugunduzi na mradi wake. Umesema "kutumia wadhifa wake anasema hili eneo ni langu..." - kuna sheria za umilikaji wa migodi mzee. Mimi naona WEWE bado una safari ndefu, huwezik kupigania haki yako kama hujui hata haki yako ni nini.
Jaribu kufanya utafiti zaidi kabla ya maneno uliyoyasema hapo juu. Ungeweza kupendekeza nini kiongezwe/kirekebishwe katika sheria ya umilikishwaji wa migodi etc lakini ni wazi huelewi hata sheria zilizopo zinasema nini.
Kwani Manji akifuata sheria na akamiliki....na....akapata hela....na akalipa kodi. Kuna ubaya gani? JFYI opponent wake Manji anamiliki migodi mingi tu Tanzania, lakini hii sio ishu.
Kiswahili kinakuwa tatizo hata kwa waswahili wenyewe... WAZIRI KAPUYA AIBIWA! mbona taarifa nilizonazo ni kuwa waziri Kapuya leo kapelekwa India kwa matibabu zaidi sasa ataibiwa vipi naomba ufafanuzi hapo..
Kilichoibwa ni hivyo vitu sio waziri...
Teh teh teh teh
Kwa hiyo wewe Tanzania kukigundulika mafuta yenye thamani ya $1,000 billioni na visima hivyo vikiwa owned na Manji badala ya serikali huoni tatizo lolote! ama kweli mvunja nchi ni mwananchi! Huyu huyu manji baada ya kuuza magodown yake kwa shilingi 47 billioni hadi hii leo hataki kulipa kodi ya shilingi 1.3 billion leo unamtegemea awe na visima vya mafuta halafu awe tayari kulipa kodi!
Mimi haki ninayopigani ni haki ya Watanzania wote ili na wao wawe na kiwango cha maisha ya kuridhisha na hili linawezekana kabisa kama viongozi wakiacha ulafi na ubinafsi wa kujilimbikizia mali. Inakuwaje watu wawe na migodi inayowaingizia mabilioni ya pesa na wakati huo huo asilimia kubwa ya Watanzania wakiishi katika maisha ya dhiki kubwa. Hawajui hata mlo wao mwingine utatoka wapi. Hawajui kodi ya pango wataitoa wapi, hawajui m(wa)toto wao watamsomesha vipi kwa kuwa hawana uwezo wa kumudu gharama za shule, hawajui wakiugua watapata wapi fedha za kujitibu na kununua dawa.
Hakuna haki yoyote ya raia mmoja kumiliki mgodi au migodi ya madini! Hebu wewe unayejua sheria ziweke hizo sheria hapa za watu binafsi kumiliki migodi ili tuzichambue tuone kama zimeweka maslahi ya Watanzania mbele. Nina maswali yafuatayo kwako. Je sheria ya kuruhusu mtu binafsi kuown mgodi ilitungwa mwaka gani? Iliandikwa kwenye govt gazette? Je alinunua mgodi huu kwa kiasi gani na ni nani aliyepanga bei ya mgodi huo? Je mapato nayoyapa anaandika mahesabu (financial statements) kuonyesha kila mwaka amepata mapato kiasi gani, je mtu ambaye hana wadhifa serikalini ana nafasi sawa na kiongozi wa siri kali au CCM kupata mgodi au ndio yale yale ya kujilimbikizia mali, kutoa rushwa na ufisadi wa hali ya juu ambapo mtu wa kawaida hana uwezo wa kuown mgodi? Na huyo waziri analipa kodi inayostahili kwa mfuko wa Taifa au mapato yote anayatia mfukoni bila mfuko wa taifa kuambuliya chochote? Lete hizo sheria kama unavyozifahamu ili tuzichambue. Hakuna haja ya kuandikia mate wakati wino tunao.
Kiongozi kama alivyo mtanzania mwingine ana haki ya kuwa na miradi ya kumuongezea kipato. Cha msingi muhukumu kwa kutumia influence ya madaraka kukiuka taratibu za biashara au mradi husika, na si kumhukumu kuwa na mradi huo.
Utajiri hauji kwa vikundi, isipokuwa kutumia fikra na jitihada binafsi katika kufikia malengo yako, leo ukisubiri miradi ya watu ikuletee maendeleo yako binafsi, utakufa maskini. Nani wa kumfanyia kazi mwingine?
Hivi leo tunataka mtu ambaye ameingia madarakani akiwa na miradi yake binafsi inayompa pesa nyingi, aiuze au agawe mali zake hizo? Mambo hayawezi kwenda namna hiyo.
Kama mtu kawekeza kwenye mafuta yakagundulika kuwa na hifadhi kubwa, unataka serikali iutwae huo mradi? Unakumbuka yaliyotokea kwenye azimio la Arusha? Hicho ndo kilichofanyika, miradi ikafa hatimaye wakaingiza wanachoita UBINAFSISHAJI.
Kama kuna kampuni au mtu halipi kodi, huo ni udhaifu wa mamlaka zetu. Ni mara ngapi tumesikia nchi za watu watu wakifilisiwa au mali zao zikiuzwa kwa kukwepa kodi? Tukifikia hatua hiyo, watu watakuwa wanapeleka wenyewe kodi kabla hawajafatwa.
Na ndo hapo dhana ya kutengeneza mabilionea itafanikiwa, watatoa ajira kwa wengi na huenda nawe "Bubu ataka kusema" na wengine watajikuta maisha yamekuwa bora. Kwani kwa Mengi kuwa na pesa wangapi wamefanikiwa kuwa na maisha bora? Wengi tu! Tukiwa na watu kama hao laki moja, TUTAENDELEA.
Kiongozi kama alivyo mtanzania mwingine ana haki ya kuwa na miradi ya kumuongezea kipato. Cha msingi muhukumu kwa kutumia influence ya madaraka kukiuka taratibu za biashara au mradi husika, na si kumhukumu kuwa na mradi huo.