Wazee wa kujilipua kimaisha (risk takers) kwa style tofauti tukutane hapa!

Tupeni strategy, njia za kujilipua ma sio hadithi. Wanaojilipua halisi huwa hawajali ilimradi apate chake na akishapata ndio anakwenda kwenye malengo yake. Tupeni njia halisi sio stori

Mfano unatuambia kuwa ukitaka kupata million 30 kwa miezi miwili unapita hapa na hapa and the rest tunamaliza wenyewe. Risk takers tupo .na when it comes to it we never back down no matter what

Sent using Jamii Forums mobile app
nimeandika na kufuta mara nyingi nisijue ni lipi jibu sahihi la kukupa

Kama umesoma uzi huu toka mwanzo hadi mwisho na hujapata kitu bhasi this thing may not be for you maana ukisoma post za watu wengi ni kama wameamshwa na wanafikiria kuyarudia yale waliyoyaacha kutokana na mfumo uliopo wa kusoma na kupata ajira...

hiki kitu kinatakiwa kitoke ndani yako na uwe na hamasa ya kukiamini na kukiishi ili ukitimize ... kila mtu ana malengo tofauti na hatuwezi kuwa na njia moja kwa mfano ruge mutahaba wa sekta ya burudani na bakhresa wote walirisk lakini kwa njia tofauti

Kitu cha kwanza yakupasa kuwa na ndoto ama vision itakayokusukuma wewe kufanya lolote ili uifanikishe
ila mission ni wewe mwenyewe utapiga hesabu gani ili uyafikie malengo yako yaani hakuna "GENERAL RULE" .

Pengine waweza kufanya kazi katika makampuni yanayojihusisha na kitu ukipendacho ili kutengeneza experience na network , kuwafuatilia waliokutangulia kupitia vitabu vyao ama mahojiano nao ama waweza kuanza na biashara itakayokuPa financial muscles yaani njia zipo nyingi na ni wewe tu wapaswa kuwa na passion ya kitu unachotaka kukifanya na kujitolea kufanya research ili upate uhakika zaidi..
The more you work on it ,the more clearer it becomes

Usiwe mvivu .. Jihangaishe na jiamini
 
I wish you could impact me with reality of this ideas of you. I wish I could have power to impliment this or knowing where to start. am so desperate

Sent using Jamii Forums mobile app
Its never too late to start again.
The reality of all these ideas depends on how willing you are in making them real.

Jitathmini, umetoka wapi, upo wapi na unataka uelekee wapi. Kama upo pabaya, nini kimekufikisha hapo?

If you manage to do that, only the sky could be the limit!

- KANA -
 
-KANA- kwa maisha ya bongo kuacha kazi na kwenda kusoma masters USA sio risk at all in fact unajiongezea fursa kwenye maisha yako.

Risk ni kuacha kazi nzuri USA kuja kujaribu maisha bongo.
Sio kweli unayosema bwashee hata kuacha kazi nzuri bongo kwenda US ni Risk pia maana sio kwamba ukifika America basi ndio mambo yako yawe mazuri, ni lazima upambane haswa ili kulifikia lengo lako lililokupeleka huko. Wewe unaleta mawazo kama ya wabongo walio wengi kufikiria kwamba ughaibuni pesa ziko kwenye miti kama matunda vile yanadondoka..kuna watu kibao wanafika majuu na bado wanachemsha wanaona bora wangejikalia bongo waendelee na kazi zao.Usiwadanganye watu hapa bana tunapeana mauzoefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau wanaotaka kujilipua mlioko kwenye hii thread huu ndio muda muafaka wa kuanza application ya Green card lottery na deadline ni October.
Angalizo: muhimu kuicheza/ apply kwenye genuine website ya US govt. Kuna nyingine za kitapeli zitawalia pesa kuweni makini ukiona t inayotaka fees achana nayo. Tz tuna nafasi kubwa sana ya kupata maana wakenya wamecheza sana hio.kila la kheri wadau; kazi ni kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutimiza ndoto yako na kuchukua risk ni vitu viwili tofauti. Unaweza kutimiza ndoto bila ku-risk au unaweza kutimiza ndoto kwa ku-risk.

Huyu alikuwa na ndoto ya kwenda USA kaenda via legal channels, safe and acceptable way,education. Mwingine alikuwa na ndoto ya kufika USA kazamia meli kashushwa Afghanstan, kakaa pale miaka mitano kapita boda kwa boda katokea Russia huko then kazamia tena meli kafika USA.

Hawa wote wawili wametimiza ndoto yao ya kufika USA ila alie-risk ni mmoja tu hapa.

Kwa hiyo ku- risk kwako ni kupata "tabu"
 
Wadau wanaotaka kujilipua mlioko kwenye hii thread huu ndio muda muafaka wa kuanza application ya Green card lottery na deadline ni October.
Angalizo: muhimu kuicheza/ apply kwenye genuine website ya US govt. Kuna nyingine za kitapeli zitawalia pesa kuweni makini ukiona t inayotaka fees achana nayo. Tz tuna nafasi kubwa sana ya kupata maana wakenya wamecheza sana hio.kila la kheri wadau; kazi ni kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni vizuri ukawarushia link hapa mkuu kama utaweza.
 
Sio kweli unayosema bwashee hata kuacha kazi nzuri bongo kwenda US ni Risk pia maana sio kwamba ukifika America basi ndio mambo yako yawe mazuri, ni lazima upambane haswa ili kulifikia lengo lako lililokupeleka huko. Wewe unaleta mawazo kama ya wabongo walio wengi kufikiria kwamba ughaibuni pesa ziko kwenye miti kama matunda vile yanadondoka..kuna watu kibao wanafika majuu na bado wanachemsha wanaona bora wangejikalia bongo waendelee na kazi zao.Usiwadanganye watu hapa bana tunapeana mauzoefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Niwadanganye ilu nipate faida gani? Uzoefu tunaoongelea hapa ni pia 'chances'. Hata huku kujilipua mnakozungumzia asilimia kubwa hawafanikiwi,wengi wanafeli. Na hapa tnazungumzia mtu alieacha kazi kwenda kusoma masters kama wewe na si mzamijaji tu. Hata ukirudi na masters yako una nafasi nzuri zaidi kuliko ulivyoondoka.
 
Naomba MUNGU Baada Ya Mwaka Mmoja Nitarudi Hapa Kuja Kutoa Ushuhuda Sasa Hivi Bado Nipo Chimbo Baada Ya Kujipua
 
Sio kupata tabu. Ni hatari au hasara au upotevu unaoweza kuupata kwa kiu yako ya kutumiza ulichokusudia.

Kwahivyo tunakubaliana kwamba jamaa aliacha kazi ya kwanza kasota pamoja yakuwa anayo degree.Kapata kazi tra noti ndefu kaacha.Kaenda usa kasoma na kuishi huko.
Tukijumlisha vyote (jamaa) alipata hasara kimaisha na kifamilia (kwa kiu yake ya kutimiza alichokusudia) na sasa anavuna alicho panda.
Mkuu PRONDO ungefurahia mafanikio ya huyu mwanaJF kama angekua std 7 na alikuwa anauza maji mjini.
Hongera zitolewe zinapostahili.
 
Asante chief,
Kwanza mtu anaetaka kutakeRisk lazima ajichinguze mwenyewe kama yupo fit japo sio sana lkn atleast uwe fit kwenye kuvumilia na kusimamia misimamo yako,

Jinsi unavyozidi kusimamia misimamo yako na kuvumilia ndo unavyozidi kukomaa ktk haya mambo....maana kuna wakati lazma ujikute peke yako na umezungukwa na wakosoaji, wakatishaji tamaa, na wengine watajaribu kkuzuia kabisa.....

Ss kama ukiwa sio mvumilivu na huna msimamo itakua kazi bure tu,

Kama hujawai kulia basi jiandae kisaikolojia mana lazima utalia tu....na naposema kulia sio lazima ulie kwa sauti na kugalagala HAPANA, hapa utajikuta machozi yanakutoka tu mfululizo tena yakiwa ya moto kabsa,

Kwa upande wangu machozi yamekuwa ni faraja kipind fulani....nlijikuta nipo kwny wakat mgumu..wazaz hawanielewi...ndugu ndo kabisaa...marafik wanakushangaa tu,
.....nlikua natafuta muda na mahali nakaa peke yangu na kutafakar maamuzi yangu.

Nashkuru Mungu amenipa Moyo wa kuvumilia kwkweri....

Jambo langu la kwanza lililonipa ujasiri ni siku niliyomgomea mzee wangu kwenda Advance...nlikua na sababu zangu na misimamo yangu ambayo ad ss mzee hajawai kunilaum tena kuhusu yale maamuzi,

......pia nakumbuka Risk nyngne ni pale nilipo amua kuacha kazi ktk shirika fulani ili nijaribu kufanya mishe zangu mwenyewe, aisee hili ndo lilikuwa kubwa kuliko mana si wazazi, marafik, girlfrnd, wachungaj na wazee yani wote walinishambulia hakuna mfano...

....nilipiga moyo konde nkakomaa na msimamo wangu, girlfrnd akasepa marafk wakanilaumu, wazaz na wachngaj ss kila siku ilikua kunisema tu....ofcoz kuna kipnd maneno yao yanakugusa kias kwamba unawaza kwnn ulifanya vile...lkn kitu kimoja kilinipa nguvu nilipo kumbka tu shuruba za kuamka alfajir kurudi usiku hoi...af mwsho wa mwez laki nne na nusu

Nkasema hapana kwkwer sirudi kule aisee....

Kwhyo jaman tunapotaka kuingia kwenye hii kitu tuwe tayar kwa haya yote na mengine mengi.....

Swala kubwa lingne hapa ni kutokuwa limbukeni wa POMBE...
Ukiwa mpenz wa hizo mambo alafu ukajijengea taswira kwamba pombe inaondoa stress aisee utafaidisha watu maana utakunywa adi ubadilike rangi...

Jiandae kuptia haya:-

Kulia
Stress
Kuachwa
Kusemwa
Kutengwa
Kujichukia
Kukosa muelekeo mwanzon

MUNGU NDIO FARAJA PEKEE YA KWERI KTK KIPINDI HIKI......
Kiukweli unanitia moyo ingawa sijafikia kiqsi hicho ila unachongea kinaualisia sana...najua ndo maana nakubaliana na ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aah! Aisee, mbona unaniongelea mimi! Haya maamuzi niliyafanya miaka 21 ilopita. Wala sijutii, na kichekesho zaidi, aliyekuwa bosi wangu miaka hiyo, leo hii anapiga kibarua kwenye moja ya vitega uchumi vyangu. Confort Zone ndo inayowaathiri waajiriwa na wasomi wetu wengi.
Mkuu naomba ufafanuzi juu ya Comfort zone

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana watu tumeomba tushauriane na kuelewesha haya mambo humu,
Kufata mkumbo ni mbaya sana maana utakua hujui nn unataka...ila ukiwa na malengo na mipango yako madhubuti huwezi kushindwa,

Kuacha kazi au shule kisa fulani ameacha na hujui sababu za yy kuacha ni tatizo hilo, dunia hii kila mtu na maono yake...kila mtu na mapito yake ss mtu ukisema uvae viatu vya mwenzio na hujui anavaa namba ngapi kuna mawil either VIKUBANE au VIWE VIKUBWA, uwezekano mdgo sana KUKUTOSHA.

kwhyo ni heri kuwaelimisha kuliko kuwatisha vijana, kila mtu anataka kuwa tofauti.

"Take Risk at your own Risk"
Comments kama izi lazima zitokee ili kukupa nguvu mtu mpambanaji,tusiogope

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba ufafanuzi juu ya Comfort zone

Sent using Jamii Forums mobile app
Mfano...

Uko home kwa baba ako..unapata maji..chakula...vocha...inshort unapata kila kitu unachotaka!!

Sasa hii ni moja ya comfort zone...

Mara nyingi comfort zone zinafanya isione uhalisia wa dunia ulivyo na itakufanya ujione uko safe kumbe you are not!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom