Waziri alejeshewa pesa aliyo toa kama rambi rambi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri alejeshewa pesa aliyo toa kama rambi rambi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fidel80, Sep 25, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Bw. Cyril Chami.
  Waziri wa JK Cyril Chami amerejeshewa pesa aliyo toa kwenye msiba wa mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi. Alitoa kiasi cha 50,000/= baada ya kutoa akasema anatoa basi tu huyu mwandishi alikuwa ananichafua kwenye magazeti jamaa wakaamua kumrudishia pesa zake kwa njia ya cmu.
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Wakuu hii kitu imetokea leo mliopo mjini mnaweza ipata kwenye gazeti la Alasiri
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Bw. Cyril Chami, amekwaa kashfa nzito baada ya kudaiwa kumsimanga marehemu kwenye msiba mmoja na hivyo wafiwa kudaiwa kumrejeshea pesa zake zote alizotoa kama rambirambi ya mpendwa wao.
  Tukio hilo, limetokana na msiba wa mwandishi wa habari, Ali Sonda (47) wa gazeti la Mwananchi mjini hapa, ambaye alifariki dunia Septemba 14 mwaka huu.
  Inadaiwa kuwa Naibu Waziri Chami, alitoa pesa za rambirambi kiasi cha shilingi 50,000 kwa mazishi ya mwandishi huyo aliyefia katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi, huku pia akitoa maneno ya masimango yaliyowakera waandishi wenzie wa habari na mwishowe kuamua kumrejeshea pesa zake kwa njia ya simu ya mkononi.
  Inadaiwa kuwa Chami alisema anatoa pesa kwa marehemu Sonda basi tu, kwani enzi za uhai wake alikuwa akimchafua sana, kauli ambayo iliwafanya waandishi ambao ni sehemu ya wafiwa kuamua kumrejeshea rambirambi yake, kwani walidai kuwa Sonda (marehemu) ametuhumiwa na Naibu Waziri Chami ilhali ikijulikana fika kuwa hawezi kufufuka na kujitetea.
  Uamuzi wa kususia rambirambi ya Chami kutokana na msiba wa marehemu Sonda, umetolewa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni baada ya Kamati ya mazishi kutamka kwenye majumuisho yaliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Cren kuwa haikuridhishwa na kauli alizotoa Chami ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), wakati akitoa rambirambi yake kwa marehemu (Sonda).
  Kaimu Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Lini Kamafa, alisema wao na kamati hiyo ya mazishi haikufurahishwa na kauli za Chami wakati akitoa rambirambi yake kuhusiana na kifo cha mwenzao, hivyo wanasusia rambirambi hiyo kwa kumrejeshea fedha yake yote.
  Kamafa akasema hawakufurahishwa na kauli iliyotolewa na Naibu Waziri huyo kuhusu uhusiano wake na Sonda wakati wa uhai wake na waandishi wengine wa habari mkoani Kilimanjaro kwa jumla.
  Akadai kuwa pamoja na mambo mengine, Mbunge huyo (Chami), anadaiwa kumtupia lawama marehemu huyo kwa kile alichodai kuwa alikuwa akimwandika vibaya katika magazeti.
  "Kwanza namchangia Sonda basi tu .... kwani alikuwa akinichafua... na nimeshawasaidia sana waandishi... nakutuma nenda kawaambie na ujumbe umefika, " mmoja wa waandishi hao akasema kwa kukariri maneno ya Chami.
  Kamafa akasema wamelazimika kurejesha Sh. 50,000 na kwamba kama Chami ataona hajatendewa haki, anayo nafasi ya kuomba kukutana na waandishi hao ili kuelezea malalamiko yao.
  "Kwanza Sh 50,000 tayari tumeshazirejesha kwake kwa kutumia simu yake ya mkononi... huko alipo tayari zitakuwa zimeshamfikia, " akasema Kamafa na kushangiliwa na waandishi wenzie wa mkoani Kilimanjaro.
  Sonda ambaye alikuwa miongoni wa waandishi wa Mwananchi Mkoa wa Kilimanjaro, alizaliwa mwaka 1962 na kufariki dunia baada ya kuugua kifua kwa muda mrefu na kuzikwa nyumbani kwao katika Kijiji cha Chekereni.
  Alasiri ilipomsaka Chami kwa njia ya simu leo asubuhi ili kuweza kupata maelezo yake, haikuweza kufanikiwa kwani simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita hadi kukatika bila kupokelewa.


  CHANZO: ALASIRI
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,392
  Likes Received: 81,396
  Trophy Points: 280
  Duh! Si ungetoa tu na dukuduku lako kubaki nalo mwenyewe!? Shilingi 50,000 tu unataka kumsimanga Marehemu!!!? Mwache akapumzike kwa amani.
   
 5. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Shame!
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  watu wengine bwana hiyo rambirambi kwani aliombwa atoe?jamani inabidi tuamng'oe huyu huko moshi vijijini ana nyodo sana huyu
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyu jamaa ana balaa sana Gubu la mke wake linamtafuna.
  Mikosi ndo imeanza hivyo dah na Ubunge sijui kama atarudi
   
 8. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  mke wake alifanyanini?
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  Sep 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Please Fidel Majibu..........adhere ot jf slogan homiiii!
   
 10. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #10
  Sep 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wamefanya jema sana ndugu wa wafiwa...Kama anaona hela zake ni ishu sana , basi azile yeye na familia yake..
  Shit damned him.. Kwahiyo amefurahia kifo chake siyo?
   
Loading...