Waziri Jenista Mhagama aifuta leseni ya Wakala wa Ajira Pepsi

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,681
39,012
Wanaukumbi.

Waziri wa Ajira, Kazi, Sera na Bunge, Jenista Mhagama amefuta leseni ya wakala wa ajira wa Kampuni ya SBC Tanzania, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji vya Pepsi jijini Mwanza baada kukiuka Sheria ya ajira na uhusiano kazini.Pia, ameiamuru kampuni hiyo kumlipa kila mfanyakazi Sh50,000 kama faini ya kutokuwa na vifaa vya usalama kazini na kutotekeleza taratibu na sheria zilizowekwa na Idara ya Usalama na Afya Kazini (OSHA).

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mwanza, pia alitoa siku 14 kwa kampuni hiyo kukamilisha vifaa vyote vinavyohitajika kwa wafanyakazi pamoja na kuwalipa stahiki zao. Mhagama alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kiwanda cha Pepsi na kukuta wafanyakazi 50 hawana vifaa hivyo. “Nafuta kibali cha wakala wa ajira hapa kama utahitaji kuendelea na kazi hiyo uje wizarani ili kuomba upya,” alisema Mhagama.

Wakizungumza leo, baadhi ya wafanyakazi hao walisema wanasafisha kreti moja ya soda yenye chupa 24 kwa Sh100 na kwamba, ikitokea wakavunja chupa hutakiwa kulipa. Katika hatua nyingine, Mhagama alimtaka Mkurungezi wa Kiwanda cha Samaki cha Vickfish cha mjini hapa, kumlipa stahiki Yunis Marko kwa kufanya kazi bila kulipwa haki zake kwa mwaka mzima.

Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema ajira 35,000 zilizalishwa mwaka jana mkoani humo. Ofisa Kiongozi wa Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi wa Migogoro ya Kazi (CMA) mkoani Mwanza, Ephraim Lusega alisema kesi 566 za kazi ziliripotiwa kuanzia Januari mwaka jana hadi Desemba na 96 zilisuluhishwa au kuamriwa
 
huyo mkuu wa mkoa alikuwa wapi mpka Jenista anachukua hatua, Jpm hebu fanya yako kama kawaida kwa wakuu wa mikoa walio mizigo maana hizi kero kwa wananchi zimezidi.
Mulongo yupo ili kupambana na cdm mwanza
 
Nivema lakini viwanda vingi vinamatatizo kamahayo,nivema aje na mkakati na usimamiwe na wakuu Wa mikoa. Ni namnagani viwanda vinapaswa kujali haki za watumishi wake na vinaendeshwa vipi.
. Pia kula gereji kubwa za magari vijana wanakata mikono kila kukicha na kisha wanafukuzwa bila msaada ss waziri ataweza kuzungukia kote hko?
 
Mh Waziri, hapo bado hujatatua tatizo, hizo job agency zinazooperate tanzania zimulikwe zote, na ikiwezekana vibali vyote vya job agency vifutwe na masharti mapya yawekwe na kusimamiwa na serikali yenyewe ipasavyo, hizi job agency zinanyonya watanzania na kuwatumikisha kama mambwa.. kuna job agency zinamilikiwa na wahindi hapa yaani ni full unyonyaji na ubabe,, pia mh Waziri jitahidi kwenye hizi sekta kusiwepo kabisa na job agency Madini,mafuta na gas, ajira zifanywe na makampuni yenyewe. Kuna job agency pia za wakenya mh Waziri ni full kuleta wakenya bila kujali wazawa au bila kuangalia kuwa wanaoperate tanzania...
 
Kwa mtazamo mdogo ni.kwamba amehangaikia kijipu kidogo sana maana malalamiko ya aina hiyo mengi sana. Tanzania yetu malalamiko ni mengi sana na hakuna mahala sijaaikia malalamiko ya hao wafanyakazi hasa private sector, kila mahala kilio na mateso. Mara wafukuzww bila kulipwa stahili, vifaa vya kazi, wakiugua hakuna huduma nk. Hasa hao wahindi.ni.ahida tupo. Kwingine napo viwanda na sehemu mbalimbali walipo wachina. Serikali imulike pote.
 
Wanaukumbi.

Waziri wa Ajira, Kazi, Sera na Bunge, Jenista Mhagama amefuta leseni ya wakala wa ajira wa Kampuni ya SBC Tanzania, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji vya Pepsi jijini Mwanza baada kukiuka Sheria ya ajira na uhusiano kazini.Pia, ameiamuru kampuni hiyo kumlipa kila mfanyakazi Sh50,000 kama faini ya kutokuwa na vifaa vya usalama kazini na kutotekeleza taratibu na sheria zilizowekwa na Idara ya Usalama na Afya Kazini (OSHA).

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mwanza, pia alitoa siku 14 kwa kampuni hiyo kukamilisha vifaa vyote vinavyohitajika kwa wafanyakazi pamoja na kuwalipa stahiki zao. Mhagama alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kiwanda cha Pepsi na kukuta wafanyakazi 50 hawana vifaa hivyo. “Nafuta kibali cha wakala wa ajira hapa kama utahitaji kuendelea na kazi hiyo uje wizarani ili kuomba upya,” alisema Mhagama.

Wakizungumza leo, baadhi ya wafanyakazi hao walisema wanasafisha kreti moja ya soda yenye chupa 24 kwa Sh100 na kwamba, ikitokea wakavunja chupa hutakiwa kulipa. Katika hatua nyingine, Mhagama alimtaka Mkurungezi wa Kiwanda cha Samaki cha Vickfish cha mjini hapa, kumlipa stahiki Yunis Marko kwa kufanya kazi bila kulipwa haki zake kwa mwaka mzima.

Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema ajira 35,000 zilizalishwa mwaka jana mkoani humo. Ofisa Kiongozi wa Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi wa Migogoro ya Kazi (CMA) mkoani Mwanza, Ephraim Lusega alisema kesi 566 za kazi ziliripotiwa kuanzia Januari mwaka jana hadi Desemba na 96 zilisuluhishwa au kuamriwa
Wanasiasa huwa wanatutajia idadi ya ajira kumbe ajira zenyewe ndo huwa za kipuuzi kama za hao wahindi,mti anafanya kazi mwaka mzima na humpi pesa yake
 
Ktk mawaziri ninawakubali uyu mama yumo
Huyo mama juzi kaenda kiwanda cha bora,wafanyakazi wanamwambia 'Hapa tunaitwa Kondoo weusi' na wahindi,huyo mhindi mpaka leo sijamsikia akifanywa lolote,na wafanyakaz walilalamika mbele yake,ndo ubaguzi wenyewe huo,me niliisoma hiyo habari kwenye MWANANCHI
 
Nampongeza waziri kwa kutuma meseji kali kwa wakala zote nchini. hata hivyo nashauri amulike wakala hizo ili na yanayotokea ktk sehemu nyingine ya nchi nayo yakome!
 
huyo mkuu wa mkoa alikuwa wapi mpka Jenista anachukua hatua, Jpm hebu fanya yako kama kawaida kwa wakuu wa mikoa walio mizigo maana hizi kero kwa wananchi zimezidi.
Bado tena jana kapewa 48 hrs na naibu waziri Luhanga Mpina ajieleze kwanini mwanza ni chafu?
 
Wanaukumbi.

Waziri wa Ajira, Kazi, Sera na Bunge, Jenista Mhagama amefuta leseni ya wakala wa ajira wa Kampuni ya SBC Tanzania, watengenezaji na wasambazaji wa vinywaji vya Pepsi jijini Mwanza baada kukiuka Sheria ya ajira na uhusiano kazini.Pia, ameiamuru kampuni hiyo kumlipa kila mfanyakazi Sh50,000 kama faini ya kutokuwa na vifaa vya usalama kazini na kutotekeleza taratibu na sheria zilizowekwa na Idara ya Usalama na Afya Kazini (OSHA).

Akizungumza wakati wa ziara yake katika Mkoa wa Mwanza, pia alitoa siku 14 kwa kampuni hiyo kukamilisha vifaa vyote vinavyohitajika kwa wafanyakazi pamoja na kuwalipa stahiki zao. Mhagama alitoa maagizo hayo jana alipofanya ziara katika kiwanda cha Pepsi na kukuta wafanyakazi 50 hawana vifaa hivyo. “Nafuta kibali cha wakala wa ajira hapa kama utahitaji kuendelea na kazi hiyo uje wizarani ili kuomba upya,” alisema Mhagama.

Wakizungumza leo, baadhi ya wafanyakazi hao walisema wanasafisha kreti moja ya soda yenye chupa 24 kwa Sh100 na kwamba, ikitokea wakavunja chupa hutakiwa kulipa. Katika hatua nyingine, Mhagama alimtaka Mkurungezi wa Kiwanda cha Samaki cha Vickfish cha mjini hapa, kumlipa stahiki Yunis Marko kwa kufanya kazi bila kulipwa haki zake kwa mwaka mzima.

Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Magesa Mulongo alisema ajira 35,000 zilizalishwa mwaka jana mkoani humo. Ofisa Kiongozi wa Kituo cha Usuluhishi na Upatanishi wa Migogoro ya Kazi (CMA) mkoani Mwanza, Ephraim Lusega alisema kesi 566 za kazi ziliripotiwa kuanzia Januari mwaka jana hadi Desemba na 96 zilisuluhishwa au kuamriwa
Mbona ameingilia utendaji wa osha?ninavyojua adhabu hiyo ilibidi itolewe na osha kama wafanyakazi wanafanya kazi ktk mazingira hatarishi na kuna adhabu zake, awache kukurupuka
 
Hawa wakuu wa mkoa waliowekwa na mzee wa msoga kwa maslah ya chama s watendaji hawana professional yoyote ndiyo maana madudu yanaonekana kwa mawazir yaan jk aliharibu sana hii nchi
 
Serikali inatakiwa na jicho kwa kila shughuli za uzalishaji na huduma ambazo zinahusu kuajiri raia wake. Serikali ikikaa mbali na waajiri wanajifanyia wanavyotaka.
Hicho alicholifanya Waziri Mhagama ni sahihi na ileweke hilo ni tone tu la maji kwenye bahari.
Waende mbali zaidi na zaidi. Wakala wa Kazi ni mere middle men wanaonufaika na mishahara ya wafanyakazi wanaojidai kuwatafutia Kazi. Kwani Waajiri hawawezi kutangaza na watu kuomba kama zamani.
Huenda ni mpango wa serikali wa kuwatafutia Kazi watu lakini kwa utaratibu huo bora wabadilishe. Kazi zote zitangazwe
 
Back
Top Bottom