Wazee wa kimila au machifu mnatengwa. Hili nalo mkalitazame

Mzalendo120

JF-Expert Member
Jul 2, 2022
1,431
1,845
Ndugu wanajukwaa habari zenu. Moja kwa moja kwenye mada.

Nimekua nikifuatilia au kuona shuhuli mbalimbali za kiserikali zinazohudhuriwa na viongozi wakuu wa nchi.

Kabla ya kuanza kwa shuhuli hizo tunashuhudia dua au maombi mbalimbali kutoka kwa viongozi wakiroho kutoka pande mbilitu ambao niwaislam na Wakristo.

Ukiachilia mbali madhehebu mbalimbali yanayopatikana kwa waislam na wakristo baadhi yao kutoshiriki mara nyingi kama sio mara zote,ninaona kuna kundi limetengwa kabisa.

Kundi la watu wakitamaduni au wapagani pamoja na machifu hawashirikishwi katika kuombea mikutano au shuhuli hizo. Jambo linalonishangaza, nipale ambapo vipindi vya uchabuzi wazee wakimila wanaitwa wakiwa wamevaa mangozi yao na mamikia yao ya mifugo.

Kwanini hao wazee wanatengwa? Au hawawezi kuombea mikutano na vikao mbalimbali?

Au miungu yao haiaminiwi kama inaweza kuleta ahueni kwenye shuhuli hizo?
Au nikwanini viongozi hao wasiendeshe sala zao kama bunge ambapo makundi yote hayatohisi kutengwa?

Mnaowatenga wazee hili nalo mkaliangalie
 
Mkuu wapagani hawana dini sasa unataka wakaombee kitu gani? 😂😂😂😂
 
Hata hao viongozi wa dini huwapaswi kuitwa kwenye hayo matukio ya kiserikali, kwenye kupokea ndege wanaitwa viongozi wa dini ili kufanya nini??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom