Wazimbabwe walala nje ya mabenki wakisubiri kutoa pesa

Wazimbabwe walala nje ya mabenki wakisubiri kutoa pesa

amygdala

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Posts
1,082
Reaction score
999

_92254761_df16afae-d6fc-4c94-9c0f-3f1f5b9887d8.jpg

Image caption Zimbabwe iliacha kutumia sarafu yake mwaka 2009

Wazimbabwe si watu wa kutaka pesa zao kuchezewa hasa baada ya kuzinduliwa kwa noti ,mpya ambazo zina lengo la kusuluhisha tatizo la uhaba wa pesa nchini humo.

Picha za watu wakiwa wamelala nje ya mabenki wakisubiri yafunguliwe ili watoe pesa zao zimekuwa zikichapishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Gavana wa benki kuu Jonathan Moyo, alisema mwezi Mei kuwa noti hizo zitadhaminiwa na mkopo wa dola milioni 200 kutoka benki ya Africa Export-Import

Noti hizo za dola 5, 10, 20 zitakuwa na thamani sawa na zile wanazotumia za Marekani.

Zimbabwe ilianza kutumia dola za Marekani ilipoacha kutumia sarafu yake mwaka 2009.

Tangu wakati huo wazimbabwe wamekuwa wakitumia dola pamoja na sarafu za nchi zingine ikiwemo ya Afrika kusini ya rand na ya China ya yuan
Wazimbabwe walala nje ya mabenki wakisubiri kutoa pesa - BBC Swahili
 
huo ndio unaitwa uhujumu uchumi sasa

hahahhh
 
Huyu Mugabe chizi kweli.amtukana Obama huku anatumia USD.
Unajua issue ilikuwa kila Wazimbabwe wakitengeneza pesa zao zinakosa nguvu, mpaka walipofika kwenye hayo mabilioni wakaona isiwe tabu, wakamwambia mmarekani kama wewe ndio unashusha viwango vya pesa zetu basi shusha na za kwako wakaamua kutumia US$ na kweli at least mambo yakaanza kubadirika na watu wakaanza kuingiza vitu kwa sababu ya Dola
 
Mugabe amefika mwisho hawezi kufanya Zimbabwe ika improve kwa lolote zaidi ya kutaka kufia madarakani
 
Unajua issue ilikuwa kila Wazimbabwe wakitengeneza pesa zao zinakosa nguvu, mpaka walipofika kwenye hayo mabilioni wakaona isiwe tabu, wakamwambia mmarekani kama wewe ndio unashusha viwango vya pesa zetu basi shusha na za kwako wakaamua kutumia US$ na kweli at least mambo yakaanza kubadirika na watu wakaanza kuingiza vitu kwa sababu ya Dola
Uchumi mbovu tu marekani hana sababu ya kushusha sarafu ya Zimbabwe nchi masikini waache kuhangaika na uchina. Zimbabwe si tishio kwa uchumi wa marekani.
 
Hivi kwani hawa wameshindwa hata kumchomoa kwa nguvu madarakani huyo kikongwe?
7e13ec00d00f446a5d20fad7199340ee.jpg

"It is only when mosquitoes land on your
testicles that you realize there is always a
way to solve problems without using
violence".

Robert Mugabe.
 
Back
Top Bottom