Wazazi wamkataa kisa kabila, hivi ukabila utaisha lini?

faith lady

Member
May 26, 2017
41
16
Habarini wadau,

Nina rafiki yangu alikuwa na mchumba wake wanapendana sana so akaenda kumtambulisha kwao wazazi hawamtaki huyo binti kwa sababu ya kabila lake ameumia sana ni binti aliyejitunza na ana hofu ya Mungu na amemsubiria huyo mchumba wake muda na akawa mwaminifu leo yule kaka amekata mawasiliano na yule dada.

Please nishaurini nimsaidiaje, mpaka ameanza kuchukia kabila.
 
Simple nasepa zangu nakwenda kutafuta mwingine....ukabila ni tatizo asee
Thanx kwa ushauri ila inaumiza mnoo usiombe ikukute..hii tabia ya watu kugeneralize tabia ya mtu mmoja na wengine wako hivyo sio nzuri unakuta inawaharibia wengine wa kabila kama hilo jaman watanzania tubadilike tunaumoza watu ambao hawastahili
 
Kweli kabisa ukabila ata mm siupendi ni mambo ya dunia ukiwa na hofu na Mungu ndani yako uwezi kufikiria mambo ya kabila
Yaani na unaumiza watu wasiostahili hivyo mpaka kuna kabila ukifikiria kwenda kutambulishwa unaanza kuogopa jinsi watu wanavyogeneralize tabia ya mtu wa hilo kabila na kuwadhani wote ni wabaya
 
Ukabila na udini ni matatizo yanayoikumba hii nchi lakini hayasemwi.

Ipitishwe sheria Kali ya kuwaadhibu wote watakaoonesha viashiria vya udini na ukabila.

NB kama unaoa ama kuolea, unatakiwa kuwapa ndugu zako taarifa ya maamuzi yako ya kuishi na uliyemchagua na siyo kuwataka ushauri.
 
Thanx kwa ushauri ila inaumiza mnoo usiombe ikukute..hii tabia ya watu kugeneralize tabia ya mtu mmoja na wengine wako hivyo sio nzuri unakuta inawaharibia wengine wa kabila kama hilo jaman watanzania tubadilike tunaumoza watu ambao hawastahili
Kweli kabisa pia unakuta mtu kama hivy ushampenda kwa dhati ukabila mara dini vinaingilia kati.Ukabila na dini ni maisha ya ndani kabisa ya nafsi ya mtu mara nyingi huathiri sana maisha ya nje ya mtu
 
Ukabila na udini ni matatizo yanayoikumba hii nchi lakini hayasemwi.

Ipitishwe sheria Kali ya kuwaadhibu wote watakaoonesha viashiria vya udini na ukabila.
Thanx..ila me naona sisi wenyewe ndo tunasababisha kuna wengine wanasema kabisa labda kabila lile ni baya wanauwa watu na haifai kuolewa binti wa hilo kabila na kumbe sio kweli na kila mtu anatabia yake alivyoumbwa nayo..hii tabia ya kugeneralize tabia za watu na kusema vibaya makabila ya watu bila uhakika kusumbaza uzushi tu inatesa sana watu usiombe ikukute
NB kama unaoa ama kuolea, unatakiwa kuwapa ndugu zako taarifa ya maamuzi yako ya kuishi na uliyemchagua na siyo kuwataka ushauri.
 
Mie mwenyewe nishakosa mume kisa elimu yangu au Massimo yangu..hivyo mapenzi yana baguliwa na elimu,kabila na dini...
 
Tatizo tuna generalize kumbe kila mtu ana mfano wake
Kweli kabisa stela usiombe ikukute inaumiza mnoo .mimi pia ilishawahi nitokea nililia mnoo ila baadaye nilimwachia Mungu nashukuru ananipigania naendelea vizuri..ndo maana huyu rafiki yangu najitahidi kumshauri asikate tamaa hakuwa wakwake huyo ila inakuwa ngumu sana kwake amekataa tamaa kabisa na anaona umri umeenda yaani Mungu amsaidie tuu
 
Inawezekena alikuwa amemchoka,akamtafutia sababu kupitia kwa ndugu zake
 
Habarini wadau..na rafiki yangu alikuwa na mchumba wake wanapendana sana so akaenda kumtambulisha kwao wazazi hawamtaki huyo binti kwa sababu la kabila lake ..ameumia sana ni binti aliyejitunza na ana hofu ya Mungu na amemsubiria huyo mchumba wake muda na akawa mwaminifu .leo yule kaka amekata mawasiliano na yule dada..pls nishaurini nimsaidiaje mpaka ameanza kuchukia kabila

Pole kwa kupatwa na matatizo, ila usikate tamaa.
Hongera kwa kujitunza, vijana wapo humu watapiga hodi huko ofisini muda si mrefu, Washakusona.
 
Inawezekena alikuwa amemchoka,akamtafutia sababu kupitia kwa ndugu zake
Sidhani kwa sababu hata wazazi wake walivyomkataa huyo binti aliwaomba sana kuwa ni binti anayempenda na hawezi oa mwanamke mwingine ila wazazi wakakataa kabisa na wakasema akimuo huyo binti hawamtambua tena kama mtoto wao ..
 
Back
Top Bottom