Waziri Apinga Agizo La Waziri Mkuu.

Wana JF,
Hili swala limekuwa likinisumbua sana. Je mawaziri wetu wako chini ya RAIS au PM. Ukiangalia ni nani anawateuwa swala ni kwamba wote wanateuliwa na RAIS na hivyo kwa maana nyingine wote BOSS wao ni RAIS. Hapa sasa inakuja ni MAPENZI ya RAIS na si katiba kumpa PM madaraka zaidi au kumyima.
FMES umetoa mfano mmoja tu. Ila ukikumbuka wakati wa Mwinyi, wakati Mkapa ni Waziri wa Elimu na Bilali ni Katibu mkuu pale walikuwa hawapikiki. Ndiyo maana wengine wanasema chanzo cha urafiki kati ya Mahalu na BWM. Bilali alikuwa akiwa na shida anakwenda moja kwa moja kwa Rais na kumruka Mkapa. Kigoma Malima pia nasikia alikuwa akimruka PM na kwenda kwa Rais moja kwa moja na kwa sababu PM hana nguvu ya kumuondoa waziri wala kumkemea, ilikuwa ni kasheshe.
Mie ningelitaka au ningelipendekeza kuwa Rais amteuwe PM. PM achague mawaziri wake na kuwaapisha kama timu yake. Najua kuna wizara itabidi tu wakubaliane na Rais nani awe maana mwisho wake ni kuwa Rais anakuja kuweka sahihi SARIKALI mpya ianze kazi na kwa hiyo bila kukubaliana naye hamna kitu. Ila ukweli utakuwa kwamba, Mawaziri wote watakuwa KWELI chini ya PM. NA Serikali itakuwa kweli ni TIMU MOJA. Rais yeye abaki kama alivyo sasa, kutembelea nchi moja baada ya nyingine na akirudi anapata tu maelezo kutoka kwa PM na kwenda kukagua shughuli kama zinakwenda sawa na walivyokubaliana. Hapo hakuna Waziri kutoa FYOKO kwani PM anaweza kumtimua kazi palepale. System ya sasa naona inampa RAIS majukumu mengi sana na MADARAKA MAKUBWA SAANA. (Amiri jeshi, Rais, Mume, Baba, mwenyekiti wa chama, M/K wa AU, Kiongozi wa mawaziri(PM LIKE), ...................) This is three much. Hivi na UKUU WA VYO VIKUU bado uko kwa RAIS? Mie Sikonge huku sina habari nyingi.
 
Ngeleja hivi punde amesema kuwa kuhusu Meremeta waziri mkuu alisema atalitolea kauli ila kwa sasa hana cha kuongeza zaidi na amemwomba Dr.Slaa kuwa asimchukulie shilingi kwani hana maelezo ya zaidi.
 
Dr.Slaa atatoa hoja ya kutaka maelezo hivi punde nafikiri atataka kushika shilingi japo sijui ila wale wanaoangalia Bunge waendelee kufuatilia.
 
Spika kambania Dr.Slaa ,kwa kisingizio kuwa muda umeisha ile hali alikuwa wa kwanza kutajwa ila hajapewa nafasi ya kutoa hoja yake .


Maigizo maigizo ze comedy.........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom