Waziri Denmark asema Ramadhani ni 'hatari kwetu sote'

Waziri Denmark asema Ramadhani ni 'hatari kwetu sote'

nankumene

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2015
Posts
7,408
Reaction score
8,225
Matamshi hayo kutoka kwa waziri uhamiaji na utangamano Inger Stojberg, mwanachama wa chama cha mrengo wa kati wa kulia cha Kiliberali, yanakuja baada ya kuanza wiki iliyopita, kwa mfungo wa Ramadhani, ambao ni mwezi ambamo Waislamu duniani kote wanafunga kuanzia alfajiri hadi jua linapozama.

"Natoa wito kwa Waislamu kuchukuwa likizo wakati wa Ramadhani ili kuepusha madhara kwa jamii nyingine ya Denmark," Stojberg aliandika katika makala ya gazeti la udaku la BT.

"Nashangaa iwapo amri ya kidini inayoagiza kutekeleza nguzo ya miaka 1,400 ya Uislamu inawiana na jamii na soko la ajira tuliyonayo nchini Denmark mwaka 2018."

Alisema pia kwamba anahofia kufunga kunaweza kuathiri "usalama na uzalishaji," akitolea mfano wa madereva wa basi wanaoshinda "bila kunywa au kula chochote kwa zaidi ya saa 10." "Hii ni hatari kwetu sote," alisema.


Waziri Inger Stojberg anajulikana kwa mitazamo yake hasi kuelekea uhamiaji.

Stojberg aliwahi kuzua utata mwaka uliopita alipoweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, picha yake akiwa anatabasamu huku amebeba keki kusherehekea hatua ya 50 ya Denmark kukaza sheria za uhamiaji.

Moja ya hatua kali zaidi ilianza kutekelezwa mwaka 2016, ambayo iliwaruhusu askari polisi kuwanyang'anya wakimbizi vitu vyao vya thamani, ingawa miongozo ya serikali iliziondoa pete za uchumba na harusi, baada ya hatua hiyo kusababisha hasira na kulinganishwa na Ujerumani ya Wanazi.

Stojberg pia alikosolewa kwa kuanzishwa matangazo kadhaa katika magazeti ya nchini Lebanon mwaka 2015, akiwaonya wanaopanga kutafuta hifadhi ya ukimbizi, juu ya ugumu uliopo katika mchakato wa kutafuta hifadhi nchini Denmark.

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, nchi hiyo imeimarisha sera zake kuhusu uhamiaji, ikisisitiza kuwa wahamiaji laazima wajifunze kwanza tamaduni za taifa hilo na lugha ili kutangamana katika soko la ajira.
source DW Waziri Denmark asema Ramadhani ni 'hatari kwetu sote' | DW | 21.05.2018
 
Kila mtu na amani yake...
Ukiwa na imani kufunga hakuna tatizo
 
Wamewahi kufanya utafiti kuona kama ajali zinaongezeka sana wakati wa Ramadhan ili kujiridhisha kwamba dereva aliyefunga anasababisha ajali?

Moja ya sifa ya kiongozi ni kuzuia mihemko na kuwa makini kwenye matamshi yake.
 
"...kufunga kwa zaidi ya masaa 10 bila ya kula chochote... "

Itabidi na waislam wanywe maji mchana kisha waendelee na swaumu kama wakristo.

Ahasnte.
 
Funga ni Imani tu.Watu wanafunga na asubuhi wanafanya mazoezi kwa saa 3 na wanaendelea na funga kama kawaida.
 
Halafu anakuja mtu et anapinga taratibu zao wazanzibari huko kwa kuzuia kula hadharani mchana wa mwezi wa ramadhani.

Tuheshimu tamaduni za watu.
Hao wanaopinga wana matatizo na ni udini unao wachoma.
Hivi wanajua kama znz ni nchi na ina utaratibu na utamaduni wake ? Na utaratibu na utamaduni huo hauwezi kuingiliwa na JMT ?
 
Hayo maneno angeenda kuyaongelea mbele ya hadhara Iran
 
"...kufunga kwa zaidi ya masaa 10 bila ya kula chochote... "

Itabidi na waislam wanywe maji mchana kisha waendelee na swaumu kama wakristo.

Ahasnte.
Amekosea kuingilia imani za watu na kuzikosoa. Yote kwa sababu watu wanaziacha nchi zao kwenda kwa nchi za wengine. Sasa wenyeji wenye kiburi wanasema chochote wanachotaka.
 
Amekosea kuingilia imani za watu na kuzikosoa. Yote kwa sababu watu wanaziacha nchi zao kwenda kwa nchi za wengine. Sasa wenyeji wenye kiburi wanasema chochote wanachotaka.

Mkataa kwao mtumwa mkuu. Mtu kwao.
 
"...kufunga kwa zaidi ya masaa 10 bila ya kula chochote... "

Itabidi na waislam wanywe maji mchana kisha waendelee na swaumu kama wakristo.

Ahasnte.
.....Aliekwambia wakristo wanakunywa maji mchana wakifunga nani mkuu?

Au umewaza tu hivyo utashi wako?
 
Back
Top Bottom