Waziri Augustine Mahiga: Tamko la Rais ni sheria!

Ndiyo maana ya kuwa Amiri Jeshi Mkuu. Amri yake haihojiwi lazima itekelezwe kwa mamlaka yake ktk Ulinzi na Usalama wa Taifa. Na ana "kinga" ya kutoshitakiwa.
Ana kinga ya kutoshtakiwa kwa yale atakayofanya akiwa madarakani ambayo yapo katika mamlaka yake kisheria (jurisdiction). Kwahiyo akifanya jambo nje ya mamlaka yake (ultra vires) anashtakika na kupandishwa mahakamani vizuri tu. Mamlaka ya Rais na mipaka yake inawekwa na katiba. Kisheria hakuna mtu aliye juu ya katiba.
 
Amezuia mikutano ya vyama vya Siasa, iliyowekwa kikatiba na ameweka utaratibu wake mwingine wa kufanya mikutano hiyo na ametoa sababu ya kufanya hivyo, nani amemshitaki? Wanasheria wamelijua hilo ndio maana wako kimya.
 
Nimemsikiliza waziri wa Sheria na Katiba, Dkt Augustine Mahiga, akiongea na waandishi wa habari, tarehe 18 mwezi huu, akidai kuwa tamko la Rais lishakuwa sheria tayari!

Alikuwa akiongelea kuhusu maagizo aliyoyatoa Rais Magufuli baada ya kutembelea gereza la Butimba, baada ya kuagiza kuwa msongamano wa wafungwa kwenye gereza hilo unatisha, kwa hiyo akaagiza kuwa mahabusu ambao wamelundikana kwenye gereza hilo,ambao kesi zao zinadhaminika waweze kudhamiiwa.

Hili tatizo la msongamano wa wafungwa siyo la leo wala Jana, Bali ni la muda mrefu sana na watu mbalimbali wamepiga sana kelele sana kuhusu tatizo hilo, lakini vyombo vinavyohusika vilijifanya kama vimeweka pamba masikioni na kutotaka kabisa kusikiliza kero hiyo. Lakini sasa katamka Mheshimiwa Rais Magufuli, nimeona hatua za "fast track" zikichukuliwa kutatua tatizo hillo

Hata hivyo kilichonishangaza ni hilo tamko la Waziri wa Sheria na Katiba, Augustine Mahiga, kutamka kwenye kikao cha waandushi wa habari eti tamko la Rais ishakuwa sheria tayari!

Ninavyojua Mimi ni kuwa nchi inakuwa na sheria mama, ambayo ni Katiba ya nchi, ambayo inatakiwa kila mwananchi wa nchi hii anapaswa kuitii na kuiheshimu na ndiyo sababu hata Rais wa nchi anaapa kabla ya kushika madaraka kuwa atailinda na kuitii

Kumbe watendaji wetu wakuu wanachukulia kivingine kuwa tamko la Rais la kwenye majukwaa ya kisiasa ndiyo ishakuwa sheria, hata kama Rais anatamka vitu ambavyo vipo.kinyume cha Katiba!

Ndiyo maana tumeona Mheshimiwa Rais, akitamka kwenye majukwaa ya kisiasa kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya siasa vya upinzani, ingawa inajulikana wazi kuwa tamko hilo ni batili, kwa kuwa nchi hii inaongozwa na Katiba ya nchi, ambayo hata yeye Rais aliapa kuitii na kuitekekeza kabla hatijamkabidhi madaraka hayo ya kulingoza Taifa hili, na katika Katiba hiyo ya nchi inaeleza wazi kuwa nchi hii itaongozwa na mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, lakini kama alivyoongea Waziri Mahiga kuwa tamko la Rais lishakuwa sheria na hivyo kulifanya Jeshi la Polisi nchini kuwazuia viongozi wa vyama vya siasa nchini kufanya mikutano hata ya ndani, kwa madai kuwa hilo ni agizo la Mheshimiwa Rais!

Hivi tamko la Rais, hata kama linavunja sheria za nchi hii linawezaje kuwa ni sheria, wakati yeye Rais aliapa kuitii na kuitumikia Katiba ya nchi hii??

Nayakumbuka maneno ya busara sana aliyowahi kuyatamka Baba wa Taifa hili, Mwalimu Nyerere, katika moja ya hotuba zake, wakati wa uhai wake, nanukuu "Tunachagua Rais ambaye tunamtaka ni LAZIMA aitii Katiba ya nchi, ambayo tulimwapisha kabla ya kuingia Madarakani, ili aiheshimu na kuitii Katiba hiyo na kama Rais huyo hataki kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi yetu, ni bora Rais huyo akatuachia Urais wetu na yeye akaenda kufanya shughuli nyingine" Mwisho wa kunukuu
Huyo mzee naye ndo maana hujikojolea hovyo hovyo!
 
Jee kujua kuna msongamano wa watu magerezani, ilibidi kwenda kulishuhudia Mwanza. Mbona hapo Keko karibu ya magogoni pamefurika
Hiyo ndiyo inaitwa "east or west, home is best"

Kama kuna magereza mengi nchini, lakini Rais ameamua kwenda kuliangalia gereza la "nyumbani" kwake
 
Baba wa Taifa alisema, “Katiba ya nchi inanipa madaraka makubwa sana. Akija mtu na kuyatumia vibaya madaraka hayo makubwa sana basi atakuwa kama mungu.”

Hakukosea hata chembe. Imagine kama angekuwa bado yuhai jinsi angemchana huyo nduli na dikteta tena bila kukwepesha si hawa waovu wengine Mkapa na Kikwete wanahofia hata kukohoa kwa jinsi wanavyomuhofia huyo mwendawazimu.

Ndio maana tunaitwa Nchi za dunia ya tatu.
Wengine wamefika mbali hadi kutuita Shit holes.
Nchi hizi bado hazijastaarabika katika kiwango cha kufaa katika maisha ya binadamu.
Bado tuna kama ushamba fulani hivi.
Tusipokuwa madarakani tunawalaumu watawala.
BAK, tukikupatia nchi unaweza kuwa mwovu zaidi ya huyo unayemlaumu.
Tukipata madaraka tunakuwa vinara wa kuvunja sheria.
Tukiambiwa ukweli tunaghadhabika na kutoa adhabu Kali.
Tunataka kusifiwa tu hata tunapo haribu.
Hatutaki kukosolewa wala kujiwajibisha.
Tunahukumu haraka makosa ya wengine ilihali wenyewe tunazidi kutenda uovu.
Hatujali ustawi wa jamii Bali ustawi wa vitu.
Tatizo hili lipo ktk nchi zote zinazoitwa za dunia ya tatu na sio Tanzania tu.
Ni kwamba bado hatujastaarabika.
In short,
Bado Washamba.
 
Baba wa Taifa alisema, “Katiba ya nchi inanipa madaraka makubwa sana. Akija mtu na kuyatumia vibaya madaraka hayo makubwa sana basi atakuwa kama mungu.”

Hakukosea hata chembe. Imagine kama angekuwa bado yuhai jinsi angemchana huyo nduli na dikteta tena bila kukwepesha si hawa waovu wengine Mkapa na Kikwete wanahofia hata kukohoa kwa jinsi wanavyomuhofia huyo mwendawazimu.
Ndiyo maana tulifanya kosa kubwa kuipoteza fursa nzuri sana ya ile Rasimu ya Katiba ya Warioba na kwa namna huyu unayemwita nduli anavyoendesha nchi hii kwa sasa ni ndoto kuipata Katiba mpya!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Naam hawa wahuni na mainterahamwe waliona kifo cha ccm hivyo wakaamua kupora majadiliano yale.

Ndiyo maana tulifanya kosa kubwa kuipoteza fursa nzuri sana ya ile Rasimu ya Katiba ya Warioba na kwa namna huyu unayemwita nduli amavyoendesha nchi hii kwa sasa ni ndoto kuipata Katiba mpya!
 
Yuko sahihi tamko lolote la Mheshimiwa Rais linakuwa sheria kwa sababu lazima litekelezwe. Ndiyo maana Rais hawezi kuongea jambo lolote hadharani kisha ukasema ni maoni yake. Rais hana maoni binafsi. Hivyo chochote anachoongea kwa umma kina impact.
Hahaha huu ujinga hata mimi nimeona.
 
Keshakuwa mganga njaa tu. Akili kubwa haiwezi kuacha nchi ikaendeshwa kwa mihemko na matamko. Ukweli ni kuwa, akili kubwa hata ambazo tulizijua na kuzipenda zamani hasa ndani ya Lumumba, kwa wengi sasa hivi hazipo. Tumekubali kuunda kwa bidii taifa LA wanafiki. Taifa linalothamini na kusifia UGANGA njaa kama ndio MBINU ya kisasa badala ya akili na busara. Amen.
Ni kweli tamko la Raisi ni sheria.
Akiamrisha wewe ukamatwe na kuwekwa ndani masaa 90 itatekelezwa na vyombo vya dola Mara moja, hata kama huna kosa lolote.
Tamko hili linawaelekeza washauri wa Raisi kumshahauri vizuri na kuhakiki matamshi ya Raisi yasije leta madhara kwa jamii.
Tamko la Raisi linaweza hata kuibadili Sera ya nchi.
Mahiga ni akili kubwa, kama ni mtu wa harakaharaka huwezi kumwelewa.
Ana hadhi ya Uraisi wa nchi.
 
Wanasheria watz walinyamazishwa. Katikatu ya vitisho vya maguvu ya dola, Lissu aliongea
Amezuia mikutano ya vyama vya Siasa, iliyowekwa kikatiba na ameweka utaratibu wake mwingine wa kufanya mikutano hiyo na ametoa sababu ya kufanya hivyo, nani amemshitaki? Wanasheria wamelijua hilo ndio maana wako kimya.
 
Wanasheria watz walinyamazishwa. Katikatu ya vitisho vya maguvu ya dola, Lissu aliongea
Kila mu anauwezo wa kuongea. Mwanasheria tunamtegemea atumie ujuzi wake kwa kuchukua hatua za kimahakama. Lissu anaesimama mahakamani kumtetea mtusi wa mitandaoni anashindwaje kutetea nguvu ya katiba mahakamani? (Kama kweli imekiukwa)
 
Lakini hapaswi kuongea kitu "against" Katiba yetu ya nchi na ndiyo sababu kabla ya kuanza kutekekeza madaraka yake ya Urais, anaapa kuwa ATAIHESHIMU na KUITII Katiba ya nchi yetu. Full Stop

Sijui kama kweli hujui kwamba Tanzania ilishakuwa banana republic muda mrefu sana kabla ya awamu hii. Nchi imekuwa ikiendeshwa kwa “busara za rais”. Mahiga is smart; anaijua hali halisi. Rais ndiyo katiba; ndiyo sheria hadi siku mtakapofanikiwa kurejesha utawala makini nchini.
 
Nijuavyo mimi ni kuwa kauri ya Rais ni amri na sio sheria,ndio maana anaweza akaongea kitu huku anacheka na baada ya muda mchache kitu kile alichokiongelea kinatekelezwa,na ingekuwa kauri ya Rais ni sheria basi nafikiri watu wangekuwa wanahukumiwa kwa kunukuu baadhi ya kauri za Marais walioyatamka hasa kwenye taasisi husika (Mahakama)
 
Ni kweli tamko la Raisi ni sheria.
Akiamrisha wewe ukamatwe na kuwekwa ndani masaa 90 itatekelezwa na vyombo vya dola Mara moja, hata kama huna kosa lolote.
Tamko hili linawaelekeza washauri wa Raisi kumshahauri vizuri na kuhakiki matamshi ya Raisi yasije leta madhara kwa jamii.
Tamko la Raisi linaweza hata kuibadili Sera ya nchi.
Mahiga ni akili kubwa, kama ni mtu wa harakaharaka huwezi kumwelewa.
Ana hadhi ya Uraisi wa nchi.
Hahahahaaa...nimependa hapo..'kama ni mtu wa harahaharaka huwezi kumwelewa'
 
.

Back
Top Bottom