Pia ukumbuke kuwa ndani ya chadema kuna wizi na upigaji wa pesa za michango ambazo viongozi wa chadema wanagawana na kwenda kuzifanyia anasa night club na madem
- Tunachokijua
- Madai
Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikiambatanishwa na Kichwa cha habari "Mpasuko mkubwa, wazee wabwaga manyanga CHADEMA" ambapo anaonekana Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Unguja Hashim Juma akisema wao baraza la wazee wamejitoa kutokana na mbinu chafu walizopanga CHADEMA baada ya kuona wangeruhusu uchaguzi ufanyike wasingeshinda.
Je, ni upi uhalisia wa Video hiyo?
JamiiCheck imejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kwa kukata na kuunganisha vipande isivyostahili huku video hiyo ikiwa ya mwaka 2019 na si 2026.
Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia Google Reverse image search umebaini picha ya Juma Hashim iliyoambatana na taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya The Citizen Novemba 08, 2019 ambapo Baraza la Wazee la Chadema liliwataka wanachama wa chama hicho kutotoa ushirikiano wowote kwa viongozi wa serikali za mitaa waliochaguliwa Novemba 24, 2019, baada ya chama hicho kuamua kususia uchaguzi huo.
Aidha kwa kutumia maneno muhimu (keywords search) kupitia neno "CHADEMA" JamiiCheck imetafuta taarifa kuhusu chama hicho hasa baraza za wazee siku ya tarehe 08, Novemba 2019 ambapo ilibaini video iliyochapishwa na Millard Ayo YouTube ikiwa na kichwa cha habari "CHADEMA WAZUNGUMZA KUJITOA UCHAGUZI MDOGO, CCM WANATUOGOAPA"
Katika video halisi Hashim Juma aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la wazee wakati huo alikuwa akitoa kauli ya baraza hilo kufuatia tamko la mwenyekiti wa chama hicho taifa kujitoa kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa 2019, ambapo Hashim alibainisha kuwa walizazimika kujitoa kutokana na Mbinu chafu za chama tawala CCM