Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,854
- 30,198
WAZEE WANA USEMI "CHINI KUNAKWENDA WATU"
Picha hizo mbili hapo chini hazihitaji maelezo mengi ni picha za Abdul Sykes na Julius Nyerere na wake zao.
Picha ya Abdul Sykes imepigwa Government House katika Garden Party ya Gavana Edward Twining na mkewe Mrs. Twining miaka ya 1950 wakati akiwa kiongozi wa TAA.
Picha ya Nyerere imepigwa miaka ya mwanzo ya uhuru 1960s.
Wazalendo hawa wawili hakuna aliyefungua kinywa chake kueleza kuhusu urafiki wao wala kueleza historia ya kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Lakini kwa bahati historia za wazalendo hawa wawili zote zimeandikwa na kwa hakika ndiyo historia ya harakati ya kupambana na ukoloni wa Mwingereza kupitia chama cha TANU.
Wake zao Bi. Mwamvua na Maria Nyerere wameshuhudia yote kwa macho yao na wamesikia mengi kutoka kwa waume zao katika yale ambayo yalifanyika wakati ule.
Baada ya karibu miaka 20 kupita Bi. Mwamvua maarufu kwa jina la Mama Daisy alikutana na Mama Maria Ukumbi wa Diamond siku Mwalimu alipokuwa na mkutano wa kuwaaga Wazee wa Dar es Salaam mwaka wa 1984.
Mama Maria Nyerere alikutana na wanawake wa Dar es Salaam baada ya Mwalimu kumaliza hotuba yake ya kuaga.
Siku ile ndiyo kwa mara ya kwanza Mwalimu alimtaja Abdul Sykes hadharani.
Mama Maria alipomuona Mama Daisy katika kundi lile la akina mama, Maria Nyerere aliwaambia wale wanawake waliokutanika kumuaga, ''Huyu Mama Daisy na mumewe ndiyo waliotupokea mimi na mume wangu hapa Dar es Salaam.''
Maneno haya kanieleza Mama Daisy.
Ilikuwa miaka mingi imepita mashoga hawa wawili hawajaonana.
Prof. Shivji na jopo la waandishi wa historia ya Julius Nyerere, Prof. Saida Yahya-Othman na Dr. Ng'wanzi Kamata walipokuja nyumbani kwangu kunihoji kuhusu maisha ya Julius Nyerere alipofika Dar es Salaam niliwaomba wafanye juhudi wazungumze na Mama Maria kuhusu siku za mwanzo za TANU khasa ile mikutano iliyokuwa ikifanyika nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa Stanley na Mama Maria na Mama Daisy wakiwapo pale.
Sijui kilichotokea lakini kitabu kilipotoka imeelezwa kuwa Mwalimu aliishi nyumbani kwa Ally Sykes kwa miezi mitatu na imeelezwa kuwa chanzo cha taarifa ile ni Abbas Sykes.
Ukweli ni kuwa Mwalimu hakupata kuishi nyumbani kwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab Mtaa wa Kipata bali aliishi na Abdul Sykes na mkewe Bi. Mwamvua Mtaa wa Stanley.
Kidogo nilisikitika kwani kwa kosa hili mengi yamewapita yaliyofanyika nyumbani kwa Mama Daisy.
Wakati ule hakuna aliyefikiria hata kwa mbali kuwa Julius Nyerere atakuja kuwa kiongozi mkubwa sana ulimwenguni na jina lake litafahamika kote duniani.
Laiti Mama Maria angezungumza...