Waziri Angela Kairuki: Uhakiki wa vyeti haujafanywa kwa Viongozi walio katika nafasi za kisiasa!

Wanasiasa ni hawa
1. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa.
2.Diwani
3. Mbunge(wakuchanguliwa au kuteuliwa)
4. Waziri kwa sababu ni mbunge
5. Waziri mkuu kwa sababu ni mbunge.
6.Rais na makamu wa rais

Wafuatao sio wana siasa hata kama wanateuliwa na rais

1. Makatibu wakuu.
2. Ma RC na Ma DC, na wengine wengi kama CDF, IGP, jaji mkuu nk

Kifungu alicho kisema waziri leo hakiwahusu RC na DC, kinawahusu wanaochaguliwa na wananchi moja kwa moja kupitia vyama vyao vya siasa. Tukitaka RC na DC wawe wanasiasa kulingana na katiba yetu wapigiwe kura na wananchi.
 
Huwa najiuliza kila siku.Hv ingetokea labda Meya wa Chadema ndo kagundulika kafoji vyeti hv ingekuaje?!
 
Sioni sababu ya kumlaumu waziri kwa kutowahusisha kwenye list yake wale tuliodhani walipaswa kuwemo yaani, Wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa...

Mtazamo wangu waziri kafanya kazi Nzuri kwa wigo na mapana ya matakwa ya kazi zake kama alivyoeleza.

Pendekezo :
NECTA ndio ipewe hilo jukumu. Kama tumegundua Kuna wengine ambao sio watumishi wa UMMA lkn ni wanufaika wa kodi zetu Wafuatiliwe au bunge letu kama Lina Nia njema watutungie sheria . Wasiishie hapo kila kampuni kila taasisi kwa ushirikiano na NECTA wafanye msako wa vyeti Feki kila kona Bila kujali ni private au wanufaika wa kodi zetu.

Ukweli na uwazi ndio kichocheo cha kuondokana na Umasikini.
Kila mtanzania afanye anachopaswa kufanya kihalali kulingana na elimu yake
Kama ni mtanzania huna elimu, lkn unakipaji cha uongozi au ufundi ila huna elimu au cheti ufanikiwe kupitia njia hiyo...
Abraham Lincoln hakwenda shule lkn ndio Rais wa kuheshimiwa US na duniani. Hakuhangaika na mavyeti au kufojifoji Bali alijifundisha mwenyewe sheria kwa kujisomea na kuwa wawili mkubwa aliyeshinda kesi nyingi kuliko hata waliokwenda shule...

Watu wakubwa wawili Katika Ulimwengu wa dini Mtume na Yesu hawakuwa na degree lkn ndio watu maarufu wenye wafuasi wengi duniani kuliko mtu yoyote aliyewahi kuishi duniani.

Tumeanza vzr, ila hii iwe phase 1, kila mtanzania popote alipo Bila kujali ni serikalini, biashara, sekta binafsi, Muajiliwa au muajili mwenye ulaghai wa elimu arudi ktk sehemu anayopaswa kuwa.

Kama tukigundua taasisi flani vyeti sio lazima tubadili vigezo vya kupata wafanyakazi hao Bila cheti...
 
Mungu adhihakiwi.....Muda wake ukifika atawatendea haki waTanzani....imagine watumishi waliofutwa kazi km mvua bila maandalizi wengine wametumikia nchi miaka zaid ya 25 karibia wanastahafu then wananyimwa stahiki zao hii haimpendezi Mungu ata nukta....Hawa sio watumishi hewa eti wanalipwa mishahara bila kufanya kazi NO hawa walikua wanafanya kazi sema walifoji vyeti km alivofoji Bashite....
 
Ndio sheria inasema hivyo?Je,una uhakika gani serikali itakuwepo kuwashughulikia wakitenda uhalifu huo?Una uhakika gani kuwa hawajavitumia?Mfano Bashite yeye kashakitumia na kubadili jina kabisa,amekitumia pia kutimiza entry qualification chuo alichosoma!Umesahau Ndalichako alitangaza kuwasaka waliohitimu vyuo vikuu wakiwa wamefoji vyeti vya form four??
basi hapo ni uzembe wa chuo pia, walishindwaje ubaini vyeti visivyo halali???
 
Friends and Enemies..,

Who is Magufoliing who?...Angela Kairuki or Juma Poor Manager?...

Fascinating.,indeed it is very very fascinating...!what does juma poor manager think?that he is going to R.I.P bashite's drama?..

Hii kitu mbona iko wazi sana?Yusuph makamba alikuwa. Regional commissioner Dsm na hakuwa na elimu ya kutisha wala ya kustusha na hakuna aliekamshikia bango kuhusu suala la elimu hata siku moja...

Hili suala liko wazi...iachwe double standards katika hili.

Na ifamike wazi kwamba hakuna anaepinga vita dhidi ya vyeti feki kama vile ambavyo hakuna anaepiga vita dawa za kulevya...kila mwenye akili timamu lazima aunge mkono mambo hayo.

Na isieleweke kama watu wana chuki na bashite...hapana hapa tunaendelea kupiga kelele ili haki itendeke..

Hata kama bashite angekuwa kapata nafas hizo alizozipata kwa elimu ya darasa la saba kwetu sisi haituhusu na wala hatuoni umuhim wa kuhoji...ni juu yake mwenyewe juma poor manager.

Ishu kubwa ya bashite hapa ni kutumia cheti ambacho siyo chake na kufanikiwa kuongopea umma wa watanzania hadi mamlaka za uteuzi kuwa yeye ni Paul Makonda ili hali yeye ni Daudi Bashite...hilo ni kosa la jinai tena si kufoji vyeti tuh hilo ni zaid ya kufoji vyeti.

Na kuendelea kwake Daudi bashite kukaaa kimya katika hilo suala au hata mamlaka zake za uteuzi ni ushahid tosha kuwa suala hilo ni mwiba mchungu kwao na ambalo wameshindwa kabisa kulitolea clarifications...

Kama Juma Poor Manager anadiriki kusema kwamba hawez kuwasamehe ndugu zetu wenye vyeti feki na angela kairuki anasema kwamba zoez hilo halihusishi viongiz wa kisiasa wafaham fika kuwa hilo siyo jibu katika hoja hii ya bashite..

Bashite kama angekuwa kapata nafas hizo kwa vyeti vyake halisi vya darasa la saba ni sawa lakin kwake haikuwa hivyo...analindwa kwa style hii kwa nin hasa?

Ni jambo ambalo hakika liko wazi na kuendelea kukumbatiwa inatia shaka vita hii ya vyeti feki na kuondoa uhalisia wake moja kwa moja...

Daudi bashite pamoja na uozo wake mwingi ambao juma poor manager ameamua kuufumbia macho atambue kuwa hata kama itachukua kipindi chote cha utawala wa juma poor manager suala hili bado litashikiwa bango,

Angela kairuki na Joyce ndalichako hata kama wanaujua uhalisia watafanya nin?

Kwan wao hawataki kuish maisha mazur?yaliyomkuta nape kwan wameyasahau?...

Wanajua fika wakigusa suala la bashite watamgusa baba yake juma poor manager...walichobakia nacho ni kuhadaa umma na kukaa mbali kwa hoja kwamba zoez hilo halijagusa wanasiasa.

Lakin kwa hakika hili ni jambo ambalo limeondoa uhalisia wote wa vita hii dhidi ya vyeti feki na kujenga taswira mbaya ya double standards na upendeleo ambao wengine tunauona ukiegemea zaid kwenye ukabila tuh.

Ukimya wa daudi bashite katika hilo ni uthibitsho tosha kuwa hana ujasiri wa kupambana na ukweli unaomsuta.
Una ushahidi gani kuwa katumia cheti kisicho chake
 
Mbona msio na busara mnatoa matusi hata kwa Rais muelewe huyo ni RAIS wa wote hats ninyi mkikwama mnamkumbuka. Muwe na kiasi
 
Najiuliza kitu kimoja, Kwa nini vyeti vya Weteule havihakikiwi je wao wanaruhusiwa kuwa na vyeti feki?
 
Back
Top Bottom