Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 20,871
- 52,691
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi ametoa wito kwa Makundi mbalimbali kufika bila kukosa katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jijini Dar es Salaam, kesho Septemba 4, 2026.
Miongoni mwa walioitwa ni Sheikh Said Mwaipopo pamoja na kundi lake la mabaunsa, Viongozi wa Vikundi vya Mabaunsa, Mwenyekiti na Katibu wa Wamiliki wa Makampuni Binafsi ya Ulinzi, ambao wametakiwa kufika saa 3 asubuhi.
Aidha, Katambi amesisitiza kuwa Wasanii na Watu maarufu mitandaoni ambao hawakuitikia wito wake wa awali wa Septemba 2, 2026, wanatakiwa kufika bila kukosa kesho katika Wizara hiyo.
Amewataja wanaotakiwa kufika kuwa ni Jenifer Jovin (Niffer), Godfrey Tumaini (Dudubaya), Nasma Hassan Athuman (Nana Dolls) na Twalib Bakari Mungiya (Uncle T) ambao wametakiwa kufika saa 4 asubuhi.