Waziri Bashe ni mashine ya Rais Samia Suluhu

Waziri Bashe ni mashine ya Rais Samia Suluhu

Kumbuleni bashe si mwafrica ana damu ya kisomari...atamsaidia sana mama

Sisi waswahili wabantu ni kama kina kibandaa ; unawakandia CDM afu kesho yake mzinga kwa maza.
mhhh msomali si mwafrika ni nani sasa!
 
Ukimchunguza na yeye babu yake alitoka Malawi
Wa hivi huwa ni wakuja pia
Hata wazungu ukimuona mbaguzi sana ni wale walikimbia Ujerumani (Jews) wanajulikana
roho ya ubaguzi haiishii hapo bali huenda mbali zaidi hadi kubaguana wao kwa wao.
 
Jana kamlima Luhaga Mpina, Sukuma Gang leader, kama mtoto mdogo.
View attachment 2230262
Bashe tunashukuru umempa za uso huyo na ukweli 100%. Kuna watu wamekuwa mawaziri miaka 3 hakuna hata kitu kimoja unaweza kujivunia kaacha alama. Leo kama msumari wa jeneza umeupigilia sehemu yake maiti ikazikwe tu. Kuna watu wanajitoa ufahamu utasema Tanzania kisiwa kila kitu kinapanda kila sehemu duniani na kilimo ni sehemu pekee kwa nguvu zote inahitaji ruzuku kuliko kutoka ruzuku kwenye mashirika ya umma hasara tu. Kilimo ndio sehemu pekee uti wa nchi hii inastahili ruzuku.
 
Bashe ni real fighter ... Ndo Wazir pekee anayepambana
Anapambana na nini?
Maana kilio cha wakulima juu ya upandaji wa bei za pembejeo bado ziko palepale, ( zilipanda kabla ya vita msije mkasingizia vita ya Ukraine)
 
Hivi unaelewa usanii unaondelea kwenye sekta ya kilimo au umeamua kuwadharau Watanzania kwa kuleta hizi dhihaka za kusifiana?

Mbolea mfuko wa kilo 20 ni laki nusu, mwaka jana ilikuwa haizidi elfu 50. Wizi mtupu.
Hawa wanaangalia mtu anaongeaje basi wanamuona mchapa kazi.
Mchapakazi anapimwa kwa effect na sio uwezo wa kujenga hoja
 
Anapambana na nini?
Maana kilio cha wakulima juu ya upandaji wa bei za pembejeo bado ziko palepale, ( zilipanda kabla ya vita msije mkasingizia vita ya Ukraine)
Kamsikilize hoja yake bungeni na kama Una kiwanda kinachouza mbolea Kwa bei nafuu , popote kilipo duniani nenda atakupa tenda yote ya mahitaji ya tani 400000 , sio kuongea tuu , the guy anafight
 
Bashe tunashukuru umempa za uso huyo na ukweli 100%. Kuna watu wamekuwa mawaziri miaka 3 hakuna hata kitu kimoja unaweza kujivunia kaacha alama. Leo kama msumari wa jeneza umeupigilia sehemu yake maiti ikazikwe tu. Kuna watu wanajitoa ufahamu utasema Tanzania kisiwa kila kitu kinapanda kila sehemu duniani na kilimo ni sehemu pekee kwa nguvu zote inahitaji ruzuku kuliko kutoka ruzuku kwenye mashirika ya umma hasara tu. Kilimo ndio sehemu pekee uti wa nchi hii inastahili ruzuku.
Bashe ameshakua compromised na kampuni za mbolea
Yeye mwenyewe mwaka huu mwanzoni alikubali bei imepandishwa kiholela na atachukua hatua. Sasa hivi kabadilika. Ila ngoja tuisome namba tu vizuri maana washajua hata wakitusaidia sisi ni wajinga
 
Kamsikilize hoja yake bungeni na kama Una kiwanda kinachouza mbolea Kwa bei nafuu , popote kilipo duniani nenda atakupa tenda yote ya mahitaji ya tani 400000 , sio kuongea tuu , the guy anafight
Huo ni uongo na kukimbia uwajibikaji, anataka kumpa nani tender ikiwa mfumo kuagiza mbolea kwa pamoja ulishafutwa?

Bashe alikiri Bei ya mbolea imepandishwa kiholela na akasema atachukua hatua. Sasa hivi anakuja na story ya soko la dunia. Ila kwa watanzania Kama nyinyi wacha ipande tu
 
Bashe ameshakua compromised na kampuni za mbolea
Yeye mwenyewe mwaka huu mwanzoni alikubali bei imepandishwa kiholela na atachukua hatua. Sasa hivi kabadilika. Ila ngoja tuisome namba tu vizuri maana washajua hata wakitusaidia sisi ni wajinga
Hakuna bei kupandishwa kiholela tuweni wa kweli maana ya holela ni nini? mbolea inazalishwa kutoka wapi? Sote tunajuwa Russia na Ukraine ni wazalishaji wakubwa wa mbolea sasa ukiwa na main supply duniani hawachangii unadhani bei itakuwa the same? Ok kishatoa offer kama anamjuwa mtu au source mbole bei rahisi aende achukuwe contract. Kuongea ni rahisi lakini kuja na solutions ndio changamoto.
 
Bashe ajikite kutafuta investors kwenye kilimo cha umwagiliaji, akitegemea waswahili itakula kwake..

Bora achukue wataalamu wakajifunze kwa Nchi zinazofanya vizuri kwenye irrigation Ili waje na utaalamu unaotakiwa.

Mwisho ,Bora afanye miradi michache yenye tija kuliko kufanya siasa za kufurahisha kila mahala pesa zote zikaishia ardhini.
Yani umeongea point, Mimi pia Jana nililifikiria sana hili. Alete wawekezaji japo wataua local
 
ni sawa na kusema mwarabu wa misri na morocco ni mwafrica.

Kwa hiyo ni wa muscat ama?
Nani alietupanga weusi tu tukae Africa?
Hakuna faida yoyote ya kushabikia ujinga huo ni illiterates tu ndio mtaongea haya
Get a life dude
Hao ni waafrika damu na wako kwenye nchi zao
 
Yani umeongea point, Mimi pia Jana nililifikiria sana hili. Alete wawekezaji japo wataua local
Hawawezi kuua bali way compliments hao local, investors Kazi yao ni kulima for exports na hao locals ni kwa ajili ya solo la ndani ,pia watapata soko la Mazao yao..

Watumie mashamba ya serikali,kutegemea waswahili ni Kazi bure..

Waswahili waliua kilimo cha Zimbabwe
 
Ana maneno mengi lakini ground ni tofauti.

Ubaya tunapenda sana maneno mazuri ya wanasiasa kuliko vitendo vyao.

Bashe anakiri bei ya mbolea imepandishwa kiholela,Ila Cha kufanya hana.
Hugo sahihi.
Ingekuwa nchi ya kuwajibika kwa kushindwa kumanage bei ya mbolea angekuwa benchi
 
Bila shaka hapa unamzungumzia Samia. Ili kujua kama anamuelewa au hamuelewi anza na bajeti yenyewe ya kilimo. Kutoka Bil 200+ hadi Bil 700+ hizi ni dalili kubwa kuwa Samia anatambua nini cha kufanya na yeye na Bashe wana nia ya dhati ya nchi hii. Bajeti ya umwagiliaji kutoka Bil 5 hadi Bil 300 sio jambo la kubeza hata Kidogo. Cha msingi hapo ni kujipanga hizo pesa zisiliwe na wajanja wakati wa utekelezaji maana sina shaka Samia atapeleka zote.
Aisee this is massive.
 
Bashe ni jembe sana. Tuachane na usomi wake na exposure yake kubwa ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

Kwanza alianza kwa kusurvey maeneo yote ya Wizara yake nchi nzima akiwa Naibu Waziri. Ameizunguka nchi nzima.

Ametembelea taasisi zake zote na maeneo ya miradi yake nchi nzima.

Bashe ni mtu wa Umwagiliaji. Bashe anajua dhana ya uzalishaji.

Wabunge wanamkubali sana. He is very logical Minister. He knows what he is doing.

Bashe ni mashine ya hii nchi.
Waliopo kwenye sekta ya kilimo ndo wanajua kua ni Jembe au Siasa tu. Kilimo cha Tanzania bado sana kimejaa siasa sioni kama kinainuka.
 
Unapingana na yeye mwenyewe alivyosema kuwa imepandishwa kiholela? Bei imeanza kupanda kabla ya Vita vya Russia na Ukraine. Msome hapo alikubali kuwa imepandishwa kiholela na atachukua hatua

View attachment 2230330
Hapo kaongelea specific kampuni moja leo kaongelea kwa kijumla hakuna sehemu kasema mbole haijapanda duniani kaitaja kampuni moja pekee iliyofanya uhuni huo kwa wakati huo lazima tutofautishe suala la mmoja mmoja na suala la kijumla.
 
Back
Top Bottom