Wazee wa magari mtandaoni hasa hasa BEFOWARD

makaveli10

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
28,103
80,940
Baada ya kuona wabongo ni km tunaigana katika kuagiza gari, ambayo inapelekea na bei za aina ya hizo gari kupanda maradufu, leo nikasema nipitie befoward, kwenye filter nikachagua gari za chini ya dola buku $1000, matokeo yake yalinistaajabisha kidogo kuna aina za gari nimekuta bei kitola kiasi nimeshangaa

Picha zinasumbua kidogo, tuvumiliane.. Ataeweza atapandish.

Kuna hizi zimenivutia, sasa sijui tatizo nini hasa, au watu wanapandiana dau!?

1. Honda stream(2007)
$340
C&F $1422

2. Mazda axela sport manual transmission(2007)
$340

3. Vw passat variant(2007)
$350

4. Bmw 3 series(2007)
$600

5. Subaru impreza(2010) hii inaonekan iko njiani inakuja bongo.
$580

6. Honda step WGN (2010)
$510

7. Honda civic hybrid(2007)
$530

8. Noah(2005)
$400

9. Toyota mark x Zio(2009)
$640

10. Alphard (2003)
$710


Na nyingine nyingi ambazo sijaziweka hapa, wanasema ni punguzo la chrismas lakini mbona kwa gari chache tu, mfano mazda axela bei hiyo kitonga, ukitafuta nyingine ya mwaka huo huo bei ipo kwenye zaidi ya dola buku.
 
Kwenye kitonga lazima, kengele ya hatari igonge.

Mara nyingi hizo gari zinakuwa na conditioning ambayo siyo nzuri, utakuta zimekaa muda bila watu kuziulizia. Au ukiongea naye atamwambia sababu za hizo bei.

Pia, utatakiwa kulipa inspection fee, nadhani ni around $200, kuna charge nyingine siikumbiki, sijui insurance inakuwaje siku hizi baada ya sheria kusema tulipie huku Bongo.

Cha ajabu sasa, ukija na hesabu za TRA kwenye kodi, wao wana calculator ambayo si ajabu gari la $500 FOB ukalipa Kodi ya 5m mpaka kulitoa.

Ukichukua $500FOB+$200 inspection + Insurance na freight huwa ni around $1,000 una around $1,800 ambayo ni almost 4m, ukijumlisha na kodi ya 5m tayari ni 9m+.

In any case, huwezi kupata gari ambalo utalipa chini ya 8m mpaka kulitoa. Labda kama una watu TRA au exemption.
 
Tumekuwa na li nchi la hovyo sana! Huyu mzee sijui wanamhujumu au na yeye ndivyo alivyo?

Huu utaratibu kwa TRA ni wa toka nyuma, yaani wanakuchapa kodi ya ukweli.

Na ukisema ufanye appeal, gari linakuwa na storage charges zina pileup, maana linakuwa bandarini muda huo (wiki moja ndo muda usio na storage charge). Na appeal zinachukua muda kusort out.
 
The higher the demand....and vice versa. Kuna magari yanapendwa sana mfano IST haya obvious wauzaji wanajua trend wanapandisha bei. Na kuna magari yanaogopwa sana mfano Toyota zenye engine kubwa kama mark x na crown na Kwa upande mwingine zinazoogopwa ni Euro makes hii inafanya wauzaji wazishushe bei. IST inaweza kuuzwa bei Sawa na Crown/BMW haina maana hio IST ni Bora Bali ina wateja wengi.
 
The higher the demand....and vice versa. Kuna magari yanapendwa sana mfano IST haya obvious wauzaji wanajua trend wanapandisha bei. Na kuna magari yanaogopwa sana mfano Toyota zenye engine kubwa kama mark x na crown na Kwa upande mwingine zinazoogopwa ni Euro makes hii inafanya wauzaji wazishushe bei. IST inaweza kuuzwa bei Sawa na Crown/BMW haina maana hio IST ni Bora Bali ina wateja wengi.
Hii principle ndio ikanifanya nitafute magari ambayo kabla watu kuyashobokea mfano ist, rumion n.k bei bado bado..

Ndio nikakuta bei hizo lakini kabla ya yote lazima tuulizane ili kuongeza chochote kitu kichwani.
 
Back
Top Bottom