Wazazi watakiwa kuacha ukatili dhidi ya watoto

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Afya nchini Tanzania, Dk Doroth Gwajima amewataka wazazi kuacha ukatili kwa watoto ili kuwanusuru dhidi ya saratani ikiwemo ya ubongo.

Ameeleza hayo leo Alhamisi Februari 4, 2021 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya saratani duniani katika viwanja vya hospitali ya rufaa Kanda ya Bugando jijini Mwanza,

Watu zaidi ya 200 wamepatiwa saratani kwa siku mbili bila malipo.

Katika maelezo yake, Dk Gwajima amesema kuna haja ya wazazi kuangalia mienendo na malezi ya watoto wao ili kuepuka utoaji wa adhabu zinazoweza kuwasababishia athari za kisaikolojia.

"Yaani usije ukafikiri sisi wote tukikutana tuna afya njema ya akili, tunaweza tukawa hatuumwi malaria hatuna presha lakini tuna matatizo ya afya ya akili, hebu kwenye jamii tunayoishi tuangalie mienendo ya watoto wetu tukianzia wakiwa wadogo, akikushinda kumpiga na kumletea machungu mtoto akiwa mkubwa atakuwa katili huyo," amesema Dk Gwajima.

Amewataka viongozi wa dini kufufua mifumo ya uadilifu kwenye jamii ili kusaidia kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na ukatili dhidi ya watoto.

"Changamoto za maisha ni nyingi kila mtu anazipitia mwingine akiona mwenzake anakula nyama kwa wingi anamuonea wivu wewe kula mboga za majani ndiyo zinakusaidia kukuepusha na magonjwa ya saratani, pia lazima tuwalee watoto wetu kwenye mfuko wa kuridhika ili kuwaepusha na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani," amesema.
 
Back
Top Bottom