Waziri ataka wapiga debe waondolewe Dar

hivyo inaonesha anasema kitu anachokifaham kabisa. kama kasema hailipi na unasema aliwah kuwa mpiga debe basi ni wazi kuwa ana ushahidi na hiyo kazi kuwa hailipi. hongera sana waziri.
Ilikuwa hailipi kwasababu yeye alikuwa mpiga debe dodoma kwa kina matonya ila kwa majiji kama dar na kwingineko inalipa na hao wapiga debe wanaendesha familia zao kwa kazi hiyo.huwezi kufanya utafiti kwa mtu mmoja na kufanya hitimisho.
 
...aliposema wakafanya HATA kilimo...naona kama kilimo amekishusha hadhi au lugha tu sijamwelewa! lakini ukweli wapiga debe nchi nzima hutengeneza mazingira yasiyo rafiki sana kwa jamii zingine....utafutwe utaratibu mzuri wa hawa Jamaa, tukikurupuka hawana simile hawa and they have almost nothing to loose kama sio uhai wao tu....mtaani itakuwa balaa hata ndala tu zitaibwa!!
 
Njia rahisi ni kuhakikisha mradi wa mabasi yaendayo kasi unaanza kazi, mabasi yapo barabara tayari sielewi ni nini kinachokwamisha.
 
asantee sana Mh.Simbachawane nadhani Makonda atalifanyia kazi kwa ufasaha na tukaondokana na hii adha ya wapiga debe kwasababu wengi ni wezi na wakwapuaji
 
Kazi ya mkuu wa mkoa sio kukimbizana na wapiga debe, meya na mkurugenzi wake wawatoe na sijui watafanyaje kazi wakati wameshachaniana blauzi
 
Mi naona wakomae na omba omba wale watoto wamekuwa wengi sana mtaani hivi sasa
 
Visionary leaders walihitajika Sana kipindi hiki has a kwa nafasi za maamuzi,yaani kabla ya kutoa amri ushatoa suluhisho!!kuna watu wataishi maisha ya kunyanyasika hii nchi Kama sio raia!!kuna wapiga debe wanasomesha na kulisha familia kwa kazi hiyo
 
Watanzania hawa waliozoea kelele sasa watakua wanabebwa kupelekwa posta Kumbe anakwenda ubungo, Tanzania watu ni wajinga wakupindukia, wamezoea kelele Ndio aingie kwenye daladala upumbavu,. Nchi gani inaendeshwa kiwendawazimu kama hii?

Naipongeza hii kuwafukuza wapiga Debe wote ili kuwe Na Amani Na utulivu kwenye vituo.
 


minazani mpango ni bubu huo.

kuwatoa sawa ila wanaenda wapi baada ya kuwatoa?

mnajua ni familia ngapi zinategemea upiga debe wao? na hizo familia zitaishije?

nakubari wazo ni zuri maana wanakera sana katika vituo vya magari, ila kukiwa hakuna mpango wa kubalance ili kusiwe na usumbufu pia kwa hawa watu, maana wakikosa pesa wataiba tu hawana njia nyingine.

mi nashauri waanze kuwatoa maeeneo posta na feri kwanza, huku kwengine hebu waache wakiwa wanaendelea kuumiza kichwa jinsi ya kuwapunguza hawa watu wote, maana hapa tunazungumzia si chini ya vijana na wazee 500, kwa kukadilia.

wakija naamur tu bila plan, watakuwa wanawaadhibu hawa mabwana, itabadilika kuwa lengo ni kuwakomoa na kuwaadhibu pia lengo halitafanikiwa kama la waalimu kusafiri bure.

watumie akili sio nguvu kutimiza hili jambo zuri sana
 
Ni bora wapiga debe waondolewe watu tupumue na wizi wao....na wengi wao ni waathirika wa madawa ya kulevya ni vizuri pia wakasaidiwa kupelekwa reharb......maana ni kero kubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…