Waziri George Mkuchika unamdanganya nani?

Waziri George Mkuchika unamdanganya nani?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
7,189
Reaction score
9,807
Jana Waziri George Huruma Mkuchika, Waziri katika Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za Wabunge wa Upinzani na CCM kuhsu watu kutekwa, kupotezwa au kushambuliwa mchana kweupe na Mwandishi wa Habari Bwana MUSIBA anavyotoa matamko ya KICHOCHEZI lakini TISS wamekaa kimya.

Waziri katika kama kawaida ya Serikali ya CCM Kajibu hoja zote kisiasa na propaganda nyingi zenye kupotosha. Kwa kifupi niseme alichofanya Mkuchika ni KUJIBU HOJA NZITO KWA MAJIBU MEPESI,YA KITOTO NA YENYE KUPOTOSHA.

Mkuchika anawatetea TISS au UWT(Usalama wa Taifa) kwamba ATI TISS HUFANYA KAZI ZAO KIMYAKIMYA NA KUSHAURI SERIKALI NINI CHA KUFANYA. Huu ni uongo wa mchana kweupe. Usalama wa Taifa ya sasa kiukweli hawa ni USALAMA WA CCM na Serikali yake. TISS wako kutetea CCM na kukandamiza, kuonea, kunyanyasa na kuua Wapinzani kwa MASLAHI YA CCM NA SERIKALI YAKE.!!!

Kama kweli TISS wanafanya kazi kwa weledi unaostahili kama TISS ya enzi za Baba wa Taifa tusingelikuwa tunasikia upuuzi unaofanyika kwa sasa hapa Tanzania. Watu wameuawa huko Kibiti kwa karibu mwaka mzima na TISS wapo tu. Watu wakihoji kwanini watu wanauawa Waziri Daktari uchwara Nchemba anasema INAWEZEKANA CHADEMA wanahusika maana haiwezekani watu wa chama fulani(CCM) peke yao ndio wanauawa lakini Upinzani hawauawi...!!!Je, TISS walikuwa wapi kujua kuwakamata hao CHADEMA au CUF au ACT-Wazalando ili dunia ijue kwamba kumbe vyama vya upinzani ni vyama vya KIGAIDI??

Wakati Mkuchika anadanganya watu kwamba UWT wanaendelea kufanya kazi zao kimyakimya, i hali halisi ni tofauti kabisa na kinachotokea kwenye eneo la tukio.. Kuna Polisi 8 huko Kibiti na mpaka leo hatujui nani walihusika..?TISS wanafanya kazi kimyakimya.....Kuna mwandishi Azory Gwanda ametoweka kutoka eneo la tukio(KIBITI) akiandika habari za Kiuchunguzi kuhusu Mauaji hayohayo na mpaka leo zaidi ya siku 100 Gwanda hajaonekana....LAKINI TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA...!!

Kuna Ben Saanane ametoweka huu ni mwaka wa pili na haijulikani yuko wapi na nani aliyemteka. Watu wakihoji wanaambiwa waulizwe CHADEMA maana wanajua alipo...??TISS wapo tu wanaendelea kufanya kazi kimyakimya...!! Tundu Lissu kashambuliwa kwa Risasi zaidi ya 30 kwenye maeneo ya Bunge tena Makazi ya Viongozi wa Serikali na Waheshimiwa Wabunge mpaka leo hakuna hata sisimizi wa kusingiziwa amekamatwa....TISS WAPO WANAENDELEA KUFANYA KAZI YAO KIMYAKIMYA......!!!

Mwanafunzi wa NIT kauawa kwa kupigwa risasi na Polisi waliokuwa wanataka kuwazuia/kuwaua Viongozi wa CHADEMA waliokuwa wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Kinondoni kuadai Viapo vya Mawakala kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi...Leo Viongozi wa CHADEMA ndo wanaambiwa wanahusika na kifo cha Acqulina Akwiline.....Kwa maana nyingine Mbowe na wenzake ndio walifyatua risasi za kumwua Acqulina....Polisi waliokuwa na silaha za moto , Kamanda Mambosaasa aliyaamrisha Polisi wafyatulie risasi za moto watu wasiokuwa na hatia na Mkurugenzi wa Kinondoni hawahusiki kabisa kwa lolote....TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA....!!!

Kwa Waziri Mkuchuchika na CCM watu kuendelea kupotea, kuuawa, kushambuliwa na wapinzani kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kesi za hovyohovyo ndiyo UTAWALA BORA wa CCM na Serikali yake huku TISS au UWT wakiende;ea kufanya kazi kimyakimya......!!!

Hitimisho ni kwamba TISS wataendelea kufanya kazi zao kimya kimya huku wakiendelea kupanga mikakati ya kuwapoteza, kuwashambulia au kuwamaliza kabisa Viongozi wote wa Upinzani kimya kimya maana ndiyo kazi ya TISS kwa sasa na huo ndiyo utawala bora...!!!
 
Kuwepo Kwa watu kama musiba kila siku anamwaga upupu na akina wale wanatafutia watu kesi za uongo ati Mchungaji fulani kazaa na Yule ati Baba Huyu ni Mzazi wa Huyu hiyo ni ishara tosha kuwa taasisi adhimu kama TISS zimepigwa ganzi na wanasiasa
 
Unaweza ukawa na Hoja ila Mimi ukinithibitishia tu ' Kimantiki ' kwamba TISS ipo nyuma ya yote haya nitakuamini zaidi.

Come on man.....!!!
Mungu amekupa akili, ufahamu na busara za kupambanua mambo. Usiwe kama dodoki ambalo likitumbukizwa kwenye maji linazoa kila uchafu/taka zilizomo majini. Let me ask you a simple question? Kwa akili yako ambayo ni finyu unafikri hawa WATU WASIOJULIKANA WANAOFANYA HUU USHENZI WAO KIMYAKIMYA NA HAWAKAMATIKI NI KINA NANI HASA? Ukinipa jibu la swali hili basi utakuwa umepata mantiki ya kwanini tunasema TISS wako nyuma ya yote haya yanayofanyika kimyakimya kwa maelekezo ya kina Mkuchika...!!Over n Out.
 
Come on man.....!!!
Mungu amekupa akili, ufahamu na busara za kupambanua mambo. Usiwe kama dodoki ambalo likitumbukizwa kwenye maji linazoa kila uchafu/taka zilizomo majini. Let me ask you a simple question? Kwa akili yako ambayo ni finyu unafikri hawa WATU WASIOJULIKANA WANAOFANYA HUU USHENZI WAO KIMYAKIMYA NA HAWAKAMATIKI NI KINA NANI HASA? Ukinipa jibu la swali hili basi utakuwa umepata mantiki ya kwaini tunasema TISS wako nyuma ya yote haya yanayofanyika kimyakimya kwa maelekezo ya kina Mkuchika...!!Over n Out.

Acha ' Upumbavu ' tafadhali na sioni unachohamakia ( panic ) ni nini halafu huwa nawapendeni mno Watu wenye ' mihemko ' ya Kipuuzi kama nyie ili niwateseni vizuri Kisaikolojia hadi mchoke. Bado narudia tena kukuuliza tena kwa jeuri zote huku nikijiamini kwamba naomba unipe ' uthibitisho ' wako wa Kimantiki kabisa kwamba TISS ipo nyuma ya mambo yote mabaya uliyoyataja hapa Tanzania. Sihitaji maelezo yako mengi kwani yamejaa tu ' Pumba ' ila nataka tu uende moja kwa moja katika ' vivid facts ' zako ili wenye ' akili ' sawasawa tukuamini na tukuelewe.

Nakusubiri.
 
Mwanzoni nilikuwa na wasiwasi juu ya yanayoendelea nchini. Nilifikiri kuhusu theory 2.
1. TISS are behind all that is taking place in our country na ipo kwenye kujivua Gamba(Wanauana wenyewe kwa wenyewe kuondoa masalia ya waliopita wabaki wale wanaounga mkono waliopo)! Sikuipa Sana nguvu theory hii!
2. Kuna KUNDI Nje ya System lililoamua kuwanyang'anya TISS Majukumu yao na kuwa paralyse kabisa wazee wa kitengo. Kwamba kundi hili nje ya TISS linamilikiwa na WALIOPO, wanaotaka kulazimisha Matakwa yao na wasio tayari kuzuiliwa na TISS! Baadae theory hii ilipata nguvu zaidi baada ya kumsoma CHAHALI kuhusu ROGUE!
Itoshe tu kusema, INAWEZEKANA MKUCHIKA AKAWA SAHIHI (endapo dhana ya Pili ina ukweli), na INAWEZEKANA akawa si sahihi endapo dhana ya Kwanza ina ukweli!

Huu Ni Mtazamo wangu tuuu, nakubali kukosolewa na kutukanwa pia!
 
Mkuchika na yey anafikiri anavyozid kujipendekeza ndio atazid kuwa imara.
 
Acha ' Upumbavu ' tafadhali na sioni unachohamakia ( panic ) ni nini halafu huwa nawapendeni mno Watu wenye ' mihemko ' ya Kipuuzi kama nyie ili niwateseni vizuri Kisaikolojia hadi mchoke. Bado narudia tena kukuuliza tena kwa jeuri zote huku nikijiamini kwamba naomba unipe ' uthibitisho ' wako wa Kimantiki kabisa kwamba TISS ipo nyuma ya mambo yote mabaya uliyoyataja hapa Tanzania. Sihitaji maelezo yako mengi kwani yamejaa tu ' Pumba ' ila nataka tu uende moja kwa moja katika ' vivid facts ' zako ili wenye ' akili ' sawasawa tukuamini na tukuelewe.

Nakusubiri.

GENTAMYCINE,

No panic no nothing but only facts....!Let me say this..YOU ARE FOOLISH TO BEGIN WITH...!!! Rejea maandiko yako niliyo ya-highlight kwa ''RED'' hapo juu...!
Wenye akili wanajua ninacho kiongea na kwa taarifa yako wewe huwezi kuwa ni mmoja kati ya watu wenye akili...Never ever.. na Mungu akuhurumie. Watu husema heri uwe maskini wa MALI kuliko kuwa maskini wa AKILI....Sasa wewe ni maskini wa AKILI na ninachelea kusema Mungu kakunyima akili na mali pia...!!!

Kama unataka ''vivid facts'' kama unavyodai nenda kamwulize Babu yako George Mkuchika au nenda Ikulu kwa JPM wanajua vizuri sana nani WANAO HUSIKA NA MAMBO HAYA MABAYA YANAYOENDELEA KUIKUMBA NCHI YA TANZANIA KWA AWAMU HII....TANGU TUPATE UHURU! Mkuchika kasema TISS wanafanya kazi zao KIMYAKIMYA na hawataki kuwa wazi, na WATU WASIOJULIKANA WALIOKO NYUMA YA MAMBO HAYA MABAYA nao wanafanya kazi zao KIMYAKIMYA na mpaka sasa HAWAJULIKANI......!!!
Remember this: TISS(UWT) = WATU WASIOJULIKANA . Kama huamini na kuelewa kwa sasa....there is a day you'll come to understand this..!!
 
Unaweza ukawa na Hoja ila Mimi ukinithibitishia tu ' Kimantiki ' kwamba TISS ipo nyuma ya yote haya nitakuamini zaidi.
Kwa akili tu za kawaida acha za shule wewe unaamini hawapo nyuma ya yanayoendelea? Na kwa uwezo wako wa kupima mambo na uzoevu ulio nao pamoja na exposure kubwa ya kukaa karibu na marais wa nchi nyingine na mashushu mbalimbali bado tu huwaoni kwenye haya matukio? Naamini unajua lakini kwa masharti ya kazi yako na unayemtumikia aidha kwa kiapo au vyovyote basi umeamua kujifanya hujui lolote! Nakuheshimu.
 
Mi nafikir hujamuelewa yeye kasema tiss wapo nyuma ya haya matukio chukulia kwa mfano yule aliemuonesha nape bastola je alichukiliwa hatua gani? nae yule ataitwa mtu asiejulikana? itoshe tu kusema jamaa wanavuunda sana ktk mipango yao yule wa kwa nape picha ipo kubwa tu anaonekana hamorapa na kitenge walimuona macho kwa macho kwa nini serikali ikane?
 
Ukiisikiliza tone ya mkuchika katika aya zilizohusu tiss na watu wasiojulikana ipo flat kwa maana ya kuwa anakisema asichokitaka na hakina ukweli! Ana kigugumizi cha ghafla ambacho kinaashiria kuwa anadanganya! Sijabahatika kumwona usoni na posture ya kichwa chake na mwili kwa ujumla ambapo ningemsoma zaidi. Kimsingi ameongopa na nafsi yake inamuuma kiuhalisia!
 
Kwenye upuuzi unaoendelea hapa nchini, kuna mambo matatu yanawezekana, moja TISS kama taasisi inahusika, mbili kuna unit ndogo ndani ya TISS inahusika na operations zao ni wachache wenye clearance ya kuzijua hivyo sehemu kubwa wako gizani na kwa kawaida huwezi kupeleka pua yako kwenye vitu ambavyo hauna clearance navyo. Na tatu TISS kama taasisi hawahusiki ili wao kama taasisi wamefeli kwa kiasi fulani kudhibiti matukio ya kipuuzi yanayoendelea kwa muda wote huu, hata kama hawatangazi mafanikio kusingekua na upumbavu unaoendelea sasa.
Ili ufanikishe tukio kama lile la kushambuliwa lisu na kwa mahali lilikofanyikia, kuna vitu vingi sana vinahitajika ambavyo unavipata tu ukiwa ndani ya system hivyo ni wazi kuna unit yenye resources za kutosha ndani ya system inayofanya kazi chafu. Ila imejaa viazi watupu
 
GENTAMYCINE,

No panic no nothing but only facts....!Let me say this..YOU ARE FOOLISH TO BEGIN WITH...!!! Rejea maandiko yako niliyo ya-highlight kwa ''RED'' hapo juu...!
Wenye akili wanajua ninacho kiongea na kwa taarifa yako wewe huwezi kuwa ni mmoja kati ya watu wenye akili...Never ever.. na Mungu akuhurumie. Watu husema heri uwe maskini wa MALI kuliko kuwa maskini wa AKILI....Sasa wewe ni maskini wa AKILI na ninachelea kusema Mungu kakunyima akili na mali pia...!!!

Kama unataka ''vivid facts'' kama unavyodai nenda kamwulize Babu yako George Mkuchika au nenda Ikulu kwa JPM wanajua vizuri sana nani WANAO HUSIKA NA MAMBO HAYA MABAYA YANAYOENDELEA KUIKUMBA NCHI YA TANZANIA KWA AWAMU HII....TANGU TUPATE UHURU! Mkuchika kasema TISS wanafanya kazi zao KIMYAKIMYA na hawataki kuwa wazi, na WATU WASIOJULIKANA WALIOKO NYUMA YA MAMBO HAYA MABAYA nao wanafanya kazi zao KIMYAKIMYA na mpaka sasa HAWAJULIKANI......!!!
Remember this: TISS(UWT) = WATU WASIOJULIKANA . Kama huamini na kuelewa kwa sasa....there is a day you'll come to understand this..!!

Bado naona ' Upumbavu ' wako tu. Ulipokuwa Shuleni au Chuoni ulisoma Somo la Communication Skills na ukalielewa vyema? Ulikuwa mzuri pia katika kufanya ' Summary ' ya Content? Unatumia nguvu nyingi sana kujibu kitu kidogo mno. Nakuuliza tena naomba unionyeshe ' Kimantiki ' kabisa ni wapi TISS ( UWT ) wamehusika na hayo madai yako tafadhali.
 
Kwa akili tu za kawaida acha za shule wewe unaamini hawapo nyuma ya yanayoendelea? Na kwa uwezo wako wa kupima mambo na uzoevu ulio nao pamoja na exposure kubwa ya kukaa karibu na marais wa nchi nyingine na mashushu mbalimbali bado tu huwaoni kwenye haya matukio? Naamini unajua lakini kwa masharti ya kazi yako na unayemtumikia aidha kwa kiapo au vyovyote basi umeamua kujifanya hujui lolote! Nakuheshimu.

Haya bhana Mnasihi no comment kwani nami nakuheshimu pia.
 
Back
Top Bottom