Waziri Kamwelwe afurahishwa na uwekezaji hoteli ya Ngurdoto

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Waziri wa ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amepongeza uwekezaji mkubwa unaofanywa katika hoteli ya kifahari ya Ngurdoto iliyopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha ambao unaendelea kuchochea dhana ya uchumi wa viwanda.

Ameyasema hayo leo Mkoani Arusha katika Mkutano Mkuu wa 30 wa Wahandisi kutoka Tanzania unaoendelea katika hoteli hiyo.

Amesema kuwa,uwekezaji ambao uliachwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa hoteli hiyo, Hayati Melau Mrema umezidi kuendelezwa na kuchochea kukua kwa uchumi katika sekta ya maliasili na utali ndani na nje ya nchi.

Kamwelwe amesema kuwa,uongozi imara ulioachwa na Hayati Mrema umekuwa ni chachu ya kuendeleza uchumi wa viwanda kama ilivyo kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano.

Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali kuiga mfano huo wa kuendeleza rasilimali ambazo zimekuwa zikiiachwa na wawekezaji ambao wametangulia mbele ya haki na baadaye kupotea .

Hoteli ya Ngurdoto ni hoteli kubwa katika Mkoa wa Arusha ambayo hivi sasa inasimamiwa na mtoto mkubwa wa Hayati bilionea Mrema, Johan Mrema akishirikiana na Meneja wake Beatrice Dallaris ambao wamekuwa wakihakikisha rasilimali hiyo inaendelea kuchangia pato la taifa.

1768630132.jpeg


IMG_20191205_095915_7.jpeg


IMG_20191205_095544_2.jpeg
 
Back
Top Bottom