gfsonwin
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 18,272
- 20,683
Nimeikuta hii Yahoo, nikamua kuitafsiri tu mjue dunia ina mambo yake.
Baada ya kupoteza watoto wao saba kwenye janga baya na kubwa sana la moto, miaka 5 iliyopita, Janelle na Ted Clouse wanaendelea kuijenga upya familia yao huku wakiwa na kumbukumbu za watoto wao wapendwa waliofariki.
Ilikuwa usiku wa kuamkia tarehe 8 mwezi March, pale moto mkubwa ulipozuka katika nyumba ya Janelle na Ted iliyoko Pennyslaviana, moto ambao uligharimu maisha ya watoto saba kati ya watoto 8. Janelle na Ted pamoja mtoto wao Leah (3) aliyenusurika kufa, waliachwa wakiwa hawana nyumba ya kuishi ndani ya majonzi makubwa sana ya kuondokewa na wanafamilia wenzao saba
Baada ya miaka kadhaa ya majonzi na huzuni nyingi Janelle na Ted walianza kupona majeraha yao na kuanza kuijenga upya familia yao.
"maisha hayawezi kuwa sawa" Janelle aliwaambia waandishi wa habari.
Kwasasa, familia ya Clouse inaungana tena na maisha ya furaha na upendo, toka moto huo ugharimu maisha ya watoto wao 7. Ted na Janelle wamefanikiwa tena kupata watoto 4 na sasa wanajiandaa kumpokea mtoto wa 5.Janelle anategemewa kujifungua mtoto wa kiume mwezi April.
'Mapema tu nitakuwa nawaambia watu nilibahatika kupata watoto 13" Janelle alisema huku akiwahesabu hadi wale aliowapoteza kwenye ajali ya moto.
Wanandoa hawa wanakumbuka kila tukio lililotokea siku hiyo ya usiku wa mwezi march, na kukubali kwamba watoto wao walipoteza maisha.
" Hakuna aliyekuwa anaishi ndani, isingewezekana" alisema Ted toka siku alipokuwa naona moshi mweusi ukifuka toka ndani ya nyumba yake.
Christina, 11, Isabelle, 9, Brady, 7, Hannah, 6, Heidi, 4, Miranda, 18 miezi, na Samantha, 9 miezi, walipoteza maisha yao siku hiyo.
Iligundulika kuwa watoto hao walizidiwa na gesi ya carbon monoxide na sumu ya moshi wenyewe iliyoingia kwenye mapafu yao.
Wataalamu wa masuala ya moto bado hawajaweza kujua nini chanzo cha moto huo, ila kuna hofu kwamba Miranda aliyekuwa na miezi 18 alibeba blanket lake la kujifunika baridi karibu na moto uliokuwa umewashwa ili kuondoa baridi ndani na baadae alilibeba blanket hilo hadi sebuleni na kuliweka kwenye makochi.
Wakati moto huo ukianza Janelle alikuwa mjamzito, na alikuwa nje ya nyumba anahudumia ng'ombe wake na mumewe, Ted ambaye huuza maziwa alikuwa amekwenda mashambani kukusanya maziwa. Janelle anadai kwamba mabinti zake wakubwa ndio waliokuwa wakiwaangalia wadogo wao kama ilivyo kawaida yao.