Ni ukweli usiopingika kuwa waziri Bashe anafanya makosa yanayoweza kuepukika hususani yale yanayoweza kuhatarisha diplomasia ya nchi kwa nchi ambapo nyenzo kubwa ya kudumisha diplomasia ni mazungumzo na falsafa ya Rais Samia ya 4R inasimamia hilo.
Ushauri ni swala moja, kupokea na kufanyia kazi ni swala lingine na endapo litaharibika haimaanishi hukushauriwa. Bahati mbaya ulowataja hubeba mizgo ya lawama ya kila aina na hawana wa kuwasemea wala msemaji. Wanapokea kama shimo la taka.