Wazazi wasimamie Watoto katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,115
2,000
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka Wazazi kuwasimamia watoto katika matumizi ya vifaa vya kielektroniki ili kuwaepusha kujiingiza katika vitendo vya ngono na ukatili mwingine mitandaoni

”Watoto wanafikia hatua kutaka kujiua kwasababu wanakutana na Watu mitandaoni wanawasema vibaya”

Ummy ameyasema hayo Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishiwa June 16 kila mwaka

”Watoto wanatumia vifaa vya kielektroniki ikiwemo simu na kompyuta kujifunzia, ni vizuri wazingatie matumizi sahihi ya vifaa hivyo ili kuepusha kufanyiwa vitendo vya kikatili”

“Katika eneo la malezi ya Watoto wetu bado kuna changamoto kubwa ya matumizi ya mitandao tuhakikishe tunawasimamia Watoto wetu wasijiingize katika masuala yasiyofaa katika mitandao hiyo, Watoto wakiwa nyumbani katika kipindi hiki wajiepushe kwenda kwenye maeneo yatakayohatarisha usalama wao, ikiwa pamoja na kubakwa, kulawitiwa, kushawishiwa kufanya ngono na hata kupata maambukizi ya corona”-

UMMY
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,898
2,000
Kwa upande wa Teknohama kwa watoto wetu hapa africa kuna changamoto sana sana, pasi usimamizi au usiwepo juu ya hii kitu ni shida.
 

Babu Kingo

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
432
250
Ummy ameyasema hayo Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishiwa June 16 kila mwaka
MUHESHIMIWA DADA UMMY TUMEKUSIKIA NA KUKUELEWA ASANTE SANA, TUNAOMBA PIA WIZARA INAYOHUSIKA NA UTAMADUNI KUENDELEA KUENZI TAMADUNI ZA KIMAADILI YA MTANZANIA NA KUWEKA VIDHIBITI DHIDI YA TAMADUNI ZA KIMAGHARIBI KWANI NI HATARISHI KWA NYAKATI TULIO NAO. SHUKRAN.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom