Waziri George Mkuchika unamdanganya nani?

Hata kama uhuru wa kutoa maoni tusichafue taasisi zenye heshima

Taasisi inafanya kazi kwa kanuni,msiingize siasa zenu kwa taasisi hii ambayo ina play part kubwa kwenye uchumi na usalama wa nchi ....

Tiss imekuwa easy punching bag kwa wanasiasa.hizo tuhuma mnazowapa uwt ni za kufikirika ,uwt hufanya kazi kwa kufuata kanuni na sio kufuata nini wanasiasa wanataka

Watch out boy
 
You're dealing with a different type of Brand....which is at its best...!!!

Hakuna cha kupandisha hasira wala kuhamaki wala kutoka kwenye reli yako ya SGR...!!
Naona unahangaika na kujirudia rudia kwa kutaka ushahidi ambao tayari unao..!! Kutumia lugha za ''kunyoosha'' kama ndugu yako anavyosema, haitakusaidia kitu..!! Deep in your heart you know the truth and that you have all the evidences that TISS are involved in this mess....!!

Another simple question: Mr.Gentamycine, can you please prove to this Forum that TISS are not involved in these???Just go ahead and prove it...!

Haya ndiyo majibu ' Kuntu ' ya maswali yangu niliyokuuliza? Halafu acha kusumbuka / kuhangaika kuniandikia kwa Kiingereza chako cha Ras Simba Mimi sikijui na nakipenda mno Kiswahili changu tafadhali. Nasubiri tena ushahidi kutoka Kwako kwamba TISS wanahusika moja kwa moja ya ' matukio ' ya Kiuhalifu yanayotokea sasa nchini Tanzania.
 
Nikikaa kimya nitakuwa sijitendei haki kama Mtanzania. Nina wajibu wa kusema kitu katika hili.
Mleta mada kaanza vizuri sana mada yake kwa kueleza mapungufu katika majibu ya Mh. Mkuchika. Ni kweli kitendo cha Mkuchika kusema Musiba anachunguzwa naTISS kimya kimya na watakapomaliza wataishauri serikali, ni upuuzi unaopaswa kupuuzwa na kila mwenye akili timamu. Kuunga mkono tamko la kitoto kama hilo lililotolewa na kiongozi wa wizara yenye dhamana ya Usalama wa nchi ni kuwadharau wazee wote wa nchi hii kama kweli tunaamini katika uzee kuna busara. Mkuchika alipaswa kudanganya kwa style nyingine siyo hii ya chekechea. Matamko ya Musiba yanadhalilisha vyombo vya dola kiujuzi na kumfanya Musiba awe bora kiutendaji kuliko wao. Labda mniambie Musiba ni miongoni mwa watendaji wa TISS ila kajificha/kafichwa kwa sababu za kikazi (Undercover). Vinginevyo hakuna sababu ya kusubiri kumchunguza mtu asiye na authority hata ya jambo dogo la kiserikali kutoa matamko makubwa yanayohatarisha uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine.
Kuhusu matukio ya utekaji na kuuawa au kujeruhiwa kwa baadhi wa watu wenye mtazamo tofauti na serikali, na kuhusisha suala hili na TISS, hili linahtaji mjadala mpana sana, lakini ukilitazama kwa ushahidi wa mazingira kutokana na matukio na mwitikio wa vyombo vya Usalama dhidi ya matukio hayo, utakuwa hujakosea ukisema aidha vyombo vya Usalama vinahusika au vinajua nani anahusika. Tukio la Lissu ni mfano wa upumbavu (narudia upumbavu) uliowahi aidha kutendwa au kushughulikiwa na vyombo vyetu kipumbavu. Tangu siku ya tukio nilisema kama kweli TISS au machanganyiko wa Idara za Kiusalama unaoitwa Task Force umehusika kwenye tukio hili moja kwa moja au kwa kuwa na taarifa na kuamua kuliacha litokee basi tuna watu WAPUMBAVU sana katika maamuzi ya kiusalama kama Taifa.
Tukio lingine linaloonesha ukosefu wa fikra tunduizi katika utendaji wa vyombo vya Usalama ni la Kijana Nondo ingawaje hili sikushangaa kwa vile inaonekana mchezo mzima ulichezwa na Polisi na hawa naamini viongozi wao wana kasoro kubwa vichwani ingawaje kina watendaji wa kati ni wazuri mno japo hawako kwenye ngazi ya maamuzi. Mfano mzuri wa uongozi wa Polisi ulio wazi kichwani ni RPC wa Dodoma.
Ukilitazama vizuri tukio la Nondo utaona wazi filamu ilivyo kosa mwongozaji mzuri hadi kufikia kuchanganya hata Location ya filamu yenyewe inatakiwa tukio gani liigizwe wapi!!
Wote mnaounga mkono hoja na mnaompinga mleta mada mnaweza kuwa na maoni mazuri lakini lililo wazi na lisilo na shaka ni kwamba Mkuchika hakuwa na uwezo wa kujibu hoja zile kwa vile hakujiandaa au hana kabisa majibu yake hata akipewa muda.
 
Hata kama uhuru wa kutoa maoni tusichafue taasisi zenye heshima

Taasisi inafanya kazi kwa kanuni,msiingize siasa zenu kwa taasisi hii ambayo ina play part kubwa kwenye uchumi na usalama wa nchi ....

Tiss imekuwa easy punching bag kwa wanasiasa.hizo tuhuma mnazowapa uwt ni za kufikirika ,uwt hufanya kazi kwa kufuata kanuni na sio kufuata nini wanasiasa wanataka

Watch out boy
Uchumi unaokuwa kwa ongezeko la 1.5trilion kweli uwt wako vizurii
 
Jana Waziri George Huruma Mkuchika, Waziri katika Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za Wabunge wa Upinzani na CCM kuhsu watu kutekwa, kupotezwa au kushambuliwa mchana kweupe na Mwandishi wa Habari Bwana MUSIBA anavyotoa matamko ya KICHOCHEZI lakini TISS wamekaa kimya.

Waziri katika kama kawaida ya Serikali ya CCM Kajibu hoja zote kisiasa na propaganda nyingi zenye kupotosha. Kwa kifupi niseme alichofanya Mkuchika ni KUJIBU HOJA NZITO KWA MAJIBU MEPESI,YA KITOTO NA YENYE KUPOTOSHA.

Mkuchika anawatetea TISS au UWT(Usalama wa Taifa) kwamba ATI TISS HUFANYA KAZI ZAO KIMYAKIMYA NA KUSHAURI SERIKALI NINI CHA KUFANYA. Huu ni uongo wa mchana kweupe. Usalama wa Taifa ya sasa kiukweli hawa ni USALAMA WA CCM na Serikali yake. TISS wako kutetea CCM na kukandamiza, kuonea, kunyanyasa na kuua Wapinzani kwa MASLAHI YA CCM NA SERIKALI YAKE.!!!

Kama kweli TISS wanafanya kazi kwa weledi unaostahili kama TISS ya enzi za Baba wa Taifa tusingelikuwa tunasikia upuuzi unaofanyika kwa sasa hapa Tanzania. Watu wameuawa huko Kibiti kwa karibu mwaka mzima na TISS wapo tu. Watu wakihoji kwanini watu wanauawa Waziri Daktari uchwara Nchemba anasema INAWEZEKANA CHADEMA wanahusika maana haiwezekani watu wa chama fulani(CCM) peke yao ndio wanauawa lakini Upinzani hawauawi...!!!Je, TISS walikuwa wapi kujua kuwakamata hao CHADEMA au CUF au ACT-Wazalando ili dunia ijue kwamba kumbe vyama vya upinzani ni vyama vya KIGAIDI??

Wakati Mkuchika anadanganya watu kwamba UWT wanaendelea kufanya kazi zao kimyakimya, i hali halisi ni tofauti kabisa na kinachotokea kwenye eneo la tukio.. Kuna Polisi 8 huko Kibiti na mpaka leo hatujui nani walihusika..?TISS wanafanya kazi kimyakimya.....Kuna mwandishi Azory Gwanda ametoweka kutoka eneo la tukio(KIBITI) akiandika habari za Kiuchunguzi kuhusu Mauaji hayohayo na mpaka leo zaidi ya siku 100 Gwanda hajaonekana....LAKINI TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA...!!

Kuna Ben Saanane ametoweka huu ni mwaka wa pili na haijulikani yuko wapi na nani aliyemteka. Watu wakihoji wanaambiwa waulizwe CHADEMA maana wanajua alipo...??TISS wapo tu wanaendelea kufanya kazi kimyakimya...!! Tundu Lissu kashambuliwa kwa Risasi zaidi ya 30 kwenye maeneo ya Bunge tena Makazi ya Viongozi wa Serikali na Waheshimiwa Wabunge mpaka leo hakuna hata sisimizi wa kusingiziwa amekamatwa....TISS WAPO WANAENDELEA KUFANYA KAZI YAO KIMYAKIMYA......!!!

Mwanafunzi wa NIT kauawa kwa kupigwa risasi na Polisi waliokuwa wanataka kuwazuia/kuwaua Viongozi wa CHADEMA waliokuwa wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Kinondoni kuadai Viapo vya Mawakala kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi...Leo Viongozi wa CHADEMA ndo wanaambiwa wanahusika na kifo cha Acqulina Akwiline.....Kwa maana nyingine Mbowe na wenzake ndio walifyatua risasi za kumwua Acqulina....Polisi waliokuwa na silaha za moto , Kamanda Mambosaasa aliyaamrisha Polisi wafyatulie risasi za moto watu wasiokuwa na hatia na Mkurugenzi wa Kinondoni hawahusiki kabisa kwa lolote....TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA....!!!

Kwa Waziri Mkuchuchika na CCM watu kuendelea kupotea, kuuawa, kushambuliwa na wapinzani kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kesi za hovyohovyo ndiyo UTAWALA BORA wa CCM na Serikali yake huku TISS au UWT wakiende;ea kufanya kazi kimyakimya......!!!

Hitimisho ni kwamba TISS wataendelea kufanya kazi zao kimya kimya huku wakiendelea kupanga mikakati ya kuwapoteza, kuwashambulia au kuwamaliza kabisa Viongozi wote wa Upinzani kimya kimya maana ndiyo kazi ya TISS kwa sasa na huo ndiyo utawala bora...!!!
Utakuwa umemwelewa kitoto. Kwa aliposema wanafanya kazi kimya kimya maana yake ni kwamba watakuwa wanajua kila tukio na aliyetenda? Mkuchika hajakosea,yeye ameelezea kazi ya TISS kwa mujibu wa uundwaji wake,sasa unachobisha nini. Hujui jinsi ya kubisha hoja,najua unajifanya unajua kama ilivyo kwa wengi wenu
 
Yaani umejiandikia tu.. ha ha haaaaa
Nasoma unashushuliwa unaishia kuwa vile vile ubishi.. ndoto zako unalazimisha.. mengi yamezoeleka humu kuishia kusa porojo za c&p
 
Mh George Huruma Mkuchika , katika Maelezo yake sioni makosa yoyote zaidi ya usahihi wa kile kinachotakiwa kutekelezwa na taasisi husika.

Tatizo lililopo mpaka mtoa mada anapata ukakasi ni ukiukwaji wa kile idara inachotakiwa kukifanya yaani KUCHUNGUZA ,KUHISI NA KUBAINI kisha kufikisha hayo kwa taasisi husika kwa utekelezaji.

Lkn sasa idara hiyo imejiingiza katika kazi zisizozao yaani kuvaa UPOLISI kila binadamu anaupenda UPOLISI na kuuchukia pale unapokuwa unamganda kinyume.

Hata ktk uzi huu ,kuna kejeli,matusi ,dhihaka na ubabe ambazo ni tabia za UPOLISI ,
 
ila yote kwa yote hayo wataenda kuyajibu kwa Mola wao, tumuombe sana Mwenyezi Mungu atuepushe na haya maasi ili tuepuke jehanam
 
Mh George Huruma Mkuchika , katika Maelezo yake sioni makosa yoyote zaidi ya usahihi wa kile kinachotakiwa kutekelezwa na taasisi husika.

Tatizo lililopo mpaka mtoa mada anapata ukakasi ni ukiukwaji wa kile idara inachotakiwa kukifanya yaani KUCHUNGUZA ,KUHISI NA KUBAINI kisha kufikisha hayo kwa taasisi husika kwa utekelezaji.

Lkn sasa idara hiyo imejiingiza katika kazi zisizozao yaani kuvaa UPOLISI kila binadamu anaupenda UPOLISI na kuuchukia pale unapokuwa unamganda kinyume.

Hata ktk uzi huu ,kuna kejeli,matusi ,dhihaka na ubabe ambazo ni tabia za UPOLISI ,
Unaweza kututhibitishia ndugu hizo allegations au ndio mihemuko za wanasiasa ,tatizo mnataka kuingiza siasa kwenye taasisi hii

Na uwt wamekuwa easy punching bag kwa wana siasa au sababu wapo kimya mbona jw na police force hamuwachezei au sababu huwa wana act ?
 
Ahsante!
Unawafahamu/unawahisi /unadhani ni kina nani? Waliozuia Mh Nape asiongee na wanahabari pale PROTEA HOTEL DSM.
 
Jana Waziri George Huruma Mkuchika, Waziri katika Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za Wabunge wa Upinzani na CCM kuhsu watu kutekwa, kupotezwa au kushambuliwa mchana kweupe na Mwandishi wa Habari Bwana MUSIBA anavyotoa matamko ya KICHOCHEZI lakini TISS wamekaa kimya.

Waziri katika kama kawaida ya Serikali ya CCM Kajibu hoja zote kisiasa na propaganda nyingi zenye kupotosha. Kwa kifupi niseme alichofanya Mkuchika ni KUJIBU HOJA NZITO KWA MAJIBU MEPESI,YA KITOTO NA YENYE KUPOTOSHA.

Mkuchika anawatetea TISS au UWT(Usalama wa Taifa) kwamba ATI TISS HUFANYA KAZI ZAO KIMYAKIMYA NA KUSHAURI SERIKALI NINI CHA KUFANYA. Huu ni uongo wa mchana kweupe. Usalama wa Taifa ya sasa kiukweli hawa ni USALAMA WA CCM na Serikali yake. TISS wako kutetea CCM na kukandamiza, kuonea, kunyanyasa na kuua Wapinzani kwa MASLAHI YA CCM NA SERIKALI YAKE.!!!

Kama kweli TISS wanafanya kazi kwa weledi unaostahili kama TISS ya enzi za Baba wa Taifa tusingelikuwa tunasikia upuuzi unaofanyika kwa sasa hapa Tanzania. Watu wameuawa huko Kibiti kwa karibu mwaka mzima na TISS wapo tu. Watu wakihoji kwanini watu wanauawa Waziri Daktari uchwara Nchemba anasema INAWEZEKANA CHADEMA wanahusika maana haiwezekani watu wa chama fulani(CCM) peke yao ndio wanauawa lakini Upinzani hawauawi...!!!Je, TISS walikuwa wapi kujua kuwakamata hao CHADEMA au CUF au ACT-Wazalando ili dunia ijue kwamba kumbe vyama vya upinzani ni vyama vya KIGAIDI??

Wakati Mkuchika anadanganya watu kwamba UWT wanaendelea kufanya kazi zao kimyakimya, i hali halisi ni tofauti kabisa na kinachotokea kwenye eneo la tukio.. Kuna Polisi 8 huko Kibiti na mpaka leo hatujui nani walihusika..?TISS wanafanya kazi kimyakimya.....Kuna mwandishi Azory Gwanda ametoweka kutoka eneo la tukio(KIBITI) akiandika habari za Kiuchunguzi kuhusu Mauaji hayohayo na mpaka leo zaidi ya siku 100 Gwanda hajaonekana....LAKINI TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA...!!

Kuna Ben Saanane ametoweka huu ni mwaka wa pili na haijulikani yuko wapi na nani aliyemteka. Watu wakihoji wanaambiwa waulizwe CHADEMA maana wanajua alipo...??TISS wapo tu wanaendelea kufanya kazi kimyakimya...!! Tundu Lissu kashambuliwa kwa Risasi zaidi ya 30 kwenye maeneo ya Bunge tena Makazi ya Viongozi wa Serikali na Waheshimiwa Wabunge mpaka leo hakuna hata sisimizi wa kusingiziwa amekamatwa....TISS WAPO WANAENDELEA KUFANYA KAZI YAO KIMYAKIMYA......!!!

Mwanafunzi wa NIT kauawa kwa kupigwa risasi na Polisi waliokuwa wanataka kuwazuia/kuwaua Viongozi wa CHADEMA waliokuwa wanakwenda kwa Mkurugenzi wa Kinondoni kuadai Viapo vya Mawakala kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi...Leo Viongozi wa CHADEMA ndo wanaambiwa wanahusika na kifo cha Acqulina Akwiline.....Kwa maana nyingine Mbowe na wenzake ndio walifyatua risasi za kumwua Acqulina....Polisi waliokuwa na silaha za moto , Kamanda Mambosaasa aliyaamrisha Polisi wafyatulie risasi za moto watu wasiokuwa na hatia na Mkurugenzi wa Kinondoni hawahusiki kabisa kwa lolote....TISS WANAENDELEA KUFANYA KAZI KIMYAKIMYA....!!!

Kwa Waziri Mkuchuchika na CCM watu kuendelea kupotea, kuuawa, kushambuliwa na wapinzani kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kesi za hovyohovyo ndiyo UTAWALA BORA wa CCM na Serikali yake huku TISS au UWT wakiende;ea kufanya kazi kimyakimya......!!!

Hitimisho ni kwamba TISS wataendelea kufanya kazi zao kimya kimya huku wakiendelea kupanga mikakati ya kuwapoteza, kuwashambulia au kuwamaliza kabisa Viongozi wote wa Upinzani kimya kimya maana ndiyo kazi ya TISS kwa sasa na huo ndiyo utawala bora...!!!
Hivi yule Ramadhani Ighondu alipompiga Ulimboka alimpiga kimya kimya!! kweli kimya kimya!!!
 
Back
Top Bottom