Waziri ashangaa ndege kuuzwa Sh500,000/=

Waziri ashangaa ndege kuuzwa Sh500,000/=

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,075
Reaction score
168,759
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiza jana alishikwa na butwaa, pale alipopewa taarifa ya kuuzwa ndege tatu za Serikali, ambazo zilikuwa katika Kituo cha Kilimo Anga kwa kiasi cha Sh500,000 kwa kila moja.
Ndege hizo, tatu zilikuwa zikitumika katika udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao .


Akisoma taarifa ya kituo hicho mbele ya Waziri Chiza, Mhandisi Mkuu wa Ndege wa kituo hicho,Gideon Mugusi,alizitaja ndege hizo kuwa ni 5H-MRN, Cessna 185 nyingine ni 5H-MRF, Cessna 185 na nyingine aina ya 5H-MRP piper Super Cub ambazo zilianguka katika vipindi tofauti.

“Ndege zote tatu ziliharibika lakini Shirika la Bima la Taifa(NIC), walilipa Serikali kupitia katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo, kulingana na viwango vya bima vilivyokuwa vikilipwa na wizara”alisema Mugusi.

Hata hivyo alisema tangu kuanguka na kuuzwa kwa ndege hizo,shughuli za kituo hicho, Kimekuwa zikidorora kwani marobani karibu wote wameondoka na kituo kimebaki na ndege moja tu ambayo pia ni mbovu na kibali cha kuruka angani kimekwisha.
Alisema kwa sasa kutokana na kukosekana kwa ndege, gharama za uendeshaji wa shughuli za kituo zimekuwa ni kubwa mno kwani wanalazimika kukodisha helikopta na gharama zake zimekuwa zikipanda mwaka hadi mwaka.


Waziri aja juu:
Kutokana na maelezo hayo, waziri Chiza alikuja juu na kuhoji iweje ndege hizo, ziuzwe kwa Sh 500,000 kila moja.


zinaendelea kufanyakazi na zinamilikiwa na nani,”alisema Chiza.
Waziri huyo, pia alihoji iwapo ndege hizo, zilifutwa kwenye orodha ya kumbukumbu za Serikali kama hazifai kwa matumizi pia kama ufutwaji wake ulifuata sheria na kanuni za Serikali.


“Leo sikuja kukamata mchawi, ila mimi binafsi nitafuatilia ili kuona kama sheria zilifuatwa au kama ndege zimeuzwa bila kufuata sheria” alisema Chiza.
Awali alisema Serikali ina mpango wa kufufua kitengo hicho na kwa kuanzia tayari imetoa fedha za kununua ndege moja.


“Naagiza mfanye mchakato haraka wa kununua ndege hii, hatutaki tena ukiritimba kwani nia ya Serikali ni kufufua kituo hiki,”alisema Chiza.
Alisema ,kituo hicho ndiyo pekee katika nchi za Afrika ya Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya kilimo anga na kama ndege zikianza kufanya kazi, basi zitaweza kukodiwa na nchi jirani.


Kituo cha Kilimo Anga kilianzishwa na wizara ya kilimo ,ikishirikiana na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika la UNDP na FAO mnamo mwaka 1979 na lengo kubwa lilikuwa ni kuimarisha utoaji huduma katika sekta ya kilimo katika kupambana na visumbufu vya mimea wahamao(migratory pest control).
 
Hebu ona UNAFIKI huu
"Naagiza mfanye mchakato haraka wa kununua ndege hii, hatutaki tena ukiritimba kwani nia ya Serikali ni kufufua kituo hiki,"alisema Chiza.
Alisema ,kituo hicho ndiyo pekee katika nchi za Afrika ya Mashariki chenye uwezo wa kutoa huduma hiyo ya kilimo anga na kama ndege zikianza kufanya kazi, basi zitaweza kukodiwa na nchi jirani.
Kama waziri anaogopa kukamata mchawi, na hajatuambia kuwa hatua kali zitachukuliwa je kuna haja gani ya kuendelea kuwa na imani na mtu huyu?
Je ni kweli alikuwa halijui hilo dili haramu kabla ya kufanywa?
Je waliouza ndege hizo walipata wapi ujasiri mkuu namna hiii? Amini amini nawaambia, huu ni upepo tu utapita.
 
Hebu ona UNAFIKI huu
Kama waziri anaogopa kukamata mchawi, na hajatuambia kuwa hatua kali zitachukuliwa je kuna haja gani ya kuendelea kuwa na imani na mtu huyu?
Je ni kweli alikuwa halijui hilo dili haramu kabla ya kufanywa?
Je waliouza ndege hizo walipata wapi ujasiri mkuu namna hiii? Amini amini nawaambia, huu ni upepo tu utapita.

Unadhani mfanyakazi wa kawaida kabisa wa kituo hicho anaweza kuuza ndege kwa 500K? Zitakuwa zimeuzwa na vigogo
 
ndege.jpg


Hii ndio ndege iliyouzwa laki tano
 
Wanafiki tu hawa anashangaa nini sasa yy wakati anapanga ziara ya kwenda huko alikuwa hajui haya?

Sent from Samsung tablet
 
kuuzwa kwa bei iyo kutakua na justification tu kama zilikua beyond repair na zikauzwa kama scaps metal ila kama zimefufuliwa na zinatumika then that is an issue!!!!
 
Hii nchi bwana...siasa zimeingiliwa kweli kweli....ina maana bei ya ndege ni ndogo kama simu yangu ya mchina?
 
Kumbe hata mimi ninaweza kununua ndege japo inayohitaji matengenezo!
 
Chiza anatia aibu, yaani moja kwa moja nauona ushiriki wake kwenye hili dili chafu

Mimi sioni dalili ya ushiriki. Ninachoona mimi ni

Mfumo hovyo hovyo wa mawasiliano na utunzaji kum bukumbu usio na malengo.

La pili tabia ya viongozi kurithi na kukaa ofisini bila nia ya kutaka kuelewa mienendo iliyopita katika ofisi zile. Sana sana kutaka kudeal na issues zitakazotokea yeye akiwepo ofisini.

La tatu ni tabia ya Watanzania na viongozi hasa wa Serikali ya kutokupenda kusoma, na kuona mafaili na vitabu vilivyomo kama mapambo ya shelves.

Nne ni lack of confidence katika kuchukua maamuzi.

Tano ni lack of trust among top government leaders. Mgawanyiko na kusalitiana ki makundi!.

Sita ni hofu kwa kutokubashiri viongozi wake watachukuliaje maamuzi yake. Pengine anaweza kupata punishment!

Saba hofu ya usalama wake kwa vile hajui nani muasisi na mshirika wa hilo deal na ni mtu wa aina gani. Nani atamlinda ama kummunga mkono?

Nane kutaka kujikosha katika jamii kwamba aoneakne yeye ni mtu safi na anajali.

Tisa Kukosa uwajibikaji, kwamba bora liende. "Nitalifunika nami hadi muda wangu utakapoisha niondoke bila lawama".

Kumi ni ufahamu mzuri wa CHIZA namna vile serikali ya TZ ilivyo na usanii, hivyo kuamua kulala mbele kwa kujua hata akishika bango mwisho wake itakula kwake! AFADHALI ASTAAFU SALAMA!
 
Back
Top Bottom