Wazee wa CCM Hai wapania kumg'oa Mbowe

Wazee wa CCM Hai wapania kumg'oa Mbowe

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
Mbowe-18April2015.jpg

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

18th April 2015
Baadhi ya wazee wa jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, wamemwita jimboni humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Danstan Malya, wakimtaka afanye uamuzi mgumu wa kurejea nyumbani, kumkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kinyang'anyiro cha ubunge Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Malya ni miongoni mwa makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaotajwa kutaka kumng'oa Mbowe kwenye kiti chake cha ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Wengine ni Mbunge wa zamani, Fuya Kimbita na Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Elisante Kimaro.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na kiongozi wa wazee hao, Mathew Kimaro, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Boma Ng'ombe.

"Kupitia tamko hili, tunamwomba mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Meru, Dastan Malya, arejee nyumbani ili ashiriki harakati za kulikomboa jimbo hili kutoka mikononi mwa chama kikuu cha upinzani nchini. Tunajua anao uwezo, ndiyo maana tunakwenda pia kumshawishi atangaze nia baada ya CCM kupuliza kipenga," alisema.

Kada wa chama hicho, Mustapha Hassan, mkazi wa Masama, alisema "Tunamshawishi agombee, kwa sababu tunaamini kwamba anao uwezo wa kulikomboa jimbo mikononi mwa Chadema, ambao wameliongoza kwa vipindi viwili vya mwaka 2000 hadi 2005 na baadae mwaka 2010 hadi sasa. Kama hakutakuwa na mizengwe ndani ya chama chetu, Mbowe ataanguka katika uchaguzi mkuu ujao," alisema.

Wazee waliojitokeza kumfuata na kumshawishi Malya ni wa vijiji vya Mungushi, Sanya Station, Rundugai, Mnadani, Machame Kusini, MailiSita na Kalali.

Hata hivyo, Malya alipoulizwa na NIPASHE kuhusu hatua hiyo ya wakazi wa Wilaya ya Hai, alikiri kufuatwa na baadhi ya wazee wakimshawishi kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Uchaguzi Mkuu ujao. "Ni kweli walikuja wazee wa Hai, huku mkoani Arusha na kuniomba niende nikagombee, nikawaeleza kwamba natafakari lakini nikawaahidi kwamba wakati ukifika nitatangaza nia hiyo," alisema Malya.

CHANZO: NIPASHE
 
Hahaaaaaaaaaa Polen wazee, mpen mbowe ushirikiano tu hakuna ccm wa kumtoa hapo, tunza huo uzi wako, muda utapofika utaniambia nilichokuambia, Ntarahamwe kupewa jimbo vigum sana,
 
Hao wazee wa CCM ni wajinga tena wajinga sana, kwa sababu:
1/Shida yao sio maendeleo bali ni CCM tu. Wanachotaka wao ni kuona Hai inaongozwa na CCM basi.
2/Yaani wameshindwa kujiamini wao wenyewe au kumwamini kijana yoyote wa CCM inayeishi Hai mpaka wakambembeleze mtu anayeishi nje ya Hai aje kuwakombolea jimbo lao.

Kwa mwendo huo CHADEMA itatawala Hai mpaka wajukuu na vitukuu vya hao wazee wa CCM.
 
Tumemchoka Bw. Mbowe, ameamua atusaliti watu wa jimboni kwake, tulimwamini sana tukampa ubunge, lkn kaamua atutelekeze, sidhani kama kuna mwanaHai anayeweza kumpa kura oct. Hana cha kutuambia
 
Nia ya hao wazee ni kukomboa jimbo kutoka upinzani na siyo maendeleo?
Hahaha kuwa na wazee Kama hao kwenye jamii ni hasara, labda wawe ni wazee wa ccm hao.
 
Mbowe-18April2015.jpg

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe

18th April 2015
Baadhi ya wazee wa jimbo la Hai, mkoani Kilimanjaro, wamemwita jimboni humo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Danstan Malya, wakimtaka afanye uamuzi mgumu wa kurejea nyumbani, kumkabili Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kinyang'anyiro cha ubunge Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Malya ni miongoni mwa makada watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wanaotajwa kutaka kumng'oa Mbowe kwenye kiti chake cha ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Wengine ni Mbunge wa zamani, Fuya Kimbita na Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Elisante Kimaro.

Uamuzi huo ulitangazwa jana na kiongozi wa wazee hao, Mathew Kimaro, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Boma Ng'ombe.

"Kupitia tamko hili, tunamwomba mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Meru, Dastan Malya, arejee nyumbani ili ashiriki harakati za kulikomboa jimbo hili kutoka mikononi mwa chama kikuu cha upinzani nchini. Tunajua anao uwezo, ndiyo maana tunakwenda pia kumshawishi atangaze nia baada ya CCM kupuliza kipenga," alisema.

Kada wa chama hicho, Mustapha Hassan, mkazi wa Masama, alisema "Tunamshawishi agombee, kwa sababu tunaamini kwamba anao uwezo wa kulikomboa jimbo mikononi mwa Chadema, ambao wameliongoza kwa vipindi viwili vya mwaka 2000 hadi 2005 na baadae mwaka 2010 hadi sasa. Kama hakutakuwa na mizengwe ndani ya chama chetu, Mbowe ataanguka katika uchaguzi mkuu ujao," alisema.

Wazee waliojitokeza kumfuata na kumshawishi Malya ni wa vijiji vya Mungushi, Sanya Station, Rundugai, Mnadani, Machame Kusini, MailiSita na Kalali.

Hata hivyo, Malya alipoulizwa na NIPASHE kuhusu hatua hiyo ya wakazi wa Wilaya ya Hai, alikiri kufuatwa na baadhi ya wazee wakimshawishi kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Uchaguzi Mkuu ujao. "Ni kweli walikuja wazee wa Hai, huku mkoani Arusha na kuniomba niende nikagombee, nikawaeleza kwamba natafakari lakini nikawaahidi kwamba wakati ukifika nitatangaza nia hiyo," alisema Malya.

CHANZO: NIPASHE

Kwani huko CCM mtu huwezi tangaza nia bila kuombwa na watu au wazee ? Naye huyo jamaa bora aendelee na kazi yake maana Mbowe atamwacha kwa mbali sana .Hao ni wazee wa magazeti ya Nipashe labda lakini kiuhalisia wazee wa CCM wanajua uzito wa kusimama na Mbowe jukwaani .
 
Tumemchoka Bw. Mbowe, ameamua atusaliti watu wa jimboni kwake, tulimwamini sana tukampa ubunge, lkn kaamua atutelekeze, sidhani kama kuna mwanaHai anayeweza kumpa kura oct. Hana cha kutuambia

Amesaliti kipi labda kwa mfano, hivi unaanzaje mtu mzima kama wewe kudai kutelekezwa? llazima hauko sawa kichwani wanatelekezwa watoto.
 
Hao wazee wa CCM ni wajinga tena wajinga sana, kwa sababu:
1/Shida yao sio maendeleo bali ni CCM tu. Wanachotaka wao ni kuona Hai inaongozwa na CCM basi.
2/Yaani wameshindwa kujiamini wao wenyewe au kumwamini kijana yoyote wa CCM inayeishi Hai mpaka wakambembeleze mtu anayeishi nje ya Hai aje kuwakombolea jimbo lao.

Kwa mwendo huo CHADEMA itatawala Hai mpaka wajukuu na vitukuu vya hao wazee wa CCM.

Sema mengine si kuwaambiwa wazee wajinga haipendez
 
Hilo umelitunga hakuna mzee mwenye akili timamu akaongea ujinga kama huo mlitoza kodi kubwa magari ya wagonjwa ili mbowe ashindwe lkn yote mkashindwa sasa umekuja na wazee wazee gani hao zaidi ya kutunga uongo.
 
Ina maana kuwa CCM imechokwa kiasi hiki,hakuna anae taka kugombea kupitia chama hicho kwa hiyari yake mwenyewe mpaka ashawishiwe?.
 
Tumemchoka Bw. Mbowe, ameamua atusaliti watu wa jimboni kwake, tulimwamini sana tukampa ubunge, lkn kaamua atutelekeze, sidhani kama kuna mwanaHai anayeweza kumpa kura oct. Hana cha kutuambia

Ina onekana hata kura hukumpa Mbowe wewe,haya endeleeni na ukiguu na njia wenu kwenda kuwashawishi wagombea wa chama chenu.

Maana yake sasa hivi CCM imechokwa na hakuna anae taka kugombea kupitia chama chenu kwa hiari yake mwenyewe mpaka ashawishiwe.

Lakini wale wote wanao shawishiwa kugombea wakikubali kugombea kupitia CCM watambue kuwa wamejipalia mkaa,watashindwa kwa aibu.
 
kwakawaida wananchi wa HAI wanaangalia umefanya nini na sio ww ni chama gani.Ukijaribu kurudi nyuma utaona HAI imekuwa ikiongozwa na vyama tofautitofauti kudhihirisha kwamba wanachagua mtu kutokana na anavyofanya na si chama
 
Malya kufuatwa ni sawa!Lowasa kufuatwa si sawa!ndani ya chama hichohicho dah!nachanganyikiwa
 
coxM89557 said:
Malya kufuatwa ni sawa!Lowasa kufuatwa si sawa!ndani ya chama hichohicho dah!nachanganyikiwa

Mwaka huu tutashuhudia mambo mengi sana
 
Hizi ni kelele za chura hazimzui tembo kunywa maji.
 
Back
Top Bottom