Wazazi Wakati mwingine mnatukosea sana

Aluwatan

JF-Expert Member
Apr 7, 2023
267
573
Jamani WanaJF ushauri naombeni maoni yenu.

I will be 27 by November niko na mtu anaenijali Sana Sana, he loves me kwakweli lakini eti mzazi wangu hususani baba hamtaki sababu ni muisilam na kabila yake na eti sababu hajasoma lakini ni mtu na biashara zake na maisha yake anajiweza tu.

Jamani baba yangu hamtaki, hataki kutoa ridhaa anioe hataki kuniozesha kwake hataki nibadili dini anatamka maneno ya laana sana kama mimi nitakua nae yaani anaongea mpaka anapitiliza na mimi nimeridhia kuwa naye yule mtu kuanzia tabia hadi mwenendo wake, na hata kufuata dini yake, na sina sababu ya kuachana nae hajanikosea Wala sijamkosea mtu wawatu jamani.

Hivi mkiangalia mzazi wangu ananitendea haki kweli au anataka nizeekee nyumbani nifanyeje jamani mimi nipo kwenye Wakati mgumu sana, naombeni ushauri wenu.
 
Acha kuongozwa na mihemko ya mahusiano, baba yako anaangalia mita mia, wewe unahangaika na mita 10, hiyo ndo tofauti ya ujana na uzee, suala la utouti wa Dini kama wewe umelelewa katika misingi ya dini utaona uzito wake, lakin kama wazazi wako ndo wenye dini huwezi kujua.
 
Unaweza usimuelewe Baba yako sasa, ila hiyo safari ya kubadili ni dini ni safari Mbaya na ngumu kuifanya sababu ya mwanaume.

Ukilazimisha utaolewa tu, ila kama waweza msikilize kwa hili, usibadili dini sababu ya ndoa, ndoa zipo tu na sio za kukufanya ugombane na Mzee.
 
Pole bestie, sidhani kama kuna mzazi anayependa mwanae asiolewe au azeekee nyumbani, usionyeshe kua una haraka sana jaribu taratibu na kwa upole kumuelewesha baba yako kua utakua na amani na furaha zaidi ukiolewa na huyo mpenzi wako, wazazi hawapendi watoto wao tuteseke ni hivyo tu.
 
Uhalisia women are terrible in choosing men.

Kwenye familia zote ama jamii zinazojielewa huwa hazimruhusu binti yao ama mwanamke wa familia yao kuchagua mume mwenyewe,,, mwanamke huwa anachaguliwa mume na kaka zake, baba yake ama wajomba zake
 

Attachments

  • 7be253e280b884e63f5d2192dc39a765.mp4
    633.3 KB
Mzee anaweza kuwa sawa kabisa, nakuomba ufuate ushauri wake kwani anajua zaidi ya unavyoelewa wewe

Tatizo hamjui tofauti ya kupenda na kutamani
Leo uko kwenu ila maisha huanza mnapoishi pamoja hapo ndio utajua upendo maana yake
Asikudanganye mtu

Msikilize Baba na wala usimchukie
 
Back
Top Bottom