Waziri Bashungwa ahimiza utunzaji wa uoto wa asili na misitu

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
WAZIRI BASHUNGWA AHIMIZA UTUNZAJI WA UOTO WA ASILI NA MISITU.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) ametoa wito kwa Watanzania kutunza uoto wa asili na misitu iliyopo nchini na kujenga tabia na msukumo binafsi wa kupanda miti.

Ametoa wito huo Oktoba 22, 2022 wakati alipotembelea makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Chamwino, Jijini Dodoma.

"Tutunze uoto wa asili na misitu iliyopo na kujenga tabia na msukumo binafsi wa kupanda miti kwenye makazi, mahali pa kazi, mashambani, mjini na vijijini" amesisitiza Waziri Bashungwa

Bashungwa amesema Uhai na ustawi wa mwanadamu na viumbe vyote hapa duniani (ecosystem) vinategemea faida lukuki tunazozipata kutoka kwenye miti na misitu.

Aidha, Bashungwa amesisitiza Uzalendo na kufafanua kuwa ni utayari wa kutetea na kulinda ustawi wa Taifa letu la Tanzania, masilahi yake pamoja na watu wake.

Wakati huo, Bashungwa amelipongea Jeshi la Kujenga Taifa kwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na malezi ya vijana, uzalishaji mali kupitia SUMAJKT na ujenzi wa miradi mikubwa ya kitaifa.
IMG-20221023-WA0008(1).jpg
IMG-20221023-WA0009(1).jpg
IMG-20221023-WA0010(1).jpg
IMG-20221023-WA0011(1).jpg
 
Back
Top Bottom