Wazee wa kujilipua kimaisha (risk takers) kwa style tofauti tukutane hapa!

RAGNAR LOTH

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
698
1,589
Vichaa / Wehu / Wasiojihurumia kama ambavyo tumezoea kuwaita ndio wanaoifanya hii dunia ikasogea mbele. Amini usiamini kama hujawahi kufanya jambo ambalo kila mtu wa pembeni yako akakuona unaenda kujimaliza / hutatoka mzima, bado hujaishi Joh, " You are still dwelling in your comfort zone".

Chunguza watu waliofanya wonders in life, they sacrificed their lives, reputation, even their parent's trust. Kama wewe kila ulichokifanya nyomi iliyoko nyuma yako ilikupa support bado hufai kujiita successful man/woman. Successfully people are few, Minority na sio Majority.

Kuna watu wanachukua maamuzi ya kuacha kazi hali wakiwa mifuko mitupu kabisa. Mtu kama huyo akija hapa akaomba ushauri " Nataka niache kazi nijiajiri ila sina hata mia mfukoni ". Majority ya comments atakazopata hapa ni kumuona mpumbavu na mtoto na asiye na life experience. Atatahadharishwa kuisoma number hadi akome.
KWA NINI? Kwa sababu wanaomshauri hawajawahi ku take risk kama hizo, they are doing nathing rather than Screaming., Hawajawahi kuwa risk takers.

Kuna watu waliamua kuahirisha kama sio kuacha kabisa masomo yao ya elimu ya juu hali wakiwa hawana kitu kwenye mifuko yao, hawakujua wangeanzia wapi, lakini leo hii ndio madereva wa hii dunia..

Believe me or not asikudanganye mtu akakwambia Jiajiri huku umeajiriwa huyo ni screamer not a risk taker.

Failure zipo kila mahali, kila siku,kwa kila mtu, they are "Inevitable". Ukianguka ukalala hapo ndo pana tatizo. Kila mtu keshafeli kwa kitu fulani hata unaowaona wamefanikiwa walishafeli mara nyingi mno asikwambie mtu. The road to success is rough x 100 Joh, and only few dare to take.


Nimeamua kuanzisha huu uzi ku share mastory za kujilipua kimaisha kuwapa courage wale wote wanaotaka kuchukua maamuzi magumu in life. Wazamiaji wa mamtoni, waacha vyuo/shule kama mimi, waacha kazi, waliofukuzwa makwao na wengineo ili risk takers msijiskie wapweke au mko wenyewe.



"Taking risk is the quickest way".



Nashauri kwenye uzi huu tuelimishane na kushauriana kuhsu hili swala "Taking risk" mana wengine watakuwa hawaelewi,

Mtu asije akakurupuka tu akaacha kazi au shule bila kujua yeye anapenda nn au anataka nn ktk maisha yake....

Taking Risk is very Risk indeed, na inakuwaga na matokeo mazuri baadae ikiwa mtake Risk anajua anachofanha otherwise watu watalia...

Sio kama nawatisha wale ambao bado hawajaingia kwenye hii Saga NO....am just trying to give out a light,

Moja ya faida ambayo imenifanya nienjoy kutake Risk ni kuwa huru na furaha na nnachokifanya, for i know where im coming from...where i am...and where i will be,

Tushauriane, tupeane changamoto na jinsi ya kuzikabili.

Nipo tayar kukosolewa hapa pia...


Nakumbuka mwaka 2003 mdogo wangu alipata division 1 point 8....mshua alifurahi sana sana...cha ajabu alikataa kuendelea na shul ...huku na huku vikao vingi kwake mpaka wazee wa kanisa, kachomoa hataki shule....akafukuzwa dogo kakimbilia zambia baadae congo...

kwa sasa ni muuza madini na anatenda za machinery aina mbal mbal nchin zambia na congo...
Mm nina degree Mavi matupu nimebaki baraka ya kumuomba omba pesa mara ooh dogo mara vile .....na mwakan anasema anarudi shule sema atasomea marekani
maisha haya acha tu..........


Nataka anza biashara ya mabucha mjini hapa,kuna vitu hela unaziona kabisa halafu unakuwa tu mkaidi kuzifuata

Nimegundua kila mradi ambao huwa nawaza nikikaa siku chache sana nakuta mradi uleule sehemu ileile plani ile ile Kuna mtu kaanzisha,nikaja kujitathmini kuwa Mimi Nina mawazo sana ninachoshindwa ni kuchukua hatua tu,sasa nimekata shauri kuwa sahivi basi naanza kufanya mwenyewe,Uzi huu nitakuja ufufua mwaka mmoja toka Leo note 8-8

Sent From fx.991


SIO KILA RISK TAKER ANAFANIKIWA MKUU,
KUNA MTU ALIRISK AKACHUKUA KIASI KIKUBWA CHA HELA AKAENDA KUHONGA WATU ILI WAMCHAGUE MTU FLANI BAADAE APIGE HELA NYINGI KAMA AKIPITA LAKINI TANGU SIKU ILE MAMBO SI MAMBO, MARA HELA IMEKAMATWA KABLA YA KUGAWIWA ,MARA BIASHARA YAKE HII INA SHIDA..........LEO YUPO JELA NA BIASHARA INAYUMBA.
ILA YOTE KWA YOTE RISK TAKER NI UJASIRI KATIKA KUTAFUTA MAFANIKIO KULIKO WAOGA KATIKA KUTAFUTA MAFANIKIO



NI miaka 6 sasa toka nilipofaulu baba yangu akakataa kunilipia Ada niende advance akadai hawez poteza pesa zake kwa mwanamke kama vipi niolewe tu.nikiwa Na miaka 19. Niliteseka huku Na kule kuishi Kwa ndugu bila future. Mungu siyo Athumani ikawa ilivyokuwa sasa hivi ananiona kama Mkombozi wa ukoo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app


Namengi sana ya kushare....still nipo kwenye progress at times nakaa natoa chozi peke angu lakini naamini mambo lazima yawe mazuri very soon....ndugu walinigeuka, shule nilikataa nkaenda chuo, chuo nkafukuzwa home wakapata sababu ya kusema too bad nkarudi home week ya kwanza ukatokea msala mekaa kwenye pool table jion nina mawazo kibao gafla tukakamatwa tukatiwa sero, ndugu wakazidi kusema.....kwa sasa atleast kuna baadhi ya ndugu washaanza kunipigia simu na kuniomba chchte....am still fighting for my own...i hope a year ahead i will be somewhere....nkiwa na elimu yangu ndogo kwani chuo nliona upuuzi tu, mtaani kuna fursa sana tu.... A year ahead ntakuja kueleza ni nini nliamua kufanya na hatua gani nlizopiga....i remember kuna maamuzi ya risk nshawah kufanya mpaka leo sijutii hata kidogo.

 
MY STORY :
Katika umri wa miaka 19 nikiwa nimemaliza tu kidato cha sita niliamua kutoendelea na elimu yangu ya chuo kikuu ingawa nilikua na ufaulu wa mzuri. Kulikua na mvutano kati yangu na mzee wangu juu ya career yangu ya baadae. Nilitaka kuwa mfanya biashara lakini alitaka niwe engineer. Ilipelekea yeye kunifukuza home hakutaka kabisa kuniona. Niliondoka na ndio nilivyokuwa nataka, alimpiga tu chura teke.

Mara moja nikaanza harakati nisijue hata wapi pa kuanzia nikawa kama nabahatisha, nikiwa sina hata mia mfukoni nilikuwa na pesa tu ya kodi ya chumba. Nililala njaa mara kadhaa nisiwe na wa kumlilia mjini hapa hata ndugu walinikataa,na marafiki nao bado wanaishi makwao wengine wakiwa bado shule. Nlisimama na kuishi kama moja. Kuna muda nlitamani kurudi nikaombe msamaha lkn kila nlipokumbuka mtu ambaye nataka niwe nikapata nguvu ya kuvumilia maswahibu.

Mungu si athumani baada ya kama miezi 10 ya njaa kali nikatengeneza mrija wangu mwenyewe wa income japo ulikua mfinyu ulinipa moyo sana wa kuendelea. Leo hii naaproach 30 hakuna hata mmoja kati ya classmate wangu anaediriki kusimama kifua mbele kwangu( Sijisifu ) na wengine wengi sana nimewaajiri. Nimepata tena vyote nilivyopoteza, nina marafiki kibao, ndugu wameongezeka hadi waliojificha awali, trust ya mzee imerudi maradufu, na elimu nategemea kuipata tena katika chuo maarufu hapa duniani mungu akipenda.

Risk taking, Hard working, and Perseverance always pays..

NILIWEZAJE KUTOKA HALI NIKIWA MIFUKO MITUPU.?

Naanza nyuma kidogo historia yngu kwa kifupi.:
Nikiwa shule ya msingi nilijitambua kuwa nimezaliwa na kipaji cha utunzi : Nilifanya composition za aina nyingi, mashairi na ngonjera ,hadithi na maigizo sana sana. Kanisani kwa vipapa nakumbuka enzi hizo kwa wale wakatoliki nilikuwa ndo gwiji wao wa kuwaandalia composition zao. Mashairi, ngonjera, na maigizo kwenye sherehe zote za darasa la saba walinifuata mimi katika umri huo huo mdogo niliokuwa nao, walimu walizipitia na kuzifanyia marekebisho madogomadogo tu.

Nilivyokuwa naendelea mbele mzazi alinipiga marufuku kwa kuona kwamba naenda kupotea. Nilisoma shule ya bweni elimu yangu ya sekondari, kwa hiyo kule nilikuwa tena mbali na mzazi nikaendeleza kazi zangu zile zile, siku za masherehe nawaandalia composition wanazotaka kwa kuwa kipji changu kilionekana wazi, kwa hiyo walinijua mapema.

Nikafaulu kwenda kidato cha tano , sasa hapa ndo tulikuwa na mvutano na mzee wangu, alinitaka nisome science mi nlitaka art kutokana na moyo wangu ulivyonituma yaani, ingawa nilikuwa nimefaulu vizuri masomo yote. Alifanikiwa kunilazimisha nikasoma hiyo science aliyoitaka. Nilipomaliza kidato cha sita nataka niende chuo ndio roho ya kujilipua iliponijia sasa. Sikutaka kumskia mtu yeyote, wengi waliniona nna kiburi, nimelaaniwa, wengine nimelogwa, kama nilivyosema hapo juu wote walinitenga kutokana na maamuzi yangu, nikabaki nimesimama mwenyewe kama moja.

Nilipofukuzwa home, nakumbuka maza alinipa 40,000/= na niliondoka na godoro na vitu vyangu vidogo. Niliitumia hiyo kulipa kodi ya mwezi tu 10,000/= nikabaki na 30,000 ya kula sikutaka niitumie kwa vitu vingine kwa sababu sikuwa na wa kumlilia.

Nilikuwa na ndoto za kuandika kitabu changu cha story kwa kuwa niliamini nikikitoa lazima kiuze kwa kuwa niliamini nna kipaji kikubwa. Kipindi icho sina cha PC wala Desk top, niliandika kwa mkono. Nakumbuka nilikuwa na mtindo wa kusoma vitabu vya mbele vya akina George Clason, Ben Carson, Paulo Coelho, Napoleon na wengineo ambavyo nilinunua kwa pesa yangu kipindi niko shule. Vilinipa mwanga sana wa kuandika kitabu chenye nondo za ukweli. Nilisom na vya watanzania akina Ben, nililinganisha nikaona weakness ya vitabu vya TZ viko too theoretical, yaani mtu akimaliza kusoma anakuwa haja gain chochote kipya zaidi ya hadithi za kufikirika tu.

Kwa hiyo nilitaka nije na kitaabu ambacho mtu ata gain anad at the same time aburudike. Nilitumia six months kuandaa hicho kitabu. Of coz pesa nliokuwa nayo ilikata nikabaki mimi na godoro langu tu, na kodi lishaisha kitambo, lkn Mungu si Athumani mzee mwenye nyumba alikuwa ni mtu mwelewa sana, alinifanya kama mwanae, akinitia moyo hata msosi alinihudumia pia, yaani nilikua sehemu ya familia yake tu, Mungu amweke mahali pepa peponi huyu mzee.

Nilipomaliza kukiandika hicho kitabu kimbembe kilikuja time ambayo nataka kufanya editing na printing ili kitoke sasa, sikujua nianzie wapi yani nilikua natanga tanga tu, mara niende mkuki na nyota mara wapi sijui na nilivyokua mdogo nilikuwa nafukuzwa kama ka mbwa kalichoingia ndani, sikupewa hata nafasi ya kusikilizwa. Lkn siku moja nakumbuka nilikutana na classmate wangu tulisoma wote huko nyuma, katika story akanambia baba ake ana kampuni ya publishing ( sitaitaja jina). Nikampa mkasa wangu mzima ikabidi binti ajitose kunipa support. Aliongea na baba yake akajitahidi kunielewa, na akanipa ushauri kwamba kwa kuwa nilikuwa bado Author mchanga nikiuze kile kitabu kwa mwandishi maarufu yeye akitoe kama chake. Ilikuwa ni ngumu lkn ikanibidi nikubaliane nae kwa kuwa hata ningesema niprinty kwa jina langu bado ata iyo pesa nilikuwa sina. Yule mzee na yeye alikuwa ni mwandishi pia kwa hiyo yeye alinisaidia kuhariri kile kitabu bure bila malipo, alishangaa kwanza alipokisoma akidhani nime copy sehemu kilikuwa na nondo za uhakika. Alikiingiza kwenye mtandao ili kuona kama nika match na kitabu chochote lkn akagundua hakikuwapo kinachofanana nacho.

Aliwatafuta waandishi kibao wa TZ tufanye bargain nao na tuingie mkataba lkn tulishindwana bei, walikuwa wananichukulia kwa kuwa mtoto na sina jina kutaka kunikandamiza na mimi nikawa mjanja niliwapa mkwanja ambao hakuna aliyeweza kufika, yule mzee nae alipoona tumeshindwana akataka nimuachie yeye lkn nae tulishindwana. Kwa kuwa alikuwa na chennel na waandishi wengine , nakumbuka kulikuwa na mwandishi maarufu wa nchi fulani hapa hapa Afrika alikuwa anakuja DSM kwenye kongamano sikumbuki lilkuwa linahusu kitu gani hasa. Akanambia atanikutanisha nae nijaribu kuongea nae kama ataweza kufika bei nimwachie kitabu akakitoe yeye. Alifanikiwa kunikutanisha nae tukaongea na akawa tayari kufika ilo dau lkn akasema tumpe mwezi mmoja akakifanyie tathmini, kwa hiyo tulisaini form za "NON DISCLOSURE", na hatua zingine. Alikuwa mtu na heshima zake sio rahisi kuiba au kukitoa bila makubaliano.

Alitimiza aadi yake baada ya mwezi alinitaka niende nchini kwake. Mfukoni hapo hata pesa ya kula sina, mzee yule yule aliyeniunganisha nae akanipa support kwa kuwa alijua naenda kupiga mawe soon. Basi nikaenda tukamalizana, nika saini mkataba nae na akanikatia % kidogo na % nyingine nikawa na share kwenye kila copy inayotoka. Baada ya miezi mitatu akakitoa kile kitabu ndo hadi leo mkwanja unaingia, kiliuza sana kuliko kawaida, na bado kila kukicha kinauza.

Mini niliamini kama kipaji ninacho siwezi shindwa kutoa tena nondo nyingine kwa jina langu, kuna vitu vini sana vya kuviandikia duniani hapa. Namshkuru Mungu, niliweza kutoka kiivyo. Na huo ndo ukawa mwanzo wa mimi kutimiza ndoto za kuwa mfanya biashara, nikaanza biashara from that time on out of nathing, kipaji kilinibeba sana. Leo hii my food Co. inaenda vizuri and i feed the Tanzanians na wana East Africa.

Kuna mambo mengi tuna uwezo nayo ujue halafu hatuyatilii maanani lkn tukiamini na kuyakomalia kwamba yatatutoa yanatutoa kweli, na sio kidogo, Mi sikubaliani na wanaosema kipaji mbele hata bongo hapa kipaji kinabeba sana tu.

All in all kuna nyanja nyingi za kutoka, this story of mine usiichukue kama iliyo ukaenda kuitumia, hutofanikiwa kama hukua na ndoto hizo, naamini kila mtu ana kitu ndani yake shida inakuja kutojiamini kama kweli unaweza. Humble beginning isikuuumize kichwa ukakata tamaa, things must work out for themselves wakuu. You only need to have a strong belief on what you are doing.
Wengi mlinitaka niweke my story hapa na nimefanya hivyo wakuu.


RRONDO, relato, newazz, Justice minister, https://www.jamiiforums.com/threads...ti-tukutane-hapa.1298011/reply?quote=22721300, https://www.jamiiforums.com/members....jamiiforums.com/members/jimmy-jimble.414202/, Kichwa Kichafu, muxar, Mdumange, mwajex, Remote, Complicator, King Jaffer Joffer, Sonia G,jabulani2017, https://www.jamiiforums.com/members...://www.jamiiforums.com/members/kurunzi.17757/

ganja gal, Mr Miller, 1kush africa, Ollachuga Oc, KakaJambazi


 
mambo mazuri ila yanahitaji kujikana nafsi na mwili...

mtu aliyenihamasisha kupenda hesabu, pamoja na kufauru vizuri aliacha kwenda chuo akakomaa na kazi akasomesha wadogo zake wote. kwa ushirikiano na mkewe leo bado ni bank officer lkn anavitega uchumi ambayo sidhani kama manager wake anamfikia na watoto wake anawalipia india vyuo kuanzia certificate hadi degree.
maisha yake huwezi kuyatenganisha na nidhamu ya pesa na hardworking.

ninajifunza vingi hasa kwa watu ambao nimewaona mubashara.

big up mkuu. huo ndio urithi wa maana kwa wazao wako
 
Najua wako wachache mno wa design hii.
Sitashangaa hii siredi kuwa mwana mkiwa.
Mkuu hauwezi kuwa mwana mkiwa. Ni vile some of us kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu hatuwezi kureveal hapa jukwaani risks tulizowahi kufanya.

But huu ni bonge moja la uzi, hasa kwa wale wasioamini katika kesho, waoga wa maisha na kujaribu na wanaoamini mafanikio katika kuajiriwa.

Note: "Success does not consist in never making mistakes but in never making the same one a second time" George Bernad Shaw
 
Nakumbuka mwaka 2003 mdogo wangu alipata division 1 point 8....mshua alifurahi sana sana...cha ajabu alikataa kuendelea na shul ...huku na huku vikao vingi kwake mpaka wazee wa kanisa, kachomoa hataki shule....akafukuzwa dogo kakimbilia zambia baadae congo...

kwa sasa ni muuza madini na anatenda za machinery aina mbal mbal nchin zambia na congo...
Mm nina degree Mavi matupu nimebaki baraka ya kumuomba omba pesa mara ooh dogo mara vile .....na mwakan anasema anarudi shule sema atasomea marekani
maisha haya acha tu..........
 
Back
Top Bottom