Wazazi wanapoingilia penzi

Kama una amini kuwa kuheshimu wazazi kunaongeza baraka pale wanapokupinga au kukushauri chukua muda kufanyia kazi ushauri wao. Ndoa ni mapenzi moto moto mwanzo kuna ups and downs baadae. Sasa kama ulioa/olewa kwa mbwembwe na jeuri ndio wale mtu ananyanyasika lakini anakomaa kwani anahisi akiwambia wazazi na ndugu watamcheka kuwa walimwambia akawaona machizi.

Raha sana ukioa/olewa na mtu ambaye wazazi wamemkubali. Wakipinga vuta muda utaanza kuona wanayosema kama umevuta muda na bado waona he/she is the one oa/olewa. Mimi nina mpaka marafiki zangu wanakiri kuwa waliambiwa na wazazi wasiolewe na waume walionao. Sasa hivi wanaliona joto la jiwe na hawathubutu kushare na ndugu zao matatizo walonayo.

hapo kwenye kuvuta subira iwapo wazazi wamemkataa mkwe ni ushauri mzuri sana NK.
Ukivuta muda kama kuna lolote baya kuhusu mtarajiwa wako litadhihirika tu.
Inaumiza mara mbili inapotokea umelazimisha kufanya jambo halafu hilo jambo likaleta -ve impacts. Ni aibu na ni ngumu kushare hayo matatizo.

Nimeshangaa kumuona Mkuu Mbu jamvini mwezi huu wa toba. Huwa anachukua likizo na kuingia hapa kwa nadra sana mpaka mwezi mtukufu unapomalizika.

• Thanks
Reactions: Mbu
habari zenu wana jamiii
nimekua nikiobserve mara nyingi inapofikia hatua ya watu kufunga ndoa wazazi huingilia kati either kumshauri mwanao aachane na mchumba wake au asifanye mambo kwa pupa....
swali linaloniumiza ni kwamba kama ww ni kijana na umeshazoeana na mtu wako ukaridhika nae wazazi wanapokwambia umwache au hafai je utachukua uamuzi gani....keep in mind to establish another new relationship takes time and energy:thinking:

Ni swala ambalo ni gumu na linatatiza na kusumbua na kuleta kuvunjika moyo maana unakuwa umeestablish a relationship for as long as u can and unafikia unataka kuoa vigenge vinaanza kumjadili mwenza wako kuwa yuko hivi na hivi au usipaparike sana kumuoa au subiri kwanza

Japo yapo ambayo wazazi wanaweza wakawa wameyaona mapungufu ila nafikiri uamuzi wa nani aolewe au aoe waachiwe wale ambao wamechaguana maana wanajua ups and down za kila mmoja. Na by the way hao waliochaguana ndio watakaoenda kuanzisha mji wao na kukaa kivyao sidhani kama wale wasemaji watakuja kuwasaidia yakiwashinda na sana sana watakuwa wanachekea pembeni
So ifikie mahali kama mtu amechagua partner wake aachwe yeye mwenyewe anayajua mapungufu ya mwenzake na ameshayakubali na ataenda nayo. Kama ni mzigo kashaamua kuubeba mwenyewe na anajua ataufikisha wapi.

• Thanks
Reactions: Mbu
Ni kweli Husninyo, Wazazi wana nia njema na mtoto wao, lakini wakati huo huo mara nyingi hawataki kutafuta muda wa kumfahamu muhusika kama anastahili kupewa baraka zao za kumuoa/kuolewa na kijana wao. Siku hizi watoto wengi ni vichwa ngumu mara nyingi Wazazi wanapoweka vikwazo mtoto huamua kusonga mbele bila baraka zao. Na mara nyingi wapenzi hawa huweka extra efforts katika ndoa yao ili kuwaonyesha Wazazi kwamba walikosea walipoweka pingamizi bila hata ya kutafuta muda wa kumfahamu mkwe wao vizuri. Na ndoa ikifanikiwa basi wanakuwa hawana jinsi bali kuikubali ndoa ile. Wazazi wengine wanakuwa wastaarabu na kukubali makosa yao kwa wanandoa hao na wengine wanaminya tu.

binafsi naona wazazi wanakosea namna ya kufikisha ujumbe either wawe na nia njema au mbaya katika hilo suala. Kama
Wazazi wameona wakwe zao wana matatizo na hawafai watumie namna nzuri ya kufikisha ujumbe ili isilete conflict baina yao.
Wasifanye mambo kwa chuki/ubaya maana mwisho wake ni aibu.
Kama NK alivyoshauri inapotokea suala kama hilo kujipa muda zaidi ni muhimu na sio kwa mtoto tu hata mzazi ikibidi apewe muda aweze kumuelewa mkwewe.... Hiyo yote ni katika kutafuta baraka za mzazi..

Hahahahah BaK sio kwamba bado mfungo haujachanganya?! usije ukatufukuzia bwana tutaanzisha mathread ya kumsaka mpaka arudi

Ngoja nijimanyazie mie nisije nikabebeshwa lawama bure za kupotea kwa Mkuu Mbu halafu watu wakakonda, kushindwa kula na hata kulala kisa Mbu kaingia mitini JF hahahahahah lol!

Kuna kitu ambacho wazazi wengi hawafanyi. Unatakiwa uwe na muda wa kukaa na watoto wako na kuwapa ushauri wa maisha including the ideal husband and wife. Sasa in most cases wazazi hawasemi wansubiri suprises afu ndio walete masharti yao. Najua huwezi sema yote maana utakuwa un restrict uhuru wa mtu lakini kuna mambo ya msingi. Kama una amini kuwa si vizuri kumix dini mwambie mwanao toka akiwa mdogo inasaidia sana kumfanya afanye maamuzi sahihi. Mimi mfano baba yangu alikuwa anatuambia wanangu mimi hata umlete nyumbani billionea as long as hajaenda shule kwa kweli sita approve. Kwa hiyo wote tulilijua hilo kuwa baba wala amind ma businessmen anataka mwanaume msomi kwa sababu anasema elimu ni lifetime insurance hata sisi alisisitiza tusome. Alikuwa anawaponda sana watu wenye pesa bila elimu including ndugu zetu ili kutupa mifano hai kuwa maisha bila elimu yanakuwa ni ya hovyo hovyo. Alikuwa anatupeleka muhimbili tuone wanafunzi wa kike wa udaktari na kutuambia ona hawa wadada they are beutiful and they got brains too. Hivyo jamani nasi kama wazazi tuwe mentors kwa watoto na kuwa tune tunavyotaka si kujakugombana mwisho wa safari kwa kosa la kutowaeleza tupendacho mapema.

...lol, kaka BaK umenipiga dongo la kishkaji ha ha..
Haya bana, acha nimalizie futari hapa niandae majibu.

Nyumba kubwa, kwa mtazamo wako Elimu na Kipato
Vinanafasi gani mshenga anapoleta mahari kwenu.

lol nakumbuka mie nliambiwaga mbona mko tofauti? nikawajibu 'My love for him conquers all'.........mh!! yalokujankuta sikuthubutu kwenda kusema!

...lol...wamaasai wa chalinze, wanyamwezi na wamanyema wa Zanzibar, waarabu wa pemba,
wachaga wa Tanga, wote watanzania hao, acheni kutunyanyapaa..

Kuna wazazi wao hugoma bila kutoa sababu watoto Wasioane.
Kumbe walishaharibu, anaogopea siri italipuka. Hii nayo imekaaje?

Nipeni mifano ya ukweli mzazi alipokataa alitoa sababu
Zipi, mambo ya "basi tu huyu simtaki" mimi mbado kukubali. Kila ndoa ina ups and downs zake, wengine
Walioana kwa baraka zote, na ndoa hazikudumu.

Marafiki na ndugu nao wasikilizwe?

lol nakumbuka mie nliambiwaga mbona mko tofauti? nikawajibu 'My love for him conquers all'.........mh!! yalokujankuta sikuthubutu kwenda kusema!

Tofauti kivipi mwj1, lol..kwani ni uniform mpaka mfanane?

...lol...wamaasai wa chalinze, wanyamwezi na wamanyema wa Zanzibar, waarabu wa pemba, wachaga wa Tanga wote watanzania hao, acheni kutunyanyapaa..

Kuna wazazi wao hugoma bila kutoa sababu watoto
Wasioane. Kumbe walishaharibu, anaogopea siri italipuka. Hii nayo imekaaje?

Nipeni mifano ya ukweli mzazi alipokataa alitoa sabcu
Zipi, mambo ya "basi tu huyu simtaki" mimi mbado kukubali. Kila ndoa ina ups and downs zake, wengine
Walioana kwa baraka zote, na ndoa hazikudumu.

Marafiki na ndugu nao wasikilizwe?

Hahaahahah Mbu hayo makabila itanibidi nirudi darasani nikasome tena......so unataka kusema hatuna tena yale makabila 120 sijui tulokuwa tunaambiwa? hahahah kumbe hata sie tuna point five eh!.............. ngoja nami nimtafute mwanangu awe point five. lol Mnyamwezi/Mmanyema wa Zanzibar!!

Ah Mbu bwana concern inawekwa kwa mzazi mama au baba.....hao wengine wasipotoa sababu yenye ushahidi.....wapotezee tu!!

Tofauti kivipi mwj1, lol..kwani ni uniform mpaka mfanane?

Lol ofkoz waliitaja tofauti ile but kwangu haikuwa tatizo na hata katika maisha yetu hilo tatizo lililotajwa haikuwahi kuwa mmojawapo la chanzo cha kutosikizana...........

Lol ofkoz waliitaja tofauti ile but kwangu haikuwa tatizo na hata katika maisha yetu hilo tatizo lililotajwa haikuwahi kuwa mmojawapo la chanzo cha kutosikizana...........

..lol, there you go... Wao wanaangalia mtazamo wa nje ya boksi tu. Mwj1, nikija kwenu na wazazi wako wakisema "huyu hutamuweza!" kidogo nitapata mashaka. Sio wazazi wangu eti ndio wakukatae..

Jol, there you go... Wao wanaangalia mtazamo wa nje ya boksi tu. Mwj1, nikija kwenu na wazazi wako wakisema huyu hutamuweza, kidogo nitapata mashaka. Sio wazazi wangu eti ndio wakukatae..

Hapo kwenye Red- Utapata mashaka ya nini? kuwa wananiingilia uhuru wangu au??
Hapo kwenye Blue kama sijakuelewa vile..!! unataka kusema inaeleweka iwapo atakayekataliwa na Mwanamke au? mh hebu nijiandae na kukataliwa!! hahahahaahaaaaaaaaaaaa kama sijawapatia sababu nyingine ya kukukatalia (kichaa!)

...lol, mwj1 acha hizo.
Haijalishi mume au mke, wazazi wanaweza
Kumkatalia muoaji au muolewaji.

Mashaka ni pale nakuja kwenu ukweni kisha
Wazazi wa mke wananambia "..huyu hutamuweza
Usijekutulalamikia, wenyewe tumemshindwa!"...

Hapo inabidi niiangalie hiyo familia kulikoni.

Jamaa yangu alipewa sababu kama hizo, mpaka leo yupo na mkewe,
mke kawa mpole na adabu zake.
'Kila shetani na mbuyu wake,' au sio?

...lol, mwj1 acha hizo.
Haijalishi mume au mke, wazazi wanaweza
Kumkatalia muoaji au muolewaji.

Mashaka ni pale nakuja kwenu ukweni kisha
Wazazi wa mke wananambia "..huyu hutamuweza
Usijekutulalamikia, wenyewe tumemshindwa!

Hapo inabidi niiangalie hiyo familia kulikoni.

Jamaa yangu alipewa sababu kama hizo, mpaka leo yupo na mkewe, mke kawa mpole na adabu zake.
Kila shetani na mbuyu wake, au sio?

.................hahahahah eti wazazi wako wanakususa jamani ah hapo hata mie sina budi kusikiza....

• Thanks
Reactions: Mbu
...lol, afadhali umeridhika na jibu langu, duuh. Nilijua nishaharibu, pheeewww....

Similar Discussions

Back
Top Bottom