wazichapa kavukavu

wazichapa kavukavu

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
KATIKA hali isiyo ya kawaida wanawake wawili ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara moja wamejikuta wakizichapa hadharani kugombania wateja eneo la Kariakoo jijini.
Wanawake hao ambao wanaojishughulisha na kuuza uji, walishikana mikononi majira ya saa 3 leo kugombania wateja huku kila mmoja akidai ni wake.

Hata hivyo mteja waliyekuwa wakimgombania kutokana na utu wake alilazimika kununua uji huo vikombe viwili kwa kile alichodai kumridhisha kila mmoja kununua bidhaa yake hiyo.

Biashara hiyo ya uji imekuwa na chati hasa maeneo ya jiji ambapo wanawake wamekuwa wakipitisha uji wa aina mbalimbali ukiwemo wa ulezi, mchele na muhogo na wamekuwa wakitembeza mitaani majira ya asubuhi na jioni kujitafutia riziki.
 
bora wamegombania mteje,nilijua ni ugomvi wa mwanaume.
maisha ni kukomaa hivyohivyo ipo siku watatoka.
 
huyo mteja ana busara sana hpe atakuwa ni mwana jf
 
Huku sasa kucholana nani alikuwepo yale maeneo, du kweli dunia haina siri.....
 
Back
Top Bottom