Wazazi wetu hawataki tuwe pamoja

Wazazi wetu hawataki tuwe pamoja

ionosphere

Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
25
Reaction score
3
Wenzangu mnisaidie nipo njia panda nina mchumba wangu ambaye tulikubaliana kuoana baada ya miaka 3 na sasa imebaki miezi saba tu kiukweli nampenda kwa dhati naye pia ananipenda kama anavyodai kwa sababu siwezi kuusemea moyo wa mtu ila kwa mtazamo wangu mimi naona pia ananipenda japo sina uhakika sana.

Sasa huyu mpenzi wangu n jirani yangu hivyo wazazi wetu wanafahamiana.

Makwazo yakaanza baada ya wazazi wangu kufahamu mwaka mmoja tu ndani ya mahusiano yetu sababu mwanamke ni muislamu na pia kubwa zaidi wanasema wanahofia uchawi kwa kuwa bibi yake mzaa mama wa mpenzi wangu alikuwa mchawi na wakanikanya nisiendelee nae.

Ila sikuwasikiliza na baada ya muda nae mpenzi wangu akasikia kwamba nmekatazwa nisiendelee nae, akaniulza swali moja kwamba linasema wewe unawasikilza wazazi wako au unafanya maamuzi yako nikamjibu mimi lazima nikuoe sitawasikilza naye akanijbu nami sipo tayari kukuacha hata kama ni bila harusi.

Wanajamiiforums tukaendelea na mahausiano yetu mpaka sasa hivi karibuni Mpenzi wangu kanipa taarifa za kunichoma moyo kwamba nae mama yake kamwambia akikubali kuolewa na mimi ahesabu hana wazazi na hawatakaa wamuelewe na sababu zao ni kwamba mimi mkristo na pia sisi majirani wa karibu mno kwa hiyo haitapendeza yeye aolewe karibu na nyumbani, na mpenzi wangu nae anasema hata kama wazazi wake hawataki yeye ni lazima aolewe na mimi.

Ila mimi naona giza tu hata pa kuelekea sioni jamani ushauri wenu ni muhimu nipo njia panda kwa nyongeza mpenzi wangu anamalizia chuo mwakani na mimi mfanyakazi kampuni fulani hivi.
 
Pole Sana Kijana
Unataka Nikushauri Nini Sasa?
 
Mi nahisi nina ushauri mzito sana wa kukupa...........lakini sijakuelewa ulivyoandika..........ni kiswahili........?
 
Ndoa zakulazimisha kama hizi mwisho zinatoa products za ajabu sana....
 
Achananen tu maana wazazi wa pande mbili wote hawajaridhia, ila ingetokea upande mmoja umeridhia hapo ilikuwa rahisi, sasa wote wamegoma mtaegemea wapi nani atawafariji? hebu fikirien mara mbili hapo tuone
 
Xaxa wewe na majnga yako yote hayo lkn hjui kndka xixi tukxhuri nn? nyambafuuu.
 
Aisee! Wazazi wa pande mbili wanainfluence kubwa sana ktk mapenzi ya watoto wao.

na hao wazazi wenu wanasababu za msingi kukutaa ndoa hiyo.

nawashauri muwache utotona muweze kudhibiti nye.ge mshindo zenu. maana hapo kinachowapeleka ni nye.ge tu! mwisho wa siku nyeg.e zinaisha mnaanza kukwaruzana na suluhisho inakua wazazi.

You must know that kukwaruzana ktk ndoa ni jambo lisiloepukika hata hao wazee wakiridhia ndoa hiyo.

point ni kwamba, wazazi kama wasuluhishi no 1 wanaweza kuwa adui.

ukumbuke matatizo hujengwa kwenye akili. tatizo likitokea inakua ni kivuno kwa ile mbegu iliyoekwa pale. kwa mantiki hiyo, hapo matatizo yameshajengwa ktk intended marriage.

Ndugu ndoa ni taasisi nyeti kuliko nyeti uzifichazo.

nakushauri usioe huyo mwanamke.
 
Hakuna ndoa hapo maana waafrika tuna oa/kuolewa kwaajili ya familia zetu!

Hivyo kama huna baraza za wazazi huwezi kuoa au kuolewa! Tafuta mwanamke mwingine! Asikudanganye mtu kuwa unaweza kuo/kuolewa bila baraza za familia au wazazi wako!
 
Back
Top Bottom