Waziri Apinga Agizo La Waziri Mkuu.

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Waziri wa Nishati na Madini Willium Ngeleja leo amepinga agizo la Waziri Mkuu Mhe.Pinda kuwa atatakiwa kutoa Kauli ya Serikali wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Nishati na Madini.

Waziri mkuu alimtaka Waziri Ngeleja kuhakikisha kuwa anatoa mwongozo na msimamo wa Serikali kuhusu KIWIRA NA TANPOWER RESOURCES LTD.

Kinyume chake kwenye Hotuba nzima ya Ngeleja hajatamka lolote kuhusiana na agizo hilo na hili linamfanya Waziri Mkuu kuonekana kuwa ni Muongo mbele ya Jamii ama asiyekuwa na uwezo wa kuagiza Mawaziri na wao wakachukua hatua , hili ni Jambo la hatari sana.;

Itakumbukwa kuwa Waziri Mkuu aliwahi pia kupuuzwa na ama kwa kupewa taarifa za uongo na Katibu mkuu wake ndugu Vicent Mrisho juu ya MEREMETA na alishindwa kumchukulia hatua zozote Katibu mkuu huyo.

Ndugu Mrisho alimwambia Waziri Mkuu kuwa MEREMETA ni suala la usalama wa Taifa kumbe ni uongo wa kutisha .

Maswaloi ya kujiuliza je? Ni kuwa waziri mkuu hana mamlaka na mawaziri?
Huyu Pinda hana sauti na ama akisema anaweza kupuuzwa na Mawaziri kiasi hiki?

Inanitia wasiwasi sana kwa huyu Waziri Mkuu kama hasikilizwi ataweza kweli kuiongoza Serikali hii?

TAFAKARINI KWA KINA JUU YA JAMBO HILI ,KUNA KITU KITATOKEA SOON.
 
Kina MREMA WAKO WENGI TU ccm..!
Watajitoa lakini bado muda kidogo tu!
Wacha wajipange kwanza kisheria!
WATAPEWA NCHI HAO NA PINDA ATAKWENDA JELA ASIPOKUWA MAKINI!
 
Acha Kupotosha,

Mhe. ngeleja alielezwa na Waziri Mkuu aandae Ripoti kuhusu Meremeta,hivyo si lazima aitoe Bungeni ila itatolewa,Leo ni siku ya Bajeti na iliandaliwa hata kabla ya Waziri Mkuu kutamka yale maneno.
 
Real? kweli hapa Bongo nuksi kama PM naye anaweza kusema kuwa waziri atatoa maelezo ya kina ila kakaa kimya ,kuna tatizo hapa kwa kweli.
Lets wait and see .....
 
Sidhani kama alitakiwa atoe kwenye hotuba yake ya Bajeti... nadhani muda bado upo. hii mada ingekuja baada ya kikao cha bajeti na Ngeleja hajatoa hiyo taarifa then tungekuwa na tatizo.
 
Acha Kupotosha,

Mhe. ngeleja alielezwa na Waziri Mkuu aandae Ripoti kuhusu Meremeta,hivyo si lazima aitoe Bungeni ila itatolewa,Leo ni siku ya Bajeti na iliandaliwa hata kabla ya Waziri Mkuu kutamka yale maneno.

Gembe hapa napingana na wewe kuwa huyu jamaa anapotosha kwani ninakumbuka kuwa Waziri mkuu alipokuwa anajibu hoja za Dr .Slaa alisema kuwa kuhusu Tanpower resources na Kiwira ,waziri husika wa nishati na madini atatoa msimamo wa serikali wakati wa bajeti yake ....

Hapa kuna kitu kimefichika , mwenye hotuba ya Pinda wakati akijibu hoja anaweza kutuwekea hapa na kuweza kuona alichosema Waziri Mkuu.
 
Mpaka Kielewe, hicho pekee (hotuba ya Pinda) ndicho kitakachoamua kama Ngeleja amekiuka agizo la Waziri Mkuu au la. Upande mwingine Waziri hawajibiki kwa Waziri Mkuu!
 
Kaangalie ansard kama alisme maneno niliyoyapigia mstari.Mwanakijiji is he knows
 
Mpaka Kielewe, hicho pekee (hotuba ya Pinda) ndicho kitakachoamua kama Ngeleja amekiuka agizo la Waziri Mkuu au la. Upande mwingine Waziri hawajibiki kwa Waziri Mkuu!

Ila ni kuwa waziri mkuu ndio msimamizi wa shughuli za serikali sasa kama waziri hawajibiki kwa waziri mkuu wanawajibika kwa nani wakiwa humo Bungeni?
 
Things Fall Apart and Our Leadership And The Destiny of Tanzania is reckoning When Rain Clouds Gather, Beware Soul Brother for although The Beautiful Ones Are Not Yet Born their Long March To Freedom is here, it is becoming No Longer at Ease, Weep Not Child for we have crossed The River Between and are approaching the Season of Migration to the North where we will crucify the Devil On The Cross more deadlier than the Trial of Dedan Kimathi and expose his Ambiguous Adventures disguised as Anthems of the Decades.

The Concubine is intrigued by A Question of Power and instigating The Enemy Within his opposition while forming The New Tribe to help him be Collector of Treasures while relegating his kin to Gathering Seaweed with No Grain of Wheat

In the Fog of the Seasons' End the Navigation of a Rainmaker disguised as president is proving to be No Easy Walk To Freedom

The Reluctant Playwright is asking The Interpreter to clear this So Long A Letter
 
No..!
Mmesahau ya MREMA?
Hapo kuna kitu inaitwa "COLLECTIVE RESPONSIBILITY"
Kwamba maamuzi ya waziri mkuu pamoja na mawaziri wote wa ccm ni ya kukumbatiwa kwa kauli moja!
Na hivyo Ngejela anaonekana atawasha moto kama wa mrema kwani ili aruhusiwe kutoa kauli ya tofauti na MPINDA HAKI...Basi itabidi ajivue uwaziri na kuwa kama mbunge HURU MWENYE KUPIGANIA UHURU!
WANAKUJA WENGINE WENGI..TARATIBU TU NA MWISHOWE WANAMTANDAO WATAKUWA ISOLATED!
 
Ila ni kuwa waziri mkuu ndio msimamizi wa shughuli za serikali sasa kama waziri hawajibiki kwa waziri mkuu wanawajibika kwa nani wakiwa humo Bungeni?
.
Mkuu ni kweli waziri mkuu ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za serikali bungeni.Hatahivyo,usimamizi huo haumpi mamlaka ya kutoa amri na maagizo kwa mawaziri wenye wizara zilizoko nje ya ofisi yake.Ana mamlaka ya kumuamuru waziri wa TAMISEMI na waziri wa masuala ya bunge maana hawa ndio wanaomsaidia kazi.Kiutaratibu wa kimfumo yeye PM ndiye waziri wa TAMISEMI na masuala ya Bunge.Na ndio maana hotuba yake ya bajeti inagusa maeneo yote hayo.Mh kombani na Mh.Malmo wanamsaidia tu.Sasa hawa ndio anaweza kuwaagiza jambo na lazima litekelezwe haraka.
Hali ni tofauti kwa wizara zinazojitegemea kama ya Mh.Ngereja.Mh Ngereja yeye anawajibika kwa Rais.Ni Rais tu ndiye anayeweza kumuamuru kufanya jambo na akalitekeleza haraka sana.Na tukumbuke Rais pia ni sehemu ya bunge kwa mujibu wa katiba ya nchi.Na ndio maana hotuba na miswada yote ya wizara hizo hujadiliwa kwanza na baraza la mawaziri,ambako mh.Rais ndiye mwenyekiti. PM na waziri ni wajumbe wa kawaida katika kikao hicho.
Kwa hiyo kama PM alisema Mh.Ngereja atalizungumzia hilo ,basi ilikuwa ni maoni ama mapendekezo na wala sio maagizo.PM kuwa msimamizi wa shughuli za serikali bungeni kuna maanisha kwamba anahakikisha kuwa majukumu ambayo serikali imepanga kuyatekeleza bungeni basi yanatekelezwa kikamilifu.Kama ni maswali ya wabunge ni jukumu lake kuhakikisha yanajibiwa yote na kwa ufasaha.Na ndio maana mara nyingine utamuona PM akitoa majibu ya ziada kuhusu jambo lolote kwa wizara yoyote ile.PM pia atawajibika kuhakikisha mahudhurio ya mawaziri na manaibu wao bungeni.Ni lazima mawiziri wote wamuombe ruhusa PM kama kuna dharura ya kusafiri au kutohudhuria kikao.Lakini zaidi ya hapo mawaziri wote(isipokuwa wa nchi ofisi ya PM) huwajibika kwa Rais.
Sasa nikirudi kwenye mada kuu ni kwamba, kama wadau wengine walivyosema muda bado upo.Kwa hiyo hakuna haraka tusubiri.Kwanza ni kwamba Mh.Ngereja ametoa hotuba ya bajeti.Sasa inawezekana kabisa wakati wa kufunga mjadala wa hotuba yake akagusia suala hilo.Kwa hiyo hapa napo pana muda wa kusubiri.Lakini hata kama asipogusia wakati wa kujibu hoja za wabunge,yawezekana akapata nafasi ya kufanya hivyo kabla ya mkutano wa bunge kuisha.Muhimu ni subira tu.Ni lazima mwisho wa siku watanzania tutapewa majibu na serikali juu ya suala hili.
 
What is COLLECTIVE RESPONSIBILITY?
 
Vyovyote vile, iwe kisheria au kiutaratibu, ni kuwa kama mawaziri hawawajibiki kwa PM sio muhimu kwa sasa hivi. Kilichotegemewa toka kwa waziri ni kile alichosema PM, na kama alisema maelezo yatatolewa wakati wa bajeti, basi yangetolewa mwanzoni na Bw. Ngeleja, ili yajadiliwe halafu akifunga mjadala wa hotuba yake iwe kuwa anatoa tu majumlisho ya mjadala.

Hebu tuhakikishe alichosema PM ili tujue mtiririko unaotakiwa.
 
Things Fall Apart and Our Leadership And The Destiny of Tanzania is reckoning When Rain Clouds Gather, Beware Soul Brother for although The Beautiful Ones Are Not Yet Born their Long March To Freedom is here, it is becoming No Longer at Ease, Weep Not Child for we have crossed The River Between and are approaching the Season of Migration to the North where we will crucify the Devil On The Cross more deadlier than the Trial of Dedan Kimathi and expose his Ambiguous Adventures disguised as Anthems of the Decades.

The Concubine is intrigued by A Question of Power and instigating The Enemy Within his opposition while forming The New Tribe to help him be Collector of Treasures while relegating his kin to Gathering Seaweed with No Grain of Wheat

In the Fog of the Seasons' End the Navigation of a Rainmaker disguised as president is proving to be No Easy Walk To Freedom

The Reluctant Playwright is asking The Interpreter to clear this So Long A Letter

Pundit,
Should we give up our Audacity of Hope or what you told us were just the Dreams from My Father and yours?
 
Ila ni kuwa waziri mkuu ndio msimamizi wa shughuli za serikali sasa kama waziri hawajibiki kwa waziri mkuu wanawajibika kwa nani wakiwa humo Bungeni?

Waziri Mkuu ndiye mkuu wa shughuli zote za serikali bungeni, na ndiye bosi wao mawaziri wote nje na ndani ya bunge,

Check this out, Waziri wetu mmoja aliwahi kushutumiwa sana na media kuwa ni mwizi wa hela za pantoni ya Kigamboni, wakati mwizi hasa wa zile hela, alikuwa ni katibu mkuu wa wizara aliyekuwa akiitwa Ongara, waziri yule kwa hasira akaenda kwa rais kumshitaki yule katibu mkuu, alipofika kule rais akamfukuza na kumwambia awe na adabu aende kwa Waziri Mkuu kwanza,

Alipofika kwa Waziri Mkuu, yule katibu mkuu akawa amepata habari, siku moja akamfuata yule waziri na bastola na kuanza kumtishia kuwa atammaliza asipoangalia, mwisho akaondoka bila kumtwanga nayo shaba, waziri akaenda tena kwa Waziri Mkuu, kumbe bwana yule katibu mkuu na waziri mkuu lao moja, yule katibu mkuu akahamishiwa kuwa RDD wa Tabora, that is all, sasa Waziri akaamua kwenda kwa rais kulia zaidi kuwa adhabu aliyopewa yule katibu haikua sawa na kosa la kumtishia na bastola, rais akamjibu kuwa Waziri Mkuu alichoamua ndio mwisho.

Sasa kwa sababu ya hizi siasa za makundi, Ngeleja anaweza kuwa ana-belong to the kundi lenye power zaidi kuliko kundi la pinda, kwa hiyo hawezi kumtii inaeleweka, lakini Waziri Mkuu ndiye bosi wa mawaziri wote na wanapaswa kutii amri zake, period!
 
Pamoja na maelezo mazuri ya wachangiaji lakini tufahamu Pinda nae anakauli nyingi za utata ni kupenda kuwa Nice guy. Kumtegemea sana Ngeleja sidhani kama itakuwa suluhu labda tuendelee kusisitiza kupata taarifa za Kiwira bila kujali nani atazitoa.

Kila kiongozi anakwepa jukumu lake, binafsi sioni kwamba Pinda anaiweza nafasi aliyo nayo kwa mwendo alioanza nao. Pinda anaongoza kwa kutoa General statement, si unaona hata Wanzibar wamemjia juu kuhusu Zanziba ni nchi au la! Meremeta kachemka na anavyojibu maswali kwa kauli za jumla jumla.
 
Things Fall Apart and Our Leadership And The Destiny of Tanzania is reckoning When Rain Clouds Gather, Beware Soul Brother for although The Beautiful Ones Are Not Yet Born their Long March To Freedom is here, it is becoming No Longer at Ease, Weep Not Child for we have crossed The River Between and are approaching the Season of Migration to the North where we will crucify the Devil On The Cross more deadlier than the Trial of Dedan Kimathi and expose his Ambiguous Adventures disguised as Anthems of the Decades.

The Concubine is intrigued by A Question of Power and instigating The Enemy Within his opposition while forming The New Tribe to help him be Collector of Treasures while relegating his kin to Gathering Seaweed with No Grain of Wheat

In the Fog of the Seasons' End the Navigation of a Rainmaker disguised as president is proving to be No Easy Walk To Freedom

The Reluctant Playwright is asking The Interpreter to clear this So Long A Letter

Umenikumbusha homework supervision, duh ilinibidi nisome hivyo vitabu bila kupenda.
 
Back
Top Bottom