VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Ngoma ya kitoto huwa haikeshi. Vijana ndani ya CCM walijichora kama ndio wenye chama na wafiachama kuliko sisi wazee waliotukuta chamani. Tuliwapokea na kuwalea lakini wakatupoka chama na kutuweka kando kama simu simu isiyo na bando. Wakakiteka na kukitesa chama. Filamu zote za kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ni matunda ya hayo niliyoyasema.
Ushindi si kama kupanda mahindi. Ushindi, wakati wetu chamani, ulitokana na kuachia uwanja wa siasa na kupumbaza kuwa kulikuwa na usawa. Halafu, kura zilitubeba. Tulijitahidi kuonesha kwa mtazamaji yeyote kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ingawa tulikuwa na maandalizi yetu ya kichama na kidola kuhakikisha kuwa kura hazituangushi.
Wabobezi wa kisiasa chamani tulikuwa tukiulizwa cha kufanya na tulishauri bila kiburi. Tulishauri kuwa demokrasia, hata kama haipo, lazima iwepo. Lazima ioneshwe kwa watazamaji kuwa ipo. Wakati wa kuhesabu kura na kutangaza matokeo, hatukuwa na msalia mtume. Hata mabomu yasiyo na hamu yalitumika ili matokeo kueleweka. Tukapambana hadi mahakamani.
Kwa uchafuzi na filamu inayoendelea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sisi Wazee na Makada Waandamizi wa CCM tunawaomba radhi ya wazi. Waandalizi na wasimamizi wa uchaguzi huu wamekuwa vichekesho. Hata wao kwasasa wanajuta kufanya walivyofanya na hawajui watokaje kwenye mkwamo huu. Wamebaki kujiongelesha, kujikasirisha na kujichekesha.
Sisi Wazee wa CCM tunajua kuwa viongozi wetu Vijana wa CCM ndiyo walioishauri vibaya Serikali kuhusu chama chetu kupata ushindi wa kihistoria. Kuhusu kupata ushindi wa kishindo kama nyundo. Waliendeshwa na mihemko ya kutaka kutufunika kwa mafanikio ya kiuchaguzi. Sisi Wazee tupo kimya, tunawachora tu. Najua tutaitwa kuulizwa suluhisho. Tutawakatalia hadi tuone wanalia.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Songea, Ruvuma)