Wazee wa kiingereza

Mr Surplus Economy

Senior Member
Joined
Mar 19, 2018
Posts
174
Reaction score
166
Wakuu heshima kwenu. Hali ya ajira imekuwa ngumu baada ya kukaa mtaani na fani yangu ya Bachelor of human resource bila ajira nimeona nijiongeze nifundishe ata kingereza tuition angalao mkono uende kinywani. Sasa kuna sehemu nimepata hapa tuition Centre nimeunganishwa na jamaa yangu naona afadhali nipige japo kwa msaada wa material mtandaoni siku yapo ya kutosha tu

Changamoto inakuja nimekabidhiwa wanafunzi wa form two nimemuuliza mmoja alipo ishia amenionyesha ni kweny comparative and superlative form

Sasa changamoto inakuja kwamba baada ya hapo sijui inatakiwa afundishwe concept zipi ama tuseme hiyo topic huwa inakuwa na vipengele vipi kwa mfuatano hadi iishe? wenye ujuzi tujuzsne apo waeshimiwa
 
Kuna app tofaut ukijiunga unaweza kuona topic za kila somo, mfano shule app, wanafunzi waliitumia kipindi cha corona outbreak..
 
kuna dogo mmoja amemaliza environment degree mwaka jana, sasa hivi kajishikiza kama buyer / procurement, anapata walau hela ya nauli kwenda job na kurudi - mchana ana desh.

Nimemwambia aanze kusoma kozi za uhasibu mdogo mdogo, sasa hivi kuchagua hakuna ndgu, lilipoangukia ndipo huko huko unaanzia kuchuna.
 
Mkuu unamshauri asome tena kozi hizi ambazo ni pasua kichwa we mwambie kama ana akiba aende Veta akasomee skills mbali mbali mfano uoperator wa machines, ufundi like wa magari, bomba, umeme nk.nk yani huku ndio kuna lipa kwa sasa mkuuu
 
Ukifata syllabus ya bongo kufundisha English itakuletea changamoto sana.Kama unaweza mfundishe concept nyepesi ambazo zitaweza kumjenga katika kuongea,kusikiliza,kusoma na kuandika nazo:Tense,word classes,singular and plural forms,conditional sentences,speech writing,essay writing,event analysis etc.kama unaweza literature zuga na plays kama mbili afu funga hesabu zako

Kila la kheri home boy
 
Yap mkuu nimefanikiwa kupata shule direct nimeputia syllabus naona kweli ukifatilia haionyeshi baadhi ya concept za kuwafundisha wanafunzi especially kwenye grammar kama ulivyosema mkuu. Nitapiga hivo hivo kibingwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…