Waziri Bashe: Hakuna Vanilla inayouzwa Tsh. Milioni 1.5 duniani

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe @bashehussein amesema sio kweli kwamba zao la vanilla linauzwa kwa kilo Tsh.mil 1.5 ambapo amesema taarifa hizo ni za uongo huku akiwataka Waandishi wa Habari kuisaidia Serikali kufikisha taarifa sahihi kwa Wakulima kuhusu bei za mazao na taarifa nyingine za kilimo.

Bashe amesema hayo leo Ikulu Dar es salaam wakati akiongea na Viongozi pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023), unaotarajiwa kufanyika Sept 05-08,2023 Jijini Dar es salaam.

Bashe amesema “Nitaanza na swali la Mwandishi aliyeuliza je vanilla inauzwa Mil 1.5 ni uongo, nimesikia iliandikwa gazeti la Mwananchi ni vizuri kutochukua taarifa ambazo hazina uthibitisho, kwakuwa nyinyi ni Waandishi ni vizuri Vyombo vya Habari mkalipia ada kidogo kujiunga kwenye International Commodity Platform Prices ambazo zinawasaidia kuona bei za bidhaa Duniani kote lakini zipo platform kama Business Insiders ukiingia unaweza kuona bei halisi ya bidhaa fulani Duniani kwa wakati fulani”

“Tanzania tunazalisha vanilla kwa kiwango kidogo, Mikoa kama ya Kagera na Mikoa ya Kilimanjaro na vanilla ni zao ambalo lina eneo sana soko lake ni kama pareto, pareto sisi Tanzania ni Wazalishaji wa pili Duniani lakini tunazalisha tani Elfu 2 hadi Elfu 3 anayeongoza Duniani anazalisha tani Elfu 8”

“Kwahiyo vanilla zipo Nchi zimeshapiga hatua sana Duniani zinazofanya vizuri kwenye zao hili, vanilla ilipanda bei hapa miaka miwili mitatu baada ya Nchi kama Madagascar zilipokumbwa na vimbunga kwasababu wao ni Wazalishaji wakubwa na sisi ikasaidia Wakulima wetu kupata bei nzuri, kwahiyo bei ya Tsh. mil 1.5 haipo Duniani, bei ya laki 5 haipo Duniani”
 
kwanza, anakuja kukanusha baada ya watu kuhimizwa kulima, wakatafuta mashamba, wakaanza kulima, wamevuna, na sasa wamekosa masoko ndiyo anakuja kukanusha bei.
pili, anakanusha bila kutaja bei halisi, anaposema hakuna inapouzwa milioni 1.5, je inauzwaje? Milioni 1.3? Au milioni 1?
 
hatari sana...... matangazo ya bei yalikua yanarushwa hadi ITV kabisa..... waziri hukuona?

Lakini kibaya zaidi tumeuziwa miche ya mbegu kwa sh. elfu 15 kwa mche mmoja.

sasa hapo fanya hesabu rahisi tu umepanda miche 100 kwa bei hiyo ya elfu 15

daaaah .....ama kweli tumelizwa
 
Wengine tulilijua hilo la bei hiyo tangu awali. Ogopa sana watu wanaojiita wahamasishaji maarufu kama "motivational speakers."
 
hatari sana...... matangazo ya bei yalikua yanarushwa hadi ITV kabisa..... waziri hukuona?

Lakini kibaya zaidi tumeuziwa miche ya mbegu kwa sh. elfu 15 kwa mche mmoja.

sasa hapo fanya hesabu rahisi tu umepanda miche 100 kwa bei hiyo ya elfu 15

daaaah .....ama kweli tumelizwa
Watu hatupendi kushughulisha akili zetu, yaani wakati wa utandawazi huu unashindwaje kujua bei ya soko la vanilla . Kuna mmoja nilimshauri asijiingize huko akaniona nina wivu na maendeleo yake na alinihahidi kuto nipa lift akinunua HUMMER H2 ndani ya mwaka mmoja
 
kwanza, anakuja kukanusha baada ya watu kuhimizwa kulima, wakatafuta mashamba, wakaanza kulima, wamevuna, na sasa wamekosa masoko ndiyo anakuja kukanusha bei.
pili, anakanusha bila kutaja bei halisi, anaposema hakuna inapouzwa milioni 1.5, je inauzwaje? Milioni 1.3? Au milioni 1?
Mimi sina wa kumlaumu, walaumiwe hao walio umizwa kwa ujinga wao na waendelee kupigwa. Tena wengi ni wafanya kazi yaani waajiliwa wa taaluma fulani yaani wameshindwa kutumia elimu yao kufikiri, bei ingekuwa hivyo si watu wa kagera wangekuwa billionaires.
Kila kitu unacho taka kufanya lazima ufanye research ndogo hata historia tu ya zao la vanilla hapa Tanzania au walikuwa anafikiri kuwa wao ndo wa kwanza kulima vanilla hapa Tanzania?
 
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe @bashehussein amesema sio kweli kwamba zao la vanilla linauzwa kwa kilo Tsh.mil 1.5 ambapo amesema taarifa hizo ni za uongo huku akiwataka Waandishi wa Habari kuisaidia Serikali kufikisha taarifa sahihi kwa Wakulima kuhusu bei za mazao na taarifa nyingine za kilimo.

Bashe amesema hayo leo Ikulu Dar es salaam wakati akiongea na Viongozi pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari kuhusiana na Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-Afrika Food Systems Summit 2023), unaotarajiwa kufanyika Sept 05-08,2023 Jijini Dar es salaam.

Bashe amesema “Nitaanza na swali la Mwandishi aliyeuliza je vanilla inauzwa Mil 1.5 ni uongo, nimesikia iliandikwa gazeti la Mwananchi ni vizuri kutochukua taarifa ambazo hazina uthibitisho, kwakuwa nyinyi ni Waandishi ni vizuri Vyombo vya Habari mkalipia ada kidogo kujiunga kwenye International Commodity Platform Prices ambazo zinawasaidia kuona bei za bidhaa Duniani kote lakini zipo platform kama Business Insiders ukiingia unaweza kuona bei halisi ya bidhaa fulani Duniani kwa wakati fulani”

“Tanzania tunazalisha vanilla kwa kiwango kidogo, Mikoa kama ya Kagera na Mikoa ya Kilimanjaro na vanilla ni zao ambalo lina eneo sana soko lake ni kama pareto, pareto sisi Tanzania ni Wazalishaji wa pili Duniani lakini tunazalisha tani Elfu 2 hadi Elfu 3 anayeongoza Duniani anazalisha tani Elfu 8”

“Kwahiyo vanilla zipo Nchi zimeshapiga hatua sana Duniani zinazofanya vizuri kwenye zao hili, vanilla ilipanda bei hapa miaka miwili mitatu baada ya Nchi kama Madagascar zilipokumbwa na vimbunga kwasababu wao ni Wazalishaji wakubwa na sisi ikasaidia Wakulima wetu kupata bei nzuri, kwahiyo bei ya Tsh. mil 1.5 haipo Duniani, bei ya laki 5 haipo Duniani”
Yaani mwandishi wa habari anafundishwa jinsi ya kupata habari sahihi!
 
Hizi promo mbona zimetangazwa sana hata na vituo vya habari, nakumbuka ITV walikuwa wanatangaza sana hii hasa shamba moja lipo huko Zanzibar wakihitaji watu wawekeze na masoko yapo ya uhakika vipi na wao wanasemaje?
 
Ushauri wangu kwa wakulima, limeni mazao mliyoyazoea au mnayoyajua.
Achaneni na kilimo cha wahamasishaji wa mitandaoni hata kama ni watu mnaowaamini!
 
Watu hatupendi kushughulisha akili zetu, yaani wakati wa utandawazi huu unashindwaje kujua bei ya soko la vanilla . Kuna mmoja nilimshauri asijiingize huko akaniona nina wivu na maendeleo yake na alinihahidi kuto nipa lift akinunua HUMMER H2 ndani ya mwaka mmoja
🤣🤣🤣🤣🤣
 
yule tapeli yule kutoka njombe nilijua tu ilikua ponzi scheme ya yeye kuuza miche na technology halafu soko ni kulia na kusaga meno facken kabisa.
 
Back
Top Bottom